Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Zenón Avomo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) akichukua nafasi ya Baltasar Engonga, aliyeng’olewa kufuatia kashfa ya ukiukaji wa maadili katika ofisi ya umma. Kashfa hiyo iliibuka baada ya uchunguzi kubaini uwepo wa video zaidi ya 400 zilizorekodiwa ndani ya ofisi ya Engonga, zikionesha wake, jamaa, na maofisa wakuu wa serikali, wakiwemo mawaziri na polisi, katika mazingira ya utata.
Pia, Soma: Guinea: Kigogo Baltasar Ebang Engonga anaswa na video 400 za ngono na wake wa viongozi mashuhuri, mwanasheria Mkuu aingilia kati
Kusambaa kwa video hizo kumesababisha wasiwasi mkubwa serikalini, na hatua za kinidhamu zimeanza kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika. Ili kuimarisha uadilifu, Serikali ya Guinea Ikweta imeagiza kufungwa kwa kamera za ulinzi katika taasisi zote za umma, lengo likiwa ni kudhibiti tabia za maofisa na kurejesha imani ya wananchi kwa serikali.
Zenón Avomo, akiwa na utaalamu wa sheria na fedha, anatarajiwa kuleta mabadiliko muhimu katika ANIF. Amewahi kushika nyadhifa za juu, ikiwa ni pamoja na Jaji wa Mahakama ya Malabo, Mkurugenzi Mkuu wa Masomo ya Mikataba na Masoko ya Serikali katika Wizara ya Fedha, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha pamoja na Wizara ya Madini, Viwanda, na Nishati.
Soma: