Rais wa Marekani, Joe Biden ajikwaa na kuanguka katika hafla ya Colorado

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Rais wa Marekani Joe Biden amejikwaa na kuanguka alipokuwa akikabidhi cheti cha diploma katika sherehe ya kuhitimu kwa Chuo cha Jeshi la Wanahewa la Marekani huko Colorado.

Biden, ambaye ndiye Rais mkongwe zaidi wa taifa hilo anayehudumu akiwa na umri wa miaka 80, alisaidiwa kusimama na alionekana kuwa hajadhurika.

Rais alikuwa amesimama kwa takriban saa moja na nusu kupeana mikono na kila mmoja wa wanafunzi 921 waliohitimu.

Awali, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya White House alisema kuwa "yuko sawa".

Kulikuwa na mfuko wa mchanga kwenye jukwaa alipokuwa akipeana mikono," Ben LaBolt aliandika kwenye Twitter baada ya kuanguka siku ya Alhamisi.

"Nilipata mchanga," Rais huyo aliyetabasamu alitania waandishi wa habari alipokuwa akirejea Ikulu jioni hiyo. Ripoti ya waandishi wa habari wa Ikulu ya White House hapo awali ilisema Bw Biden alijikwaa kwenye mfuko mweusi wa mchanga alipokuwa akipanda jukwaani.

Picha za tukio hilo zinaonyesha Bw Biden akionekana kuelekeza moja ya mifuko miwili ya mchanga iliyotumiwa kuinua kifaa chake cha teleprompta huku akisaidiwa na afisa wa Jeshi la Wanahewa na washiriki wawili wa huduma yake ya siri.

Alionekana akirudi kwenye kiti chake bila kusaidiwa na baadaye akikimbia kurudi kwenye msafara wake sherehe ilipokamilika muda mfupi baada ya ajali hiyo.

7ff57960-00f7-11ee-aa08-4727df20b680.jpg

Mwandishi huyo aliongeza kuwa Rais hakujibu maswali aliporejea kwenye ndege yake. Katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre alisema Bw Biden alikuwa akijihisi "mwenye afya kabisa" na alipanda ndege hiyo akiwa na "tabasamu kubwa".

Wakosoaji wamesema Bw Biden ni mzee sana kuwania muhula wa pili kama Rais.

Kura za hivi majuzi zinaonyesha kuwa wapiga kura wengi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu umri wake mkubwa. Atakuwa na umri wa miaka 82 mwanzoni mwa muhula wa pili ikiwa atashinda.

Kuanguka huku, pamoja na kujikwaa hapo awali kutoka kwa baiskeli yake na njiani akipanda ngazi za Air Force One, kunaweza kuongeza wasiwasi huo.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, mtangulizi wa chama cha Republican atachuana na Bw Biden katika uchaguzi wa Ikulu ya Marekani 2024, na alizungumza juu ya kisa hicho kutoka kwa hafla ya kampeni huko Iowa, akisema "mambo yote ni balaa tupu".
 
Kumbe hata wao wana uchu wa ukubwa...
 
View attachment 2643152

Na kwa nin wanaweka viroba vya mchanga ktk jukwaa analopanda prezdaa
 
Nawashauri wenye kushughulika na ulinzi wa Biden waende Zimbambwe wakajifunze namna ya kutoa ulinzi kwa Rais Mzee. Walinzi wa hayati Mugabe walikuwa na mbinu hadi za kumdaka kila alipotaka kuupiga mweleka. Hii ni aibu kwa walinzi kuzubaa hadi Rais anaramba udogo kwa mweleka.
 
Nadhani itakuwa sababu ya stress anazopewa na Museveni kumkatalia ushoga hadi aangalii chini
 
Back
Top Bottom