Rais wa TFF amewaonya waandishi wa habari kutomuuliza swali lolote Rais wa FIFA kuhusu Zanzibar!

He is right, kwa sababu ki Fifa, Zanzibar doesn't exist. Kififa nchi ni moja tuu, JMT.

Ni sawa na kumuuliza SG wa UN kuhusu kilichokuwa kiti cha Zanzibar kule UN.
P
Pascal, tusidanganyane tafadhari. Wenzetu huwa wanapata habari takriban zote kabla ya kufanya jambo hivo hata ujio wa rais huyo wa FIFA na wajumbe wengine wanakila kitu kuhusu mambo yetu. Nawaomba viongozi wa ZFA watumie nafasi hii kuweka mambo sawa.
 
Hii ni kweli au uzushi tu?

Mtu mwenye akili mbovu kama hizi eti ndio alichaguliwa kuongoza TFF kweli?

Hii nchi mtu anapopata hata mamlaka ya kuwa mwenyekiti wa familia anadhani ana mamlaka ya kila aina. Ajabu kweli
Dah! Inashangaza sana. Labda kapata maelekezo toka juu kwa walio muweka hapo kwani sidhani katika Ulimwengu huu pana mtu anaewapangia waandishi wa habari maswali ya kuuliza.
 
Yawezekana kaagizwa ahakikishe hilo la kuhusu Zanzibar halizungumzwi na onyo hilohilo huwenda wakawa wamepewa viongozi wa ZFA.
 
Nadhani angemwambia kwanza huyo rais wa wa fifa asijibu swali lolote atakaloulizwa kuhusu Zanzibar.
 
He is right, kwa sababu ki Fifa, Zanzibar doesn't exist. Kififa nchi ni moja tuu, JMT.

Ni sawa na kumuuliza SG wa UN kuhusu kilichokuwa kiti cha Zanzibar kule UN.
P
Mkuu,paskal hata wewe unaunga mkono waandishi kupangiwa mambo ya kutouliza?.

Kwani huyo rais wa fifa yeye ni poyoyo kiasi kwamba hawezi jieleza mwenyewe?.kwamba hawezi jisemea yeye mwenyewe kua sisi fifa hatuitambui Zanzibar?.

Aisee ndo tatizo la kulazimisha mambo.
 
Sasa nimekuelewa,ila kuna wakati zinashitua sana comment zako.
 
Uoga mpaka makatoni.
 
Pascal, tusidanganyane tafadhari. Wenzetu huwa wanapata habari takriban zote kabla ya kufanya jambo hivo hata ujio wa rais huyo wa FIFA na wajumbe wengine wanakila kitu kuhusu mambo yetu. Nawaomba viongozi wa ZFA watumie nafasi hii kuweka mambo sawa.
Mara kibao baba na mama huwa wanagombana chumbani na kununiana, hawaongei, ila akija mgeni, wanazuga, na wanazungumza. Huyo mgeni anaweza kuwa well informed kuwa mmegombana na hamuongei, hivyo akifika, hata kama anajua mmegombana, as long as mnaongea, hawezi kuulizia vipi ule ugomvi?.

Huo ndio ugomvi wa FAT na ZFA, hawataki kabisa mgeni ajue hizi ni nchi mbili tofauti kimichezo!. Zanzibar iliwahi kufanya hivyo kwa kujiunga na OIC, kiliwaka hadi kulazimishwa kujitoa na wafia dini Fulani, kwa hoja kuwa OIC ni Jumuiya ya kisiasa. Kitendo cha Fifa kuiruhusu Zanzibar kuwa member wake ni kuitambua Zanzibar kama nchi, wakati sisi tunaitambua kama mkoa tuu!.
P
 
Mwanangwa, nachofahamu mie HAKUNA ugomvi kati ya TFF na ZFA (labda uanzishwe na uongozi huu). Viongozi wote wa FAT/TFF walikuwa sambamba na wa ZFA kuhakikisha Zanzibar inakuwa mwanachama kamili wa CAF na FIFA.
Halafu kumbuka The Great Britain, mbona FIFA imezichambua nchi hizo?
 


Acheni Kuunga Mkono "Ukandamizaji Wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari".. Utampangiaje Mwandishi Cha Kuuliza?
Hata Yule Raisi wa Maraisi Donald Trump Basi Waandishi Wako Huru Kumuuliza Chochote! Ametungiwa Mpaka Kitabu ya Kumsema Vibaya lakini Hakuzui Taaluma Hiyo ya Uandishi Kwasababu alijua Kila Raia anahaki Ya Kujua Kuhusu Yeye na Nchi Yao.

lakini cha Ajabu eti Kuhusu Zanzibar waandishi Wanakatazwa Wasiifanyie Haki Taaluma yao na Uhuru Wao! [HASHTAG]#Shithole[/HASHTAG] Country
 
Sasa akimuuliza atafanya nn?
Waandishi waulize tu.
Kwanini TFf inakula fedha zote za missaada
Bila kupeleka znz
Tuna njia za kuwauliza ...
 
Huyu nae hovyo kabisa anawapangia watu ktu cha kuongea
 
Huyu rais wa TFF wakati anachaguliwa nilikuwa nikidhani kuwa atakuwa mtu wa maana kwenye kuendeleza soka la nchi hii ni lakini nimekuja kugundua kuwa naye kumbe ni mjinga mjinga tu
Mkuu umenichekesha sana eti ni.mjinga mjinga tu. Na ni mjinga kweli. Nimeona Pasco anamtetea kuwa yupo sahihi. Ngoja tupige kimya.
 
Kuumbe ni maelekezo toka juu basi tusamehe anko Karia. Doooh hili li nchi bwana.
 

Nashahuri watu wamfuate huko Tweeter raisi wa Fifa wakamuulize je Amekatazwa kujibu swali lolote kuhusu znz ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…