Katika nchi ileee, nchi nzuri ya kupendeza, wengine wanadiriki kusema nchi ya maziwa na asali,wakati uleeee na kipindi kileeee cha watu waleeee ilifika mahala watu waleeee walianini siasa ni biashara, siasa ni kazi, siasa ni njia kuu ya kujipatia kipato
Hali hiyo, katika nchi hiyo ilipelekea watu wengi wa nchi hiyo hasa kundi kubwa la watu wenye nguvu za kufanya kazi(vijana) kujiingiza katika siasa za nchi ileeee
Bahati nzuri ama mbaya, katika nchi hiyoooo, akatokea kiongozi miongoni mwao, wengi wao wakiamini atakuwa kama waleeee, la hasha kiongozi huyo wa nchi hio alikuwa ni tofauti, mwenye maono tofauti na mitizamo tofauti
Kiongozi huyo alijaribu kufuta mtazamo wa watu wengi wa nchi hiyoooo, waliodhani siasa ni kazi na si utumishi wa kutumikia watu kwa maslahi ya watu wengi
Katika kufanya hivyo, kiongozi huyo wa nchi hiyo, wapo waliomwona kama mkombozi, na wapo waliomtazama kama adui na mtu hatari kabisa kwa ustawi wa maslahi yao binafsi
Wahenga walisema wakati ukuta!!!!