Rais wa Malawi ameagiza kuwa msafara wake usizidi magari 10 na serikali isinunue magari mapya kwa ajili yake

Malawi hawapo vizuri kwenye kukua kwa Uchumi hata dollar kupatikana ni mtihani alipoingia alileta usumbufu wa kuwafukuza wageni na kuchukua mali zao leo anatafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye kuporomoka kwa uchumi wa Malawi ndio maana anaona hata matumizi yake makubwa na viongozi wengine yamechangia kuwa hali hiyo..
 
Hi
View attachment 3354233
Kiongozi wa Malawi alitoa kauli hii katika hotuba ya kitaifa siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa Rais Chakwera, serikali yake inalenga kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi hazipotei bure.

Alisema kuwa mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ni kupunguza idadi ya magari kwenye msafara wake na kutumia magari yaliyotumika na Rais wa zamani, Peter Mutharika.

“Hivyo nimeagiza kuwa magari kwenye msafara wangu yasizidi 10, na serikali isinunue magari mapya kwa ajili ya rais,” alisema Chakwera.

Aliongeza kuwa anatarajia mawaziri wa baraza lake la mawaziri nao waweke mikakati ya kupunguza matumizi ya serikali.

Kwa mujibu wa Chakwera, lengo ni kupunguza upotevu wa rasilimali na kiasi cha fedha za umma kinachotumika kwa watu walioko kwenye nafasi za uongozi wa umma.

“Ninataka serikali yangu iwahudumie Wamalawi wote ipasavyo, kutoa huduma za kijamii ambazo hazipatikani kwa sasa, na kuhakikisha kuwa wananchi wanaweza kujikimu kimaisha,” alisema Chakwera.

Aidha, alikemea tabia ya kudai posho kwa kila shughuli, akisema kuwa hali hiyo inachangia upotevu wa rasilimali ambazo zinapaswa kuwafikia watu maskini.

Chakwera alisema kuwa jambo hili hutokea katika sekta ya umma na pia katika mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sababu watu wengi hawalioni kama matumizi mabaya ya fedha.

“Hatupaswi kuruhusu tabia hii ya watu kujitajirisha kwa kupokea posho zisizo za lazima.

“Lazima tupate njia ya kukomesha tabia hii ya kugawa posho zisizo za lazima ili kupunguza upotevu wa rasilimali,” alisema Chakwera.
https://malawi24.com/2020/07/26/chakwera-restricts-motorcade-to-maximum-of-10-vehicles/

Note:
Wakati nchi majirani wanapunguza matumizi yasio na tija, Tanzania ndio kwanza wabunge wanaongezewa pesa, serikali inanunua magari ya gharama kubwa wakati huduma za afya na miundombinu iko taabani. Pia huduma za maji na umeme bado ni changamoto hivyo kama nchi tuna la kujifunza hapa.
View attachment 3354236
Hii inatuhusu nini, acha kuokoteza maupuuzi huko kila nchi ina utaratibu wake
 
Gentleman,
kama Taifa huru linalojitegemea kiuchumi, kijamii na kisiasa,
itafanyika misafara ya maana kadiri iwezekano kwa maslahi mapana ya usalama wa viongozi wetu wa kitaifa na usalama wa waTanzania wote kwa ujumla.

hiyo tutafanya bila ruhusa ya yeyote 🐒
Sawa gentleman acha tuone kama tutafika popote
 
Malawi hawapo vizuri kwenye kukua kwa Uchumi hata dollar kupatikana ni mtihani alipoingia alileta usumbufu wa kuwafukuza wageni na kuchukua mali zao leo anatafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye kuporomoka kwa uchumi wa Malawi ndio maana anaona hata matumizi yake makubwa na viongozi wengine yamechangia kuwa hali hiyo..
Sure ni kweli hali ni mbaya sana, gharama ya maisha inasemekana imekuwa kubwa sana hasa baada ya Kwacha kuwa devalued by 45%
 
View attachment 3354233
Kiongozi wa Malawi alitoa kauli hii katika hotuba ya kitaifa siku ya Jumamosi.

Kwa mujibu wa Rais Chakwera, serikali yake inalenga kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi hazipotei bure.

Alisema kuwa mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ni kupunguza idadi ya magari kwenye msafara wake na kutumia magari yaliyotumika na Rais wa zamani, Peter Mutharika.

“Hivyo nimeagiza kuwa magari kwenye msafara wangu yasizidi 10, na serikali isinunue magari mapya kwa ajili ya rais,” alisema Chakwera.

Aliongeza kuwa anatarajia mawaziri wa baraza lake la mawaziri nao waweke mikakati ya kupunguza matumizi ya serikali.

Kwa mujibu wa Chakwera, lengo ni kupunguza upotevu wa rasilimali na kiasi cha fedha za umma kinachotumika kwa watu walioko kwenye nafasi za uongozi wa umma.

“Ninataka serikali yangu iwahudumie Wamalawi wote ipasavyo, kutoa huduma za kijamii ambazo hazipatikani kwa sasa, na kuhakikisha kuwa wananchi wanaweza kujikimu kimaisha,” alisema Chakwera.

Aidha, alikemea tabia ya kudai posho kwa kila shughuli, akisema kuwa hali hiyo inachangia upotevu wa rasilimali ambazo zinapaswa kuwafikia watu maskini.

Chakwera alisema kuwa jambo hili hutokea katika sekta ya umma na pia katika mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sababu watu wengi hawalioni kama matumizi mabaya ya fedha.

“Hatupaswi kuruhusu tabia hii ya watu kujitajirisha kwa kupokea posho zisizo za lazima.

“Lazima tupate njia ya kukomesha tabia hii ya kugawa posho zisizo za lazima ili kupunguza upotevu wa rasilimali,” alisema Chakwera.
https://malawi24.com/2020/07/26/chakwera-restricts-motorcade-to-maximum-of-10-vehicles/

Note:
Wakati nchi majirani wanapunguza matumizi yasio na tija, Tanzania ndio kwanza wabunge wanaongezewa pesa, serikali inanunua magari ya gharama kubwa wakati huduma za afya na miundombinu iko taabani. Pia huduma za maji na umeme bado ni changamoto hivyo kama nchi tuna la kujifunza hapa.
View attachment 3354236
Taarifa hiyo imfikie nanilii!
 
Sawa gentleman acha tuone kama tutafika popote
Tupo vizuri, uelekeo wa Taifa ni mzuri sana, tutavuka na kufika salama tuendako kama Taifa, na tutafika kwa amani na mshikamano mkubwa sana miongoni mwa waTanzania 🐒 🐒
 
No policy changes au sheria yeyote iliyobadilika kusapoti maneno yake, waswahili wanasema maneno matupu hayavunji mfupa,aache ujinga
 
Chakwera niliwahi kukutana naye kwenye kongamano moja Washington, Ana akili za kizungu mno!
 
Wakati wenzake wanaandaa mipango ya kuwasaida wananchi sisi tunaandaa mipango ya kufunga kanisa
 
Back
Top Bottom