Kiongozi wa Malawi alitoa kauli hii katika hotuba ya kitaifa siku ya Jumamosi.
Kwa mujibu wa Rais Chakwera, serikali yake inalenga kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi hazipotei bure.
Alisema kuwa mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ni kupunguza idadi ya magari kwenye msafara wake na kutumia magari yaliyotumika na Rais wa zamani, Peter Mutharika.
“Hivyo nimeagiza kuwa magari kwenye msafara wangu yasizidi 10, na serikali isinunue magari mapya kwa ajili ya rais,” alisema Chakwera.
Aliongeza kuwa anatarajia mawaziri wa baraza lake la mawaziri nao waweke mikakati ya kupunguza matumizi ya serikali.
Kwa mujibu wa Chakwera, lengo ni kupunguza upotevu wa rasilimali na kiasi cha fedha za umma kinachotumika kwa watu walioko kwenye nafasi za uongozi wa umma.
“Ninataka serikali yangu iwahudumie Wamalawi wote ipasavyo, kutoa huduma za kijamii ambazo hazipatikani kwa sasa, na kuhakikisha kuwa wananchi wanaweza kujikimu kimaisha,” alisema Chakwera.
Aidha, alikemea tabia ya kudai posho kwa kila shughuli, akisema kuwa hali hiyo inachangia upotevu wa rasilimali ambazo zinapaswa kuwafikia watu maskini.
Chakwera alisema kuwa jambo hili hutokea katika sekta ya umma na pia katika mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sababu watu wengi hawalioni kama matumizi mabaya ya fedha.
“Hatupaswi kuruhusu tabia hii ya watu kujitajirisha kwa kupokea posho zisizo za lazima.
“Lazima tupate njia ya kukomesha tabia hii ya kugawa posho zisizo za lazima ili kupunguza upotevu wa rasilimali,” alisema Chakwera.
https://malawi24.com/2020/07/26/chakwera-restricts-motorcade-to-maximum-of-10-vehicles/
Note:
Wakati nchi majirani wanapunguza matumizi yasio na tija, Tanzania ndio kwanza wabunge wanaongezewa pesa, serikali inanunua magari ya gharama kubwa wakati huduma za afya na miundombinu iko taabani. Pia huduma za maji na umeme bado ni changamoto hivyo kama nchi tuna la kujifunza hapa.