Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa Klabu ya Yanga kutengua maamuzi ya kujitoa kushiriki kombe la Kagame Cup.
Karia amesema sababu ambazo Klabu ya Yanga imezitoa kutoshiriki michuano hiyo hazina mshiko yoyote na ameuomba uongozi wa Klabu ya Yanga kubadili maamuzi hayo ndani ya saa 48 zijazo.
Karia ameongeza kuwa vilabu vya Rayon Sports na Gor Mahia ambazo wapo kundi moja na Yanga kwenye michuano ya Caf Confederation Cup wamethibitisha kushiriki Kagame Cup na wao wana michezo kama Yanga.
Klabu ya Yanga Jana iliwasilisha barua ya kujitoa kushiriki kombe la Kagame Cup kutokana na kubanwa na ratiba ya michuano hiyo kwa mchezo wa tatu wa makundi ya Kombe la Shirikisho.