TANZIA Rais wa Namibia, Hage Geingob afariki Dunia

Mwaka 2014 alidhihirisha alivyowahi kutibiwa prostate cancer.

Mwaka 2015 akagombea, unaona ambavyo hakuficha historia ya afya yake kisa atakuja kugombea. Hakuongopa kwamba ni mzima hajawahi kuwa na shida.

January mwaka huu tukaambiwa anaumwa, anaumwa nini, amefanyiwa operation gani, bado tatizo gani na ataenda Marekani lini.

Wakati huo chama kimeishamtangaza mgombea wa kuwania kiti kwenye uchaguzi wa November, bado tupo February.

Si mnaona wenzetu mambo yao yalivyonyooka. Sisi kupata mgombea fujo kama tumekurupushwa, Rais kuumwa ni uchuro, mgombea mtarajiwa huwa hajawahi umwa na press up anapiga (kumbe aliwahi pelekwa hadi Uingereza kwenye matibabu ya moyo). Tafrani tu.

Apumzike kwa amani!
 
Poleni sana wa Namibia ila ukweli unasaidia sana taifa halitakuwa na taharuki 7bu mliwaandaa kiseikorojia kuwa anaweza kupona ama asipone RIP😭😭
 
Apumzike Kwa amani

Nje ya mada!
Kule hawana ujuzi wa kuficha taarifa kuanzia ugonjwa hadi kifo?
 
kama hakua dictator, basi Mungu ampokee kwenye utukufu wake.

kama alikuwa dictator......................jazeni wenyewe johnthebaptist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…