Rais wa Syria aionya Israel dhidi ya kuiburuza Syria vitani

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa ameituhumu Israel kwa kujaribu kuiburuza Syria katika vita na amesema nchi yake haitakubali kunaswa na chambo hicho.Katika hotuba iliyorushwa mapema alfajiri katika runinga ya taifa, rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amesema hawatawapa Israel fursa ya kuwaingiza watu wa Syria katika vita ambavyo vinatumika tu kuigawanya nchi na kupanda uharibifu.

Rais huyo wa Syria ameilaumu Isreal kwa kutumia ukosefu wa utulivu kufuatia mabadiliko ya utawala, akiituhumu kwa kuilenga miundombinu ya umma na kutaka kukwamisha juhudi za ujenzi mpya.

Akizungumzia machafuko katika mkoa wa kusini wa Sweida, Al-Sharaa amesema serikali yake imeingilia kati kufikisha mwisho makabiliano kati ya makundi ya eneo hilo yaliyokuwa yakipigana.

Wakati huo huo, China imetoa wito uhuru wa Syria uheshimiwe baada ya Israel kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya nchi hiyo, ikiwa ni katika kuiunga mkono jamii ya wachache ya Druze.
 
Huyu mwamba hajiamni Ata kidogo yaan Israel anapiga ndan kabisa anapotaka mda anaotaka yeye yupo tu anashindwa na hamas kikundi cha wahuni tu anyways tumpe mda huenda hana vifaa mana kachukua nchi ikiwa ovyo kweli
 
Hao wanaojiita "Waisrael" sijui ni kizazi cha Ibilisi gani! Muda wote wenyewe wanatafuta tu chokochoko za kupigana vita na majirani zao.

Zamani walikuwa wanaishambulia Syria kwa kisingizio cha uwepo wa Rais Bashaar Al Assad! Sasa hivi amewekwa kibaraka wao, bado kila siku ni kutafuta tu chokochoko!
 
Netanyahu anatumia vita km sababu ya kukwepa kesi za ufisadi zinazomkabili kila kesi ikitaka kuendelea anatafuta vita hili ashindwe kwenda mahakamani nchi ipo kwenye hali ya hatari ndio maana ikipoa vita huku unasikia kaanzisha kwengine.
 
Back
Top Bottom