redio
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 5,813
- 12,921
Lete ushahidi, Izo siasa za akina Issa hayatou baada ya kushindwa uchaguzi hazina nafasi kwasasa. Watu wanataka waiongize CAF milele, Walishindwa kwenye Sanduku la kura sasa wanaleta figisu.![]()
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia anadaiwa kuwa miongoni mwa walionufaika na TZS milioni 46 ($20k) zilizogawiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad zinazodaiwa kuwa ni rushwa.
Rais Ahmad anatuhumiwa kwa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi, ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipotwaa uongozi wa chombo hicho kikubwa cha soka Afrika.
Nyaraka zilizowasilishwa FIFA zimeonesha kuwa Ahmad Ahmad aliisababishia CAF gharama ya ziada ya takribani TZS bilioni 2 (
$830,000) kwa kuagiza vifaa kupitia kampuni ya Ufaransa ijulikanayo kama Tactical Steel.
Pia anatuhumiwa kuwadhalilisha watumishi wanne wakike wa CAF ambao majina yao hayakuwekwa bayana.
Zaidi Ahmad Ahmad anatuhumiwa kukiuka sheria za CAF na kuongeza uwakilishi wa Morocco ndani ya shirikisho hilo.
Aidha anatuhumiwa kutumia zaidi ya TZS milioni 925 ($400,000) of CAF za CAF kwa ajili ya magari nchini Misri na Madagascar ambapo ofisi ndogo za CAF zimefunguliwa.
Afisa mwanamizi wa CAF ambaye hakutaka jina lake lifahamike amesema kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (EC) ya CAF, Amr Fahmy aliyetoa tuhuma hizo dhidi ya Rais wa CAF amefutwa kazi.
CAF imethibitisha kuwa Fahmy alifutwa kazi Alhamisi iliyopita katika mkutano wa EC, siku moja kabla ya droo ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), lakini hawakueleza sababu.
Nafasi yake imechukuliwa na Mouad Hajji kutoka Morocco.
MY TAKE:
Karia kashaanza kuletewa utundu Lissu, nasubiri akane. Unaleta Siasa kwenye Mpira
Sent using Jamii Forums mobile app