‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima Maxence Melo wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬

‪Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ampa heshima Maxence Melo wa JamiiForums kwenye mkutano wa AU‬

Hata rais wetu mtukufu JPM anatambua mchango wa JF na anaomba malaika washuke waufunge mara moja.
Na kweli tulishukiwa ila ilikuwa ni TCRA nikawa najaribu kuangalia kama wana "Mabawa"lakini sikuyaona hahahaha!
 
Wenzetu wanampongeza huku kwetu wanamfungulia makesi kila siku, aisee sijui hili jamaa letu likoje
 
Hutawaona vijana wa Lumumba wakimpongeza Melo japokuwa hili ndo jukwaa lao pendwa

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Mkuu kuna msemo (" baniani mbaya kitu chake dawa") Jiwe japo anataka kumfunga maxence lakini yeye mwenyewe yumo humu na fake ID lakini wale vijana wa Lumumba (Wasaka tonge au njaa Kali) hawalijui hili wao kazi yao ni kusikiliza anaropoka kitu gani nao wafuate mkondo
 
Katika maraisi watakaopoteza umaarufu baada ya kutoka madarakani ni pamoja na huyu Jiwe!
Umaarufu wake tayari umeshapotea hukumbuki yule Eyakuze kaambiwa sio raia wa Nchi hii baada ya kutamka umaarufu wa Jiwe umeshuka. Nchi ikiwa na kiongozi Dikteta 🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂 kazi ya wapambe na wateule ni kumsifu kuliko wanavyomsifu Muumba wao! tena kinafiki
 
Max , kuna uwezekano mkubwa Sana akaja kuwa shujaa wetu wa demokrasia...
Mungu amuongoze Sana, amuepushe na tamaa na wenye hila......
Awe makini pia na mishe mishe zake
..we need JF this time strong more than never before in the history of this country......
Bravo@Maxence...
 
Nadhani Buhari ameonesha wazi jinsi Wanigeria wanavyomkubali na kushangaa kipaji alicho nacho Melo kuna jirani yangu mmoja Mnigeria anasema Melo ni mmoja wa Watanzania wachache wenye akili sana ni vile yupo kwenye Nchi masikini mfumo unawachukia wenye vipaji ni lecture wa UNISA...
 
Namkumbuka sana Marehem Deo Filikunjombe aliposema tatizo la nchi hii ni mawaziri.

Lakini pia naona Tatizo la nchi hii ni Taasisi zilizopo kisheria kama ilivyo TCRA wanatumika vibaya kuwalinda watawala badala ya kulinda maslahi ya umma.

Tuhuma nyingi zinazoweza kuibuliwa kupitia mitandao zinazimwa na TCRA badala ya TCRA kutumia taarifa wanazoziona na kuwakabidhi TAKUKURU na wakati Mwingine hata Tume ya maadili kuchunguza kwa wakati tofauti badala ya kuwatisha walioleta mada au tuhuma kwa kudhani kuwa ndio wanawalinda watawala hasa mawaziri .
 
Ni jambo jema Maxence Melo kupewa heshima hiyo kwa mchango wake, lakini ikumbukwe kuwa ili kuwa na jukwaa lenye manufaa kwa taifa ni lazima sheria za nchi zizingatiwe, tusijisahau kuwa na uhuru usio na mipaka ya kisheria kwa kuwa tu tuko anonymous hapa mtandaoni kwa uweza wa simu janja zetu!

JF libaki kuwa jukwaa la mawazo ya kila mmoja kuheshimiwa na kupeana changamoto si kuwa jukwaa lenye maudhui ya kuwapendelea watu folani na kuondoa maudhui ambayo hayapendezi machoni pa watu fulani kutokana na itikadi zao kuwa hazikubaliani na mawazo ya wengine!

JF isibaki kuwa jukwaa la kupondea serikali bila kutoa mawazo mbadala ya nini kifanyike ili kusonga mbele bila kuharibu hali ya hewa (kutoa lugha zisizo na staha kwa viongozi wa serikalini)
JF isiwe jukwaa la Moderator Fang Active kuondoa mawazo yanayoonekana kupingana na sera za vyama vya siasa vya upinzani, kwani kila mmoja anauhuru wake na mawazo yake mbadala kw akile anachokiamini.
Kongole wana JF wote especially founder Maxence Melo
 
Back
Top Bottom