Rais wa Malawi ameagiza kuwa msafara wake usizidi magari 10 na serikali isinunue magari mapya kwa ajili yake

Hiyo ndo Austerity budget.
Rais anapunguza matumizi ya Serikali ili fedha zikahudumie wananchi sio huku Bi Mwakatozo Bibi Kiziwi idd Amin Bibi ni kula raha tu.
Sa hii Maghabaribi wamemkata mirija amejikita na Uchina , Urusi na Korea Kaskazini kwa madikteta wenzake ambao hawawezi hata kumpa mwaliko.Maana hao ni mabahili kuliko ubahili wenyewe.
 
Chura kiziwi haelewi hata nini kinaendelea na itafika kipindi hata mishahara watashindwa kulipa.....maana saizi wanashindana kuiba pesa
 
Kuthubutu ni kuamua kufanya maamuzi sahihi hata kama kwa kuchelewa haijalishi kama mbele kuna uchaguzi au laa.....nakubaliana na wewe maamuzi yake yanaweza kuwa yanachagiwa na uchaguzi ulioko mbeleni ila amefanya jambo jema na huenda akaendeleza
Ya ngoja tusubiri tuone mwisho wake. Maana inanikumbusha Joyce Banda alipoona bado miezi miwili madarakani, akaja na ngonjera eti akishinda ataichapa Tanzania na kulichukua ziwa lote la nyasa ili liwe la kwao.

Wananchi wakagundua ni kamba, wakamchinjilia mbali. Maana kama kweli ana nguvu ya kufanya hivyo, basi alikuwa na nafasi ya kufanya hayo aliyoyasema miaka yote aliyokaa madarakani lakin hakufanya. Sasa kwanini aanze mikwara miezi miwili ya uchaguzi.
 
Sure.......acha tuone baada ya uchaguzi kama ataendelea na hii spirit
 
Malawi ni maskini wa kiuchumi, kijamii na kisiasa Lakini pia still kuna rushwa ya kutupwa na hakunaga kuchukuliwa hatua za kisheria, ni kusamehewa tu na mchungaji chakwera πŸ’
 
Malawi ni maskini wa kiuchumi, kijamii na kisiasa Lakini pia still kuna rushwa ya kutupwa na hakunaga kuchukuliwa hatua za kisheria, ni kusamehewa tu na mchungaji chakwera πŸ’
Upande wa Rushwa nadhani serikali ya Samia imekubuhu
 
dhana potofu haiwezi kuzuia waTanzania wasipate maendeleo gentleman πŸ’
Gentlemen mwambie kizimkazi apunguze wingi wa msafara ili pesa inayopotea onyo iende kuboresha miundombinu na huduma za afya
 
Njoo uone Tanganyika uku mkuu w mkoa w DAR kapewa Bajeti y kujenga ofisi yake Billion 60.
Wakati Jiji hali balabala za rami na changarawe tu shida na maji akuna.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Gentlemen mwambie kizimkazi apunguze wingi wa msafara ili pesa inayopotea onyo iende kuboresha miundombinu na huduma za afya
Gentleman,
kama Taifa huru linalojitegemea kiuchumi, kijamii na kisiasa,
itafanyika misafara ya maana kadiri iwezekano kwa maslahi mapana ya usalama wa viongozi wetu wa kitaifa na usalama wa waTanzania wote kwa ujumla.

hiyo tutafanya bila ruhusa ya yeyote πŸ’
 
Njoo uone Tanganyika uku mkuu w mkoa w DAR kapewa Bajeti y kujenga ofisi yake Billion 60.
Wakati Jiji hali balabala za rami na changarawe tu shida na maji akuna.
Kazi ni kipimo cha utu
Tanzania inaelekea shimoni mkuu, mambo yameharibika watu wanashindana kuiba pesa za umma tu huku huduma zikizorota
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…