Salute to madam you did well and excellent
View attachment 3601715
Hivi wewe ni mzima kabisa, au zinakuja na kupotea? Watu tunafungua haraka ili tuone hayo makubwa aliyoyafanya Samia, wewe unatuonesha picha za bendera!! This is really crap!
Nendeni shule, msipende elimu za kuunga unga. Unapoleta taarifa iwe inayojitosheleza. Hiki ulichokileta hapa ni uchafu.!
Siku nyingine ukitaka kuleta taarifa, uwe umetulia akili kwanza, usiwe kwenye mihemko, orodhesha hayo mambo aliyoyafanya Samia ambayo unayaona ni mambo mazuri au makubwa. Ninyi mmefanya Samia kama vile mdori,.mnamwandika kila wakati kama vile ni ngoma ya kuchezea. Kumtajataja mtu bila sababu ya msingi msidhani mnamjenga, mjue mnamdhalilisha.
Hata Mungu wa mbinguni , kwenye amri alizompa Musa, mojawapo ilikuwa, usitaje bure jina la Mungu wako. Mungu siyo mtani wako, hivyo isimtaje bure bila sababu.
Na wewe kama unampenda Samia au unamheshimu, usimtaje hovyp hovyo bila sababu. Unapomtaja ovyo, unamtengenezea mazingira ya ama kusemwa vibaya au kudhalilishwa.