DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Pongezi hizo za Wananchi wa Buchosa zimetolewa baada ya kupata mbolea za kupandia kwa wakati kwenye msimu huu wa kilimo ambapo mvua zimeanza kunyesha.
Juhidi hizi zote zimetokana na uongozi wa Rais Samia kwa kuhakisha wakulima wa Tanzania wanapata pembejeo za kilimo kwa wakati.
Kwa upande wake Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema mbolea ilitakakuchelewa kidogo lakini alichukuwa jukumu la kumpigia simu Chongolo na mbolea hiyo iliwahishwa na wananchi wanafurahia.
"Nampongeza kwa dhati Waziri wa Kilimo, Daniel Chingolo kwa kazi nzuri anazofanya kwa kuwajali wa kulima wakati huu wa msimu wa kilimo kwa kuwapati mbolea ya kupandia kwa wakati," amesema Shigongo.
Naye, Ofisa Kilimo Halmashauri ya Buchosa, Nestori Mjojo amesema mbolea ipo ya kutosha na mbegu za mahindi kutoka kwa Wakala wa Mbegu ya Taifa ASA nayo ipo ya kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wakulima.
Upande wa Diwani wa Kata ya Nyanzenda, Ibrahimu Mbatta amesema kuwahi kwa mbole ya kupandia pamoja na mbegu za mahindi imekuwa mkombozi kwa wakulima wa Buchosa.
Amesisitiza kuwa anaamini msimu wa mavuno utakapofika wakulima watavuna mavuno mengi na ya kutosha.