Rais wa Colombia apendekeza Cocaine kuhalalishwa duniani kote

Rais wa Colombia apendekeza Cocaine kuhalalishwa duniani kote

Cocaine katika original form yake haina madhara yoyote, Aymara Indians wanatumia kwa maelfu ya miaka.

Kumbuka COCA COLA.
Ipo siku itahalalishwa hata bangi walisema ni mbaya ila now majimbo mengi US si haramu. Nini kimebadilika kama ilikuwa mbaya?
 
Nchi ishakiwa na watu wanao jipatia utajiri kwa njia ambazo si za halali then serikali ikawachia, matokeo ya ndio haya serikali imepoteza control. Wauza poda ndio wamekuwa marole model wa vijana na future yao yao wataitengeza kwa kuwaangalia wao.
Chambua hoja yake usimchambue mtoa hoja hata miaka ya nyuma mtu angesimama na kuongea Hilo kuhusu bangi angeonekana kichaa lakini Leo hii ni kitu Cha kawaida
 
Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amesema biashara ya kokeini inaweza kudhibitiwa kwa urahisi ikiwa dawa hiyo itahalalishwa duniani kote, kwakuwa dawa hiyo si mbaya zaidi kuliko whisky.

Katika mkutano wa mawaziri uliorushwa moja kwa moja, Petro amesema Kokeini ni haramu kwa sababu inatengenezwa Amerika ya Kusini, si kwa sababu ni mbaya zaidi kuliko whisky, akiongeza kuwa wanasayansi wamechambua suala hilo.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 2022, ameahidi kupambana na biashara ya dawa za kulevya na kudhibiti matumizi ya dawa haramu. Hata hivyo, tangu aingie madarakani, uzalishaji wa kokeini nchini Colombia umeongezeka.
Pombe kali(spirits) back in the day zilikuwa haramu na zilisafirishwa kwa magendo sababu walidai zikihalalishwa watu watakunywa Hadi watakuwa wanakufa hovyohovyo Scotland ikiwa kinara wa uzalishaji na usambazaji wa pombe hiyo kwa magendo. Iliporuhusiwa watu wakaanza kuinywa kistaarabu tofauti na ilivyokuwa illegal, ikawa kwenye standards hapajawahi kuwa na shida. Nchi nyingi za Afrika pombe ya gongo si haramu na ndiyo biashara inayowafanya wamama wa vijijini waweze kusomesha watoto na maisha yako kama kawaida. Makampuni ya pombe kali ndiyo hufanya kampeni za kuharamisha gongo kama ambavyo makampuni ya sigara yalivyokuka na kampeni za kuharamisha bangi ambayo babu zetu walivuta bila shida zozote japo sasa nchi nyingi zimeshaanza kuhalalisha.
Point yangu ni kwamba kila kitu huanzia kwenye mindset, cocaine inaweza kuhalalishwa na ikawa regulated haitakuwa na madhara.
 
Ipo siku itahalalishwa hata bangi walisema ni mbaya ila now majimbo mengi US si haramu. Nini kimebadilika kama ilikuwa mbaya?
Bangi haina shida..
Njoo Hapa MHS utuone tunavyowatibu
 
Bangi haina shida..
Njoo Hapa MHS utuone tunavyowatibu
My point ni kwamba hakuna kitu kizuri au kibaya bali ni perception. Kilicho kibaya leo kesho kinaweza kuwa kizuri. Bangi walisema ni mbaya kwa miaka mingi leo huko US wameihalalisha.
Sema vita ya dawa za kulevya haiwezi isha maana sasa tatizo si cocaine tu, kuna methamphetamine ambapo kichaa trump anasema ingredients zake zinatoka china kwenda mexico ili watengeneze hizo drugs wazilete US
 
Chambua hoja yake usimchambue mtoa hoja hata miaka ya nyuma mtu angesimama na kuongea Hilo kuhusu bangi angeonekana kichaa lakini Leo hii ni kitu Cha kawaida
Labda hujaelewa ila wengi wamenielewa. Huwezi fananisha bane na poda ,hata impact yake kiafya ni tofauti.
 
Labda hujaelewa ila wengi wamenielewa. Huwezi fananisha bane na poda ,hata impact yake kiafya ni tofauti.
Lakini yeye anayesema whisk inamadhara kuliko poda Ina maana ni mtazamo tu inategemea unatazama ukitokea angel ipi kwenye angel yake kaona hivo
 
