Rais wa FIFA ampa Messi mbinu za kuwa mchezaji bora wa muda wote

Rais wa FIFA ampa Messi mbinu za kuwa mchezaji bora wa muda wote

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
MESSI 2.jpg

Rais wa FIFA Gianni Infantino ameeleza kitu ambacho nyota wa Argentina Lionel Messi anatakiwa kufanya ili awe mchezaji bora wa muda wote katika historia ya soka.

Akiongea na gazeti la The Nation la Argentina bosi huyo wa soka Duniani amesema Messi ni mchezaji mzuri lakini hawezi kuwa mchezaji bora wa muda wote mpaka ashinde kombe la Dunia.

“Messi ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini hajashinda ubingwa wa dunia akiwa na timu yake ya taifa hivyo anakosa sifa moja maana kuna wachezaji wengi tu wazuri hawajawahi kushinda kombe la dunia na hiyo ndio tofauti yao na Maradona”, amesema Infantino.

Messi na timu yake ya Argentina ipo kwenye mtihani wa kufuzu au kukosa fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi ambapo alfajiri ya kesho wanahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu au kucheza Play off na timu ya taifa ya New Zealand.

Aidha Infantino ameongeza kuwa Messi ana uwezo wa kucheza fainali za mwaka 2022 endapo ataendelea kujitunza kama sasa hivi ambapo hapati majeruhi ya mara kwa mara.

Chanzo: EATV
 
Mess hajamfikia Ronaldo, na hatamfikia kamwe,

Nasema ronaldo origiNal si wa nywele na style za mademu nasema

Ronaldo mwenye.makombe mawili ya dunia ,ball on dor 2 ,na fifa world player of the year mara 3
 
Argentina haiwezi kufuzu kwenda Urusi kamwee!
 
Mess hajamfikia Ronaldo, na hatamfikia kamwe,

Nasema ronaldo origiNal si wa nywele na style za mademu nasema

Ronaldo mwenye.makombe mawili ya dunia ,ball on dor 2 ,na fifa world player of the year mara 3
Sema fenomeno.. hatari huyu kiumbe katika ubora wake
 
Bingwa wa bara la South America mwenyewe nje...haendi Russia (Chile)
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mess hajamfikia Ronaldo, na hatamfikia kamwe,

Nasema ronaldo origiNal si wa nywele na style za mademu nasema

Ronaldo mwenye.makombe mawili ya dunia ,ball on dor 2 ,na fifa world player of the year mara 3
unamzungumzia Ronaldo ambae hajawahi kushinda uefa siyo?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mess hajamfikia Ronaldo, na hatamfikia kamwe,

Nasema ronaldo origiNal si wa nywele na style za mademu nasema

Ronaldo mwenye.makombe mawili ya dunia ,ball on dor 2 ,na fifa world player of the year mara 3
ni kwel ila Ronaldo naye hakufanikiwa kuchukua Champions League ambayo kwa ngaz ya klabu ni kombe hadhi ya juu zaidi
 
Back
Top Bottom