Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aondolewa madarakani. Uchaguzi kufanyika baada ya siku 60

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini imeidhinisha kwa kauli moja kuondolewa madarakani kwa Rais Yoon Suk Yeol baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka katiba kwa kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3, 2024, hatua ambayo ilizua mtafaruku mkubwa wa kisiasa.

Uamuzi huu unamaliza miezi ya mvutano wa kisheria na kisiasa, wakati nchi hyi o ikielekea kwenye uchaguzi wa Rais ndani ya siku 60.

Soma pia: Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aachiwa huru baada ya kuwa mahabusu kwa siku 52

Baada ya Rais kuondolewa, Waziri Mkuu Han Duck-soo atachukua nafasi ya kaimu rais kusimamia mpito wa uongozi, huku Yoon akikabiliwa na kesi ya jinai kwa mashtaka ya uchochezi.

Maelfu ya waandamanaji jijini Seoul walisherehekea uamuzi huo, huku wafuasi wake wakieleza masikitiko yao, ikiashiria mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini.

==============================================

yoon.png

A South Korean court upheld the impeachment of President Yoon Suk Yeol on Friday, officially throwing him out of office over his botched imposition of martial law and setting the stage for a new presidential election.

Yoon’s brief martial law declaration and subsequent impeachment trial have deeply divided South Korea, a key U.S. ally and one of the most vibrant democracies in Asia. Protests for and against the conservative leader’s removal from office have been held regularly, and officials had barricaded the courthouse ahead of the ruling on Friday in anticipation of possible violence.

Source: NBC News
 
Ningekua kwetu, ningekua kwetu kwetu milumbani ningemlilia mama
 
Wenzetu hawana mchezo kwenye maslahi ya nchi.Rais akichezea katiba na kutishia usalama wa nchi anakaa mahabusu kama raia wengine.Ipo mamlaka ya kumshughulikia Rais akivurunda.
 
Bora yeye Samweli Doe si walimkata masikio kabisa, maiti ikawa kama ya nyoka haina masikio
 
Ati, hiyo ndio Demokrasia!

...ni malumbano yasiyo na ulazima.
 
Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini imeidhinisha kwa kauli moja kuondolewa madarakani kwa Rais Yoon Suk Yeol baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka katiba kwa kutangaza sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3, 2024, hatua ambayo ilizua mtafaruku mkubwa wa kisiasa.

Uamuzi huu unamaliza miezi ya mvutano wa kisheria na kisiasa, wakati nchi hyi o ikielekea kwenye uchaguzi wa Rais ndani ya siku 60.

Soma pia: Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aachiwa huru baada ya kuwa mahabusu kwa siku 52

Baada ya Rais kuondolewa, Waziri Mkuu Han Duck-soo atachukua nafasi ya kaimu rais kusimamia mpito wa uongozi, huku Yoon akikabiliwa na kesi ya jinai kwa mashtaka ya uchochezi.

Maelfu ya waandamanaji jijini Seoul walisherehekea uamuzi huo, huku wafuasi wake wakieleza masikitiko yao, ikiashiria mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini.

==============================================

A South Korean court upheld the impeachment of President Yoon Suk Yeol on Friday, officially throwing him out of office over his botched imposition of martial law and setting the stage for a new presidential election.

Yoon’s brief martial law declaration and subsequent impeachment trial have deeply divided South Korea, a key U.S. ally and one of the most vibrant democracies in Asia. Protests for and against the conservative leader’s removal from office have been held regularly, and officials had barricaded the courthouse ahead of the ruling on Friday in anticipation of possible violence.

Source: NBC News
Mjinga Dan's huyu Yoon Suk. Kitu kizito kimemuangukia, sasa asubiri kesi ya udisadi wa mkewe
 
Wenzetu hawana mchezo kwenye maslahi ya nchi.Rais akichezea katiba na kutishia usalama wa nchi anakaa mahabusu kama raia wengine.Ipo mamlaka ya kumshughulikia Rais akivurunda.
Kwanini sisi tunashindwa kutengeneza katiba kama hiyo? Maana hata yao haikuandikwa na malaika ni watu walikaa chini wakakubaliana nchi iende ktk mfumo na mwongozo huu. Sisi huku kwanini tunashindwa?!
 
Nchi hiiblabda ndio kuzimu kwenyewe
Imefikia hatua watu na taasisi mbali mbali wanaona kusifia na kuabudu watawala ndo njia ya wao kuwa salama, wakati walitakiwa kukosoa mamlaka pale zinapokengeuka
 
Back
Top Bottom