Rais wa TFF ahusishwa kupokea rushwa ya mamilioni kutoka CAF. Mwenyewe akana tuhuma hizo

KAIRA-720x450.jpg

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia anadaiwa kuwa miongoni mwa walionufaika na TZS milioni 46 ($20k) zilizogawiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad zinazodaiwa kuwa ni rushwa.
Rais Ahmad anatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipotwaa uongozi wa chombo hicho kikubwa cha soka Afrika.

Nyaraka zilizowasilishwa FIFA zimeonesha kuwa Ahmad Ahmad aliisababishia CAF gharama ya ziada ya takribani TZS bilioni 2 (
$830,000) kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kama Tactical Steel.

Pia anatuhumiwa kuwadhalilisha watumishi wanne wakike wa CAF ambao majina yao hayakuwekwa bayana.
Zaidi Ahmad Ahmad anatuhumiwa kukiuka sheria za CAF na kuongeza uwakilishi wa Morocco ndani ya shirikisho hilo.
Aidha anatuhumiwa kutumia zaidi ya TZS milioni 925 ($400,000) of CAF za CAF kwa ajili ya magari nchini Misri na Madagascar ambapo ofisi ndogo za CAF zimefunguliwa.

Afisa mwanamizi wa CAF ambaye hakutaka jina lake lifahamike amesema kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (EC) ya CAF, Amr Fahmy aliyetoa tuhuma hizo dhidi ya Rais wa CAF amefutwa kazi.
CAF imethibitisha kuwa Fahmy alifutwa kazi Alhamisi iliyopita katika mkutano wa EC, siku moja kabla ya droo ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), lakini hawakueleza sababu.

Nafasi yake imechukuliwa na Mouad Hajji kutoka Morocco.

MY TAKE:

Karia kashaanza kuletewa utundu Lissu, nasubiri akane. Unaleta Siasa kwenye Mpira
Lete ushahidi, Izo siasa za akina Issa hayatou baada ya kushindwa uchaguzi hazina nafasi kwasasa. Watu wanataka waiongize CAF milele, Walishindwa kwenye Sanduku la kura sasa wanaleta figisu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karia ni mchumia tumbo tuu, nitashangaa serkali kuendelea kumuogopa huyu bwana
Sioni tofauti yake na malinzi

Wacheni majungu yenu bana, huyo jamaa ni jembe hapo TFF, amedhibiti mianya yote ya upigaji pesa TFF labda hilo ndo linalomfanya kuwa na maadui wengi sasa.Watanzania tubadilike jamani! Shutuma za kila siku zisizo na msingi hazitusaidii
 
Wacheni majungu yenu bana, hu
yo jamaa ni jembe hapo TFF, amedhibiti mianya yote ya upigaji pesa TFF labda hilo ndo linalomfanya kuwa na maadui wengi sasa.Watanzania tubadilike jamani! Shutuma za kila siku zisizo na msingi hazitusaidii

Labda Kaziba mianya kwa wengine kaacha yake
 
Mianya gani kaziba? Karia ni fisadi kama alivyokuwa mtangulizi wake malinzi
Wacheni majungu yenu bana, huyo jamaa ni jembe hapo TFF, amedhibiti mianya yote ya upigaji pesa TFF labda hilo ndo linalomfanya kuwa na maadui wengi sasa.Watanzania tubadilike jamani! Shutuma za kila siku zisizo na msingi hazitusaidii
 
Hii ni vita ya huko CAF , katibu mkuu wa CAF amefukuzwa wiki iliyopita, wiki hii anakuja na tuhuma zisizo na uthibitisho wowote. Kama alikuwa anajua yote haya kwa nini hakusema hadi afukuzwe kazi ndio aanze kuropoka tuhuma zisizo na uthibitisho.
 
huyu jamaa huwa simukubali hata kidogo cjui walimu mchaguaje hawa watu hafai hata kidogo ni walewale tu kama malinzi
 
KAIRA-720x450.jpg

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia anadaiwa kuwa miongoni mwa walionufaika na TZS milioni 46 ($20k) zilizogawiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad zinazodaiwa kuwa ni rushwa.
Rais Ahmad anatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipotwaa uongozi wa chombo hicho kikubwa cha soka Afrika.

Nyaraka zilizowasilishwa FIFA zimeonesha kuwa Ahmad Ahmad aliisababishia CAF gharama ya ziada ya takribani TZS bilioni 2 (
$830,000) kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kama Tactical Steel.

Pia anatuhumiwa kuwadhalilisha watumishi wanne wakike wa CAF ambao majina yao hayakuwekwa bayana.
Zaidi Ahmad Ahmad anatuhumiwa kukiuka sheria za CAF na kuongeza uwakilishi wa Morocco ndani ya shirikisho hilo.
Aidha anatuhumiwa kutumia zaidi ya TZS milioni 925 ($400,000) of CAF za CAF kwa ajili ya magari nchini Misri na Madagascar ambapo ofisi ndogo za CAF zimefunguliwa.

Afisa mwanamizi wa CAF ambaye hakutaka jina lake lifahamike amesema kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (EC) ya CAF, Amr Fahmy aliyetoa tuhuma hizo dhidi ya Rais wa CAF amefutwa kazi.
CAF imethibitisha kuwa Fahmy alifutwa kazi Alhamisi iliyopita katika mkutano wa EC, siku moja kabla ya droo ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), lakini hawakueleza sababu.

Nafasi yake imechukuliwa na Mouad Hajji kutoka Morocco.

MY TAKE:

Karia kashaanza kuletewa utundu Lissu, nasubiri akane. Unaleta Siasa kwenye Mpira
niko tayari kuchangia pesa taslim za kuweka mafuta magari ya polisi ( kuepusha visingizio ) ili kuwezesha Wallace Karia kukamatwa
 
Back
Top Bottom