Mwadilifu Mdhulumiwa
JF-Expert Member
- Jul 22, 2021
- 419
- 640
Wakuu Salam!
Moja kwa moja kwenye mada! Hivi karibuni akiwa ziarani katika moja ya mikoa ya kanda ya ziwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alizitaka mamlaka za kodi kuacha kudai kodi za kuanzia miaka miwili (2) nyuma, huku akibainisha wazi kuwa kitendo cha kodi hizo kulimbikizwa ni uzembe wa mamlaka zilizopewa dhamana ya kukusanya kodi hizo.
Hapana shaka uamuzi na kauli hii ya Mheshimiwa Rais imepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi walio wengi wanaoteswa na kesi za kodi pamoja na usumbufu wa kuandikiwa barua za kila wakati wakitishiwa kufikifishwa mahakamani kutokana na madeni hayo.
Hata hivyo mpaka sasa kumekua na sintofahamu kuhusu aina za kodi zitakazohusishwa na msamaha huo, huku watu wengi wakiamini kuwa agizo hilo la Mheshimiwa Rais linawahusu TRA tu na si mamlaka nyingie zinazotoza kodi.
Mfano ni wizara ya ardhi ambayo mwaka 2017, iliziagiza Halmashauri kote nchini kubambika na kudai wanachi kile ilichokiita kodi ya pango la ardhi kuanzia mwaka 1996 ,yaani miaka 26 nyuma huku limbikizo hilo likiambatana ya faini za kila mwaka ambao mbakwaji anadaiwa kutolipa na hivyo kufanya wananchi wengi kujikuta wanadaiwa madeni makubwa wasiyoweza kuyalipa!
Kitendo hiki kimesababisha wananchi wengi kujikuta wanashindwa kupata hati miliki za ardhi zao wakitakiwa kwanza walipe na kumaliza deni hilo lililokadiriwa toka mwaka 1996 . Hata hivyo wakati serikali ikifanya hivyo kuna wananchi kila mwaka walikuwa wakilipa kodi ya majengo “Property Tax” ambayo Ankara zake za madai zilikuwa zikitolewa kupitia ofisi za kata na serikali za mitaa.
Hivyo sababu aliyoitoa Mheshimiwa Rais ni ya kupongezwa sana kwani kama kulikuwa na umuhimu wa kudai hizo kodi , Basi wahusika walitakiwa kudai hizo kodi zote kwa pamoja yaani kodi ya jengo na kodi ya pango la ardhi na sio nyingine kuanza kuidai baada ya miaka 20 na hivyo kubambika madeni kwa watu wasiohusika kwani katika kipindi cha miaka 20 kuna watu wameuza na kununua ardhi toka kwa wamiliki wengine.
Zipo pia Bili za maji, Bili za umeme na leseni za biashara, Kuna familia za wananchi wanadaiwa madeni ya maji na umeme ya tangu miaka ya 2000, wazazi wa familia walishafariki lakini familia bado zinapelekewa Ankara za kudai madeni hayo. Hivyo mbali ya kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuingilia kati suala la kudai kodi za miaka ya nyuma tunaiomba pia serikali ipanue wigo wa msamaha huu ili ukahusishe pia na kodi za pango la ardhi na madeni ya tozo nyingine ambazo zina malimbikizo ya madeni ya miaka mingi.