POTOSHI Rais wa Marekani Donald Trump amesema Rais Samia aache kufungia makanisa

POTOSHI Rais wa Marekani Donald Trump amesema Rais Samia aache kufungia makanisa

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1

1750852347320.png
 
Tunachokijua
Donald Trump ni Rais wa 47 wa Marekani ambaye alichaguliwa dhidi ya aliyekuwa makamu wa Rais Kamala Harris mwezi Novemba 2024, na kumfanya kuwa rais aliyechaguliwa kuhudumu mihula miwili isiyofuatana. Rais Trump alianza kutumikia muhula wake wa pili katika ikulu ya White House baada ya kuapishwa tarehe 20 Januari 2025 akihudumu pamoja na Seneta wa Ohio, J.D. Vance, kama Makamu wa Rais.


Kipande cha video kinachomuhusisha Rais Trump

Kipo kipande cha video kilichochapishwa katika mtandao wa Instagram kikimuonesha Rais Trump akimtaka Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuacha kufungia makanisa ya wachungaji ambao hawamuungi mkono kwani kila mtu ana haki na uhuru wa kujieleza.

Je, ni upi uhalisia wa Kipande Hicho.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaaini kuwa kipande hicho cha video ni sehemu ya hotuba ya kwanza ya Donald Trump ya Julai 18, 2024, baada ya tukio la kupigwa risasi lililotokea katika mkutano wa hadhara Julai 13, 2024 huko Butler, Pennsylvania nchini Marekani alipokuwa mgombea wa Urais.

Hakuna uhusiano wawote wa Hotuba hiyo ya Trump, na kuzungumzia ufungiwaji wa makanisa Tanzania, Mathalani Kanisa linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima lilizuiliwa kuendelea na huduma zake mapema mwezi Juni 2025, ilihali hotuba ya Trump ilikuwa Julai 2024 wakati ambao hakukuwa na malalamiko ya kufungiwa kwa makanisa.

Video hiyo imepotoshwa kwa kuwekewa sauti isiyo halisi. Kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde kinabainisha kuwa, sauti hiyo kwa asilimia 99.9 imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.
screenshot-2025-06-25-163429-png.3382768
Chanzo cha habari kitasakwa kwa gharama zote 🤣
 
Ndo ujinga wa AI. Hata aliyegundua AI anashangaa kwa nini binadamu wamenuwa vilaza namna hiii hadi wanaamini AI.
 
Samia hajafinga kanisa

Kanisa la Gwajima limefungwa Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania
 
Trump hana mamlaka ya kumuamrisha rais wetu afanye nini na nini hasifanye.
 
Back
Top Bottom