Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya kuona majeshi yake yamefanikiwa kuwarudisha wanajeshi wa Urusi kwenye baadhi ya maeneo yaliyotekwa, sasa Rais wa Ukraine, Zelensky ameanza kuidharau Urusi pakubwa na kutoa utabiri wa kushinda moja kwa moja kama kwamba anapigana na mtoto mdogo.
Kwenye hotuba yake hapo jana alisema kwa sasa hakuna chochote kitakachoisaidia Urusi ishinde katika vita hivi, si silaha kutoka popote duniani wala droni za Iran. Akaongeza kuwa kwa sasa Urusi imeshindwa.
Jee ni kweli na yeye ana silaha na Jeshi hilo la kuitambia Urusi kiasi hicho. Au ni kiburi na propaganda za kivita tu.