Rais wa FIFA Gianni Infantino ameeleza kitu ambacho nyota wa Argentina Lionel Messi anatakiwa kufanya ili awe mchezaji bora wa muda wote katika historia ya soka.
Akiongea na gazeti la The Nation la Argentina bosi huyo wa soka Duniani amesema Messi ni mchezaji mzuri lakini hawezi kuwa mchezaji bora wa muda wote mpaka ashinde kombe la Dunia.
“Messi ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini hajashinda ubingwa wa dunia akiwa na timu yake ya taifa hivyo anakosa sifa moja maana kuna wachezaji wengi tu wazuri hawajawahi kushinda kombe la dunia na hiyo ndio tofauti yao na Maradona”, amesema Infantino.
Messi na timu yake ya Argentina ipo kwenye mtihani wa kufuzu au kukosa fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi ambapo alfajiri ya kesho wanahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu au kucheza Play off na timu ya taifa ya New Zealand.
Aidha Infantino ameongeza kuwa Messi ana uwezo wa kucheza fainali za mwaka 2022 endapo ataendelea kujitunza kama sasa hivi ambapo hapati majeruhi ya mara kwa mara.
Chanzo: EATV