Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Picha: Raiswa Chile Sebastian Pinera
Baraza la senate la Chile limepinga mchakato ulioanzishwa na upinzani uliolenga kumuondoa madarakani Rais Sebastian Pinera.
Upinzani ulitaka Pinera ang’olewe madarakani kufuatia sakata lililofichuliwa kwenye nyaraka za Pandora na pia kutokana na hatua yake ya kutoshirikiana na bunge wakati mchakato huo dhidi yake ulipoanzishwa.
Waliopiga kura ili rais huyo ambaye ni bilionea aondolewe mamlakani walikuwa 24, idadi ambayo ni chini ya kura 29 zinazohitajika ili mchakato kama huo ufaulu. Na waliopinga kuondolewa kwake walikuwa 18.
Endapo mchakato huo ungefaulu, basi huenda angekabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano gerezani.