Rais wa Senegal avunja Bunge kwa madai ya Kuvutana na Mhimili wa Serikali

nchi nyingi za Africa kikwazo kikubwa cha maendeleo ni vyama tawala,mfano Tz kikwazo kikubwa cha maendeleo ni CMM,,Africa Kusini ANC etc
 
Siasa na ukweli ni vitu viwili tofauti ,ni sawa na maji na mafuta. Ukisimama kwenye ukweli utaporomoka tu
 

Rais wa Senegal, Bassirou Faye amevunja bunge la nchi hiyo linaloongozwa na upinzani akifungua njia kwa uchaguzi wa haraka wa wabunge kufanyika ikiwa ni miezi sita baada ya kuchaguliwa kwake.

Ametaja sababu kubwa ya uamuzi huo ni bunge hilo kuvutana na serikali yake, jambo linalokwamisha utendaji wake hasa katika kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Uchaguzi mpya utafanyika Novemba 17, 2024, Faye alisema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni jana Alhamisi Septemba 12, 2024 ambapo aliwataka wapigakura kukipa chama chake mamlaka ili aweze kutekeleza mageuzi ya kimfumo aliyoahidi.

Wachambuzi wanasema kuwa chama cha siasa cha Rais Faye (PASTEF), kina nafasi kubwa ya kupata wingi wa viti kutokana na umaarufu wake na kiwango chake cha ushindi katika uchaguzi wa rais wa Machi 2024.

Jukwaa la upinzani la Benno Bokk Yaakar likiongozwa na Rais wa zamani, Macky Sall limelaani hatua hiyo wakidai kuwa Faye ameitisha kikao cha bunge chini ya sheria za uongo ili kutangaza kuvunjwa kwa bunge hilo, huku akimshutumu kwa kuvunja sheria.

Rais Faye mwenye umri wa miaka 44, alishinda uchaguzi huo Machi 2024 na kuwa kiongozi wa kuchaguliwa mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika, chini ya wiki mbili baada ya kuachiliwa kutoka gerezani.
 
Wabunge wasiotaka kupelekeshwa 🙂
 
ameshindwa kazi anasingizia Bunge dah 🤣
 
tumwombee kijana huyu. Ila kwa kawaida afrika wale ambao huwa wanaingia kwa nguvu ya umma na kuaminiwa mwisho huwa wanawaangusha wale waliowaamini na kugeuka miungu..
 
Fikiria bunge la nchi yetu, wabunge theluthi 2 watoke Chadema na theluthi Moja watoke Ccm na ccm ndiyo iwe imetoa Rais, patamu hapo.
sasa gentleman,
sasa ukiangalia hata hapa nchini, mathalani Hashimu Rungwe Sipunda kashinda uchaguzi mkuu na amekua Rais na ana wabunge wa3 tu wa chama chake bungeni kuna kitu anaweza kufanya kweli?

hata avunje bunge mara30 hawez kupata wabunge wa kumsaidia kuendesha nchi....
Lazima auende serikali ya umoja wa kitaifa sio kuvunja bunge anaweza akawakosa hata hao watatu alonao....


Faye na Songo wana kiburi mno, walidhani wanapendwa na wananchi kumbe wananchi walimchukia na kuchoka uongozi wa Maki Sali tu...

sasa fuatilia vizuri uchaguzi wa hilo bunge jipya, utagundua hata wale wabunge wachache wa vyama vya Faye na sonko hawarudi bungeni na wale wa kilichokua chama Tawala wanaongezeka na wanakua zaidi ya 98% bungeni, hawatamaliza miaka mitano akina Faye wataondoshwa mamlakani....

suluhisho pekee na muhimu sana ni kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pakee na wasonge mbele 🐒
 
Umesomeka.
 
Ameshajioanga kuiba na kushinda maana Tume ya uchaguzi iko chini yake
 
Tatizo liko kwenye Ideology; jamaa anataka kuendekeza siasa za usoshalisti, halafu ni islamist aliyejificha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…