Pombe kali(spirits) back in the day zilikuwa haramu na zilisafirishwa kwa magendo sababu walidai zikihalalishwa watu watakunywa Hadi watakuwa wanakufa hovyohovyo Scotland ikiwa kinara wa uzalishaji na usambazaji wa pombe hiyo kwa magendo. Iliporuhusiwa watu wakaanza kuinywa kistaarabu tofauti na ilivyokuwa illegal, ikawa kwenye standards hapajawahi kuwa na shida. Nchi nyingi za Afrika pombe ya gongo si haramu na ndiyo biashara inayowafanya wamama wa vijijini waweze kusomesha watoto na maisha yako kama kawaida. Makampuni ya pombe kali ndiyo hufanya kampeni za kuharamisha gongo kama ambavyo makampuni ya sigara yalivyokuka na kampeni za kuharamisha bangi ambayo babu zetu walivuta bila shida zozote japo sasa nchi nyingi zimeshaanza kuhalalisha.
Point yangu ni kwamba kila kitu huanzia kwenye mindset, cocaine inaweza kuhalalishwa na ikawa regulated haitakuwa na madhara.
Wakati pombe kali zilipokua ni illegal hatuna uhakika na afya za wale waliokua wakitumia kwa kificho kama waliathirika ama la though tunaweza kufikiri kwa mtazamo kwamba, there was no problem than hisia tu za wana sayansi uchwara wa wakati huo cause wanywa gongo tunao mtaani na hawana tatizo lolote, same as wavuta bangi, tupo nao mtaani, tunafanya nao kazi na hatuoni kama wana shida yeyote, huonekana tatizo tu pale wanapotoka kuvuta/kutumia but baada ya muda fulani wanakua normal tu; issue yangu ipo kwenye hizo dawa za kulevya kama cocoine, madrax nk; watumiaji wa hizo dawa tunaweza kusema eti hazina madhara? Seriously? Si tunao vijana mitaani mwetu na tunaona walivo haribika? Tazama kipaji cha Rehema Chalamila, Chid Benz, Top in Dar (TID) nk jinsi kilivo haribika, wamepotea kabisa hadi kwenye game, hawajulikani anymore, hawana faida kwa familia, jamii hata taifa, wamekua mzigo, sio asset tena. Wapo na vijana wengine wengi tu mitaani kwetu tunako ishi, mbaya zaidi hata wakiacha kutumia dawa hizo, watakaa muda mrefu mno hadi kuja kua sawa, tena baada ya kutumia dawa jingi na gharama kubwa sana. SIUNGI mkono hoja ya Pablo Escobar hata kidogo, dawa za kulevya ziendelee kua HARAMU kwa gharama yeyote
 
Lakini yeye anayesema whisk inamadhara kuliko poda Ina maana ni mtazamo tu inategemea unatazama ukitokea angel ipi kwenye angel yake kaona hivo
Inawezekana ni kweli kwa upande wako unaamini au may be ni mtizamo wako.Ila lipo wazi Kiafya huwezi fanaisha impact ya poda na bange hzifanani na hazitokuja kufanana,kukubali huu upuuzi wa Rais wa Colombia sababu ya kushindwa kwake na jamii yake ni sawa na kukubali kuangamiza kizazi cha vijana.
 
Tuwaombee hawa ndugu zetu, ndio tumeshawapoteza hivyo?
 
Kuna point kwenye hoja yake kwamba Wamarekani huona kila kitu ni haramu kwao kama hakiwaingizi pesa na huo ndio ukweli.

Rejea sakata la Tik Tok.

Wanufaikaji wakubwa wa Biashara haramu kama kokeini ni Wamarekani.

Ukweli ni kwamba hakuna soko kubwa na la uhakila kama soko la kokeini la Marekani. Hivi Trump akisema Wamarekani wanaotumia madawa ya kulevya hususani Kokeini Marekani waaache ama watanyongwa nn kitatokea?

Hata hivyo jamaa naye anatumia kitabu cha Trump. Let's see how this unfolds.
Wauzaji na wanunuzi/watumiaji wa cocaine hawalipi kodi. Kupiga marufuku madawa ya kulevya kunaponya taifa na hakuna madhara kwenye makusanyo ya kodi.
 
Ipo siku itahalalishwa hata bangi walisema ni mbaya ila now majimbo mengi US si haramu. Nini kimebadilika kama ilikuwa mbaya?
Hata Pombe ilipigwa marufuku huko Marekani miaka fulani, lakini baadae wakaufungulia ulabu maana wananchi walikuwa wanatengeneza moonshine majumbani kwao, mapato ya kodi yakawa hayapatikani na watu wakawa wanaonekana wamelewa mitaani huku Bar zimefungwa na Serikali 😆😆😂
 
Wauzaji na wanunuzi/watumiaji wa cocaine hawalipi kodi. Kupiga marufuku madawa ya kulevya kunaponya taifa na hakuna madhara kwenye makusanyo ya kodi.
Shukurani

Mkulu, kwanza kabisa naomba kutofautiana na hoja yako kwamba Wauzaji na Wanunuzi na Watumiaji wa kokaina hawalipi kodi.

Kweli hawalipi kodi za moja kwa moja, ila wakiwa wanajihusisha na ,uuzaji ni lazima watatumia aina fulani ya transportation, hiyo tranpsortation lazima itakuwa legal, ikiwa ina maana inalipa tax na makorokoro mengine kama hayo, registration, road tolls n.k n.k kama hayo ili kuweza kuuza hio kokaina. Sawa na wanunuzi wakisha likoka wataenda kumuklabu au madada poa, na huko atajihusisha kwenye uchumi fulani ambao utaenda kuingizia serikali mapato. Tax revenue? Can we agree on that?

Ni kweli pia, kupiga marufulu madawa ya kulevya kunaeza ponya Taifa, lakini kutakuwepo na madhara kwenye makusanyo ya kodi. Indirectly. Kumbuka according to various sources Cocaine inakadiriwa kuwa na soko la karibia billioni 30 Dollar. Hiyo hela haiwezi kupatikana tu bila ya uwepo wa mkusanyo wa kodi pahala.
 
Back
Top Bottom