Nani alimbadilisha Mwalimu kiitikadi?! Ukimfuatilia Mwalimu kwa umakini utagundua ni kama mwanzoni alikuwa na mtazamo wa Kimagharibi-- namaanisha ubepari hadi mwaka 1968 alipoupa kisogo rasmi mfumo huo!
Maasi ya 1964 yanatoa uwezekano mwingine wa kwamba, baada ya uhuru, Mwalimu hakuwa mjamaa! Kama ilivyo ada kwamba unapokumbwa na janga utaomba msaada kwa yule unayeamini atakusaidia; baada ya Maasi ya 1964 Mwalimu aliomba msaada toka kwa bepari Uingereza!!
Unclassified CIA Files ambazo zilifichua siri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar nazo zinatoa uwezekano mwingine wa kwamba huenda, back then, Mwalimu alikuwa na mtazamo wa Kipebari!
If so, who "converted" him?! Can it be Abdulrahman Babu ambae hata kabla Zanzibar haijamtimua Sultan yeye na wenzake walishakuwa ma-communists yaliyokubuhu yaliyomtisha hata Karume? Ikumbukwe kwamba, struggles za Abdulrahman Babu zilikuwa na back up ya kutosha kutoka nchi za kikomumisti hususani China! Hata kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari Babu alishakuwa amepeleka vijana wake Cuba kuchukuwa mafunzo ya Kijeshi kutoka Communist Cuba ili hatimae waje kumtoa Sultan!
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, Abdulrahman Babu alikuwa ndo Foreign Minister baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kabla ya kupata hicho cheo tayari alikuwa na connection kubwa na China pengine kuliko connection ambazo Mwalimu alikuwa nazo! Kwavile bado naamini Mwalimu hakuwa Mjamaa alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza; si kwamba ni huyu Babu ndie alimbadilisha? Don't forget, Babu nae wakati huo alikuwa ni msomi kama Mwalimu!
Na ikiwa hisia zangu (he wasn't a socialist from day one) ni sahihi na endapo asingekuwa TOTALLY "converted" lakini badala yake angeamua ku-practice mixed economy; am telling you, Mwalimu angeiacha Tanzania mbali sana kiuchumi. Ubepari unahitaji big brain na Mwalimu alikuwa nayo.
RIP Mwalimu.