Rais wa nchi yoyote kutumiwa salamu siku yake ya kuzaliwa na vyombo vya habari nchini ni lazima au kujipendekeza?

Rais wa nchi yoyote kutumiwa salamu siku yake ya kuzaliwa na vyombo vya habari nchini ni lazima au kujipendekeza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nami GENTAMYCINE naomba nichukue fursa hii kuwatakia 'Hepibasidei' wale wote wanaosheherekea leo hata na yule aliyekuwa jana na aliyeko leo huko Dakar nchini Senegal.

Ukiwa katika nchi yoyote ile duniani na ukakuta ama 99% ya Media zake au Media zote zinajikomba kwa mamlaka (Serikali) jua hilo Taifa ni la hovyo, halina maendeleo, lina unafiki na wanafiki wengi na idadi ya watu wasio na akili (fools) ni wengi mno.

Nashukuru Media ya (za) Tanzania yangu kwani yenyewe wala haina upuuzi huu (uliopo katika nchi zingine) na yenyewe muda wote huchapa kazi kwa kuibua mambo ya kimsingi, hukosoa, haijipendekezi kwa Serikali (mamlaka) hasa kwa kumtakia 'Hepibasidei' Rais ili waandishi wake wateuliwe katika nyadhifa mbalimbali.
 
Kazi nzuri za mama zimesababisha apendwe na kila mtanzania
 
Mapendo mapendo mapendo
Kesho kama Walivyofanya leo ( kwa Umoja Wao ule ule ) wamuelezee wazi wazi huyo Waliyejipendekeza Kwake leo kwa Kumuwishi Hepibasidei' kuwa hiyo nchi bado inapambana na Maadui zake Wakubwa Watatu waitwao Ujinga, Maradhi na Umasikini na wa Nne ( 4 ) ni Elimu duni iliyozalisha na inayoendelea Kuzalisha Mazuzu na Goigoi watupu.
 
Kwanini wana wish na wanampiga picha huku Mr wake wamemtenga?

Birthday yake ni sherehe binafsi ya kifamilia waambie hao chawa wake waache kum wish as a president huku akiwa ni mke wa mtu.
1674849479352.jpg
 
Asilimia kubwa Leo ni SHOBO NA KUJITAFUTIA TEUZI HAWAJUI KWAMBA TEUZI ZINAFANYIWAGA UTAFITI WENGI NI SHOBO TU
 
Mbona mimi pia niliwishiwa na takribani midia zote na siringi!!
 
Back
Top Bottom