KWELI Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli alifariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

KWELI Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli alifariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeleza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo majira ya saa 12 jioni kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme ambalo limekuwa likimkabili kwa takirbani miaka 10.



1658211621347.png
 
Tunachokijua
Mnamo Machi 17, 2021 ilitoka taarifa kuwa aliyeluwa Rais wa Tanzania wakati huo Hayati Magufuli amefariki Dunia. Taarifa hiyo ilidokeza kuwa Rais huyo aliyekuwa na miaka 61 alifariki kutokana na maradhi ya moyo aliyokuwa akisumbuliwa kwa zaidi ya miaka 10.

Taarifa ya Kifo cha Hayati Magufuli ilitolewa na aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu kupitia Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) na baadaye kuripotiwa pia na vyombo mbalimbali ikiwamo JamiiForums. Katika taarifa hiyo Makamu wa Rais alisema:

Mheshimiwa rais Magufuli, alilazwa tarehe 6 Machi katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme, ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10, alituhusiwa tarehe 7 machi mwaka huu na kuendelea na majukumu yake.
Tarehe 14 Machi mwaka huu alijisikia vibaya na akakimbizwa hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta.
Baada ya kifo cha Hayati Magufuli maombolezo yaliendeshwa nchi nzima na mnamo Machi 26, 2023 Hayati Rais Magufuli alizikwaMkoani Geita katika Wilaya ya Chato.

Je, Kifo cha Magufuli kilitokana na Ugonjwa wa moyo?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa baada ya kutoka taarifa ya kifo cha Hayati Magufuli baadhi ya wanasiasa na Wadau wa mitandao ya kijamii walipinga sababu ya kifo cha Hayati Magufuli iliyotolewa na Serikali na kuhusisha kifo cha Hayati Magufuli na ugonjwa wa Covid-19. Wadau wengine walienda mbali zaidi na kutaka kifo cha Hayati Magufuli kichunguzwe.

Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa hoja hizo za kupinga taarifa ya serikali bado hakuna upande wowote ambao ulitoa uthibitisho wa hoja zake.

Kutokana na hoja nyingine kukosa uthibitisho, JamiiForums inaona kwakuwa Serikali ndiyo chanzo rasmi chenye mamlaka ya kuelezea kifo cha Rais na sababu ya kifo chake, tunalazimika kuamini taarifa hiyo.
Endelea kupumzika kwa amani Chuma, Tingatinga, Jiwe. Rais uliyetimiza wajibu kwa wakati wako.
 
Back
Top Bottom