Rais wetu Dkt Magufuli ni mkombozi wa wanyonge, shujaa mpya katika bara la Afrika

Katika nchi ileee, nchi nzuri ya kupendeza, wengine wanadiriki kusema nchi ya maziwa na asali,wakati uleeee na kipindi kileeee cha watu waleeee ilifika mahala watu waleeee walianini siasa ni biashara, siasa ni kazi, siasa ni njia kuu ya kujipatia kipato

Hali hiyo, katika nchi hiyo ilipelekea watu wengi wa nchi hiyo hasa kundi kubwa la watu wenye nguvu za kufanya kazi(vijana) kujiingiza katika siasa za nchi ileeee

Bahati nzuri ama mbaya, katika nchi hiyoooo, akatokea kiongozi miongoni mwao, wengi wao wakiamini atakuwa kama waleeee, la hasha kiongozi huyo wa nchi hio alikuwa ni tofauti, mwenye maono tofauti na mitizamo tofauti

Kiongozi huyo alijaribu kufuta mtazamo wa watu wengi wa nchi hiyoooo, waliodhani siasa ni kazi na si utumishi wa kutumikia watu kwa maslahi ya watu wengi

Katika kufanya hivyo, kiongozi huyo wa nchi hiyo, wapo waliomwona kama mkombozi, na wapo waliomtazama kama adui na mtu hatari kabisa kwa ustawi wa maslahi yao binafsi

Wahenga walisema wakati ukuta!!!!
 
Acha upuuzi wako, siasa ni kazi kama kazi zingine na wanasiasa ndiyo wanaongoza kwa kuishi vizuri,(Rais, Mawaziri, Wabunge, Ma-RC, Ma-DC, Ma-DED, Ma-DAS na Mabalozi) n.k
 
Acha upuuzi wako, siasa ni kazi kama kazi zingine na wanasiasa ndiyo wanaongoza kwa kuishi vizuri,(Rais, Mawaziri, Wabunge, Ma-RC, Ma-DC, Ma-DED, Ma-DAS na Mabalozi) n.k

Wewe ni ndio mpuuzi kabisa, nani alikwambia DED na DAS ni wanasiasa????
Hao ni watumishi wa umma
 
Akili hazikutoshi, waliochaguliwa ni nje ya system siyo kama enzi ya Kikwete(kupandishwa wakuu wa idara) wengi wao ni wale walioshindwa kwenye kura za maoni.

Ma RAS, DED au DAS ni watumishi wa umma, hata kama aliyeteuliwa ni mwanasiasa, atatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo
 
Huyu jamaa atawadanganya walio vijijini kwamba ni wanyonge huku mjini kila mtu mjanja na hakubaliki..wanyonge wapo bush huko wasio jitambua cc Tabora, Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Simiyu, etc
 
Tangu mlivyoanza kumpamba hajang'aa tuu?.... 'Chema chajiuza kibaya cha jitembeza' huhitaji kumpamba wacha ajipambanue kwa matendo yake... kila mmoja atampa thamani kwa kadri atakavyojiainisha. Zaidi ya hapo itakuwa ni 'debe tupu haliachi kuvuma'

"A voice of one calling in the wildernes"
 
Huo ndio ubovu wake unaofanya aonekane hawezi maana kphaiwezekana ukashindwa mengi na ukaweza machache halafu tukuite mshindi eti kisa tu kuna machache umeshinda huo ni ujinga, bora kikwete aliye shindwa machache lakin mengi aliyaweza tofauti kabs na hali ya sasa.
 
Kwa sababu ametoka gerezani au alikuwa serikali hiyo hiyo miaka zaidi ya 25. Mungu atakulaani kutokana na machozi ya hao wanyonge wanaolala barabarani usiku wa leo.

Tumwombe mungu akufikishe hapo unapoomba awasaidie kwa sababu unajua maisha yako, wanaoteseka kweli, wenye maumivu ya maisha aliyoyasababisha ccm na wewe mnafiki.
 
Ni kiongozi mzuri ila kinachomwangusha ni masuala ya uchumi na demokrasia tu
 
Kweli ila nahisi Kuna tatizo sehemu maana tunaolia njaa huku kitaa ni sisi watu wa Hali ya Chini, nahisi Kuna mambo flan flan hayajakaa vizuri bado, ila vute subira

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rais Dr Magufuli tunamuombea awe na afya njema ya kuongoza, kwani nchi ilikuwa imefika pabaya sana. Ilikuwa mfanyakazi yeyote katika ngazi za kati au juu kama walikuwa wapinga rushwa, waadilifu, na wachapakazi walikuwa wanafukuzwa kazi au kuhamishwa au kustaafishwa simply kwa sababu ya uadilifu, sasa Rais kabadilisha kila kitu na anazidi kunyoosha Watanzania na kurudisha nidhamu katika taifa.
 
Kasoro aliyonayo ni kubwa kuliko sehem ambazo yupo perfect

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…