Rais wa Malawi ameagiza kuwa msafara wake usizidi magari 10 na serikali isinunue magari mapya kwa ajili yake

Wa kwetu msafara zaidi ya magari 100 huku yamejaza wapambe tupu, wa Zambia msafara wake hauzidi magari 2, ni misafara ya hovyo na matumizi mabaya ya mali za umma, kwanini Rais asitumie gari moja na wengine wapande coaster?
 
Sahivi Africa kuna ma-Rais watatu Boknabe, Zambia na Malawi wengine wote ni wafujaji tupu
 
Aiweke kwenye maandishi ya kikatiba ili atakayekuja kumfuata ayafuate hayo hayo maono yake.
Mkuu huyu fisadi hawezi kuiweka kwenye katiba kwa sababu yeye mwenyewe ni mgombea wa nafasi hiyo ya uraisi. Na uchaguzi huo utafanyika mwezi wa 9, i mean bado miezi mitatu tu. Hii sera anaiweka kwa muda tu kuwa blackmail wajinga ili wamchague.

Jamaa amekaa madarakani toka 2020, amekula bata, amefisadi nchi, amejaza ndugu na jamaa zake kwenye serikali, ameharibu uchumi wa nchi. Sasa hivi bado miezi mi3 ya uchaguzi ndo anajifanya kukataa matumizi ambayo ameyatumia na kuyakubali kwa zaidi ya miaka mitano ya utawala wake wa awamu ya kwanza. Ni wajinga pekee ndo wanaoweza kumuamini huyo raisi na ukizingatia wajinga hawaishi duniani.
 
Hahaha bunge watasema ka nchi kenyewe kadogo kale hata gari mbili zinatosha.

Tanganyika kubwa ndege ya rais nayo itaongezewa escort flight 10.

Na vipi utashangaa wakiongeza idadi yasafara Tanganyika, maana na chawa wameongezeka.
 
Siasa za Africa ni za kipumbavu sana
 
Siasa za Africa ni za kipumbavu sana
Raisi wa Burundi Evariste Ndayishimiye, kipindi cha kampeni za uchaguzi aliwaambia wapiga kura wamchague ili akautokomeze ufisadi kwa vitendo, na kukuza uchumi wa nchi hiyo hadi nchi yake iwe angalau katika 10 bora ya mataifa yenye uchumi mkubwa duniani 🤣🤣🤣

Akasema akishaapishwa yeye na mawaziri wake na viongozi wote wa serikali wataishi katika nyumba zao wenyewe walizozijenga. Halafu ikulu na ofisi za serikali zitapangishwa ili hela zitazopatikana zisaidie kuinua uchumi wa nchi, kutoa elimu bure, kujenga viwanda, kupanua sekta ya utalii nk.

Lakini leo ni mwaka wa 5 sasa, hakuna hata kimoja kilichotekelezwa. Na yule aliewahi kuhoji au kukumbusha kuhusu ahadi hiyo alipotezwa ghafla mpaka leo hajulikani alipo. Subiri ikifika mwezi mmoja wa uchaguzi atakuja na ahadi zingine mpya aongezee na zile za mwaka ule ili ajiokotee kura kutoka kwa wajinga. Na atapata watu watamuamini kama kawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…