Rais wa Namibia kufanya ziara ya kitaifa nchini 19 - 22 Juni, 2026

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 19 Juni, 2026 kwa ziara ya kitaifa.

Ziara hiyo, ambayo ni ya pili kuifanya nchini Tanzania tangu aingie madarakani, inaendelea kudhihirisha uhusiano wa kindugu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, uliojengwa katika misingi ya harakati za ukombozi wa Afrika, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo unaonufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Tarehe 20 Juni, 2026, Rais Nandi-Ndaitwah atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam, yatakayojikita katika masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Baadaye, viongozi hao wawili watazungumza na waandishi wa habari.

Akiwa nchini, Rais Nandi-Ndaitwah atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambako aliwahi kuishi katika miaka ya 1980 alipokuwa Mwakilishi Mkuu wa chama cha South West Africa People's Organization (SWAPO), hatua inayobeba kumbukumbu muhimu za mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Namibia.

Vilevile, atatembelea Kambi ya Wapigania Uhuru wa Harakati za Ukombozi Barani Afrika iliyopo Kongwa, mkoani Dodoma.

Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kuhitimisha ziara yake nchini tarehe 22 Juni, 2026.

20260618_180225.jpg

Soma Pia
 
Tanzania kumpokea rais Netumbo Nandi ndaitwah wa Namibia kwa ziara ya kitaifa

Screenshot 2026-06-18 at 19-02-02 Instagram.png

​
 
Anakuja Kwa ndege yake au Airtanzania kama kawaida yenu
 
anakuja kwa ndege yake au Airtanzania
 
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 19 Juni, 2026 kwa ziara ya kitaifa.

Ziara hiyo, ambayo ni ya pili kuifanya nchini Tanzania tangu aingie madarakani, inaendelea kudhihirisha uhusiano wa kindugu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, uliojengwa katika misingi ya harakati za ukombozi wa Afrika, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo unaonufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Tarehe 20 Juni, 2026, Rais Nandi-Ndaitwah atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam, yatakayojikita katika masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Baadaye, viongozi hao wawili watazungumza na waandishi wa habari.

Akiwa nchini, Rais Nandi-Ndaitwah atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambako aliwahi kuishi katika miaka ya 1980 alipokuwa Mwakilishi Mkuu wa chama cha South West Africa People's Organization (SWAPO), hatua inayobeba kumbukumbu muhimu za mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Namibia.

Vilevile, atatembelea Kambi ya Wapigania Uhuru wa Harakati za Ukombozi Barani Afrika iliyopo Kongwa, mkoani Dodoma.

Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kuhitimisha ziara yake nchini tarehe 22 Juni, 2026.

View attachment 3610553
Hiyo haiondoi ukweli kwamba Samia suluhu Hassan aliwauwa ndugu, jamaa na marafiki zetu . Huku yeye akienda kujificha kwenye kambi ya jeshi ngerengere.
 
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 19 Juni, 2026 kwa ziara ya kitaifa.

Ziara hiyo, ambayo ni ya pili kuifanya nchini Tanzania tangu aingie madarakani, inaendelea kudhihirisha uhusiano wa kindugu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, uliojengwa katika misingi ya harakati za ukombozi wa Afrika, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo unaonufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Tarehe 20 Juni, 2026, Rais Nandi-Ndaitwah atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam, yatakayojikita katika masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Baadaye, viongozi hao wawili watazungumza na waandishi wa habari.

Akiwa nchini, Rais Nandi-Ndaitwah atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambako aliwahi kuishi katika miaka ya 1980 alipokuwa Mwakilishi Mkuu wa chama cha South West Africa People's Organization (SWAPO), hatua inayobeba kumbukumbu muhimu za mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Namibia.

Vilevile, atatembelea Kambi ya Wapigania Uhuru wa Harakati za Ukombozi Barani Afrika iliyopo Kongwa, mkoani Dodoma.

Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kuhitimisha ziara yake nchini tarehe 22 Juni, 2026.

View attachment 3610553
Mkumbuke Nchi za SADC hazikutambua uchafuzi wa 29 2025 mwezi wa 10.
Kuna shinikizo na ziara kadha kuja kumuona Lissu na kuwaona waliosababisha MO29.

Na tunajua juhudi za wasababishi ya MO29 kujitenga na vurugu3, waliosababisha.

Hivyo tegemea taarifa potofu toka kwao
 
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 19 Juni, 2026 kwa ziara ya kitaifa.

Ziara hiyo, ambayo ni ya pili kuifanya nchini Tanzania tangu aingie madarakani, inaendelea kudhihirisha uhusiano wa kindugu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Namibia, uliojengwa katika misingi ya harakati za ukombozi wa Afrika, mshikamano na ushirikiano wa maendeleo unaonufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Tarehe 20 Juni, 2026, Rais Nandi-Ndaitwah atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam, yatakayojikita katika masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Baadaye, viongozi hao wawili watazungumza na waandishi wa habari.

Akiwa nchini, Rais Nandi-Ndaitwah atatembelea eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam, ambako aliwahi kuishi katika miaka ya 1980 alipokuwa Mwakilishi Mkuu wa chama cha South West Africa People's Organization (SWAPO), hatua inayobeba kumbukumbu muhimu za mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Namibia.

Vilevile, atatembelea Kambi ya Wapigania Uhuru wa Harakati za Ukombozi Barani Afrika iliyopo Kongwa, mkoani Dodoma.

Rais Nandi-Ndaitwah anatarajiwa kuhitimisha ziara yake nchini tarehe 22 Juni, 2026.

View attachment 3610553
Raisi wa Marekani, China na Urusi watakuja lini?
 
Kaja kutushangaa inakuwaje taifa lenye watu zaidi ya ml 60 tunaongozwa na mtu mwenye elimu na akili ndg hv...maajabu!
 
Back
Top Bottom