Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Akutana na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Akutana na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana leo na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Oluseguni Obasanjo.

Taarifa zaidi kutolewa

========

Obasanjo.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano leo Mei 3, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olesegun Obasanjo.

Rais Mstaafu, Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Mhe. Rais Samia kufutia vifo vya waliokuwa marais wa Tanzania ambao ni Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Magufuli.

Aidha wamezungumzia hali ya usalama barani Afrika na umuhimu wa wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro ambayo inasababisha vifo vya watu hasa wanawake na watoto

Pia wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.


Ikulu.jpg
 
watu huko twitani wanasema code wameshaisoma. kwa maana tycoon aliewekeza hapa bongo ndio kamtuma wakishirikiana na mstaafu ili mambo yao yaende.
 
watu huko twitani wanasema code wameshaisoma. kwa maana tycoon aliewekeza hapa bongo ndio kamtuma wakishirikiana na mstaafu ili mambo yao yaende.

Kwanini amtume Obasanjo wkt Mstaafu mwenyewe yuko hapa na access ya mojo kwa moja na maza?
 
Back
Top Bottom