Rais William Ruto Amteua Charles Owino kuwa Msemaji Mpya wa Serikali, Isaac Mwaura Apandishwa Cheo

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Rais William Ruto amefanya mabadiliko katika uongozi wa Serikali baada ya kumteua aliyekuwa msemaji wa zamani wa Polisi, Charles Owino, kuwa Msemaji mpya wa Serikali akichukua nafasi ya Isaac Mwaura.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei, Mwaura amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Ofisi ya Diversity, Inclusion and Disability Rights ndani ya Ofisi ya Rais.

Charles Owino, ambaye alikuwa akihudumu kama Kaimu Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya ICT, sasa atakuwa sauti rasmi ya Serikali katika kutoa taarifa za serikali, sera na majibu kuhusu masuala ya kitaifa.

Mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango mpana wa Rais Ruto wa kupanga upya viongozi waandamizi serikalini, huku yakianza kutekelezwa baada ya kuidhinishwa na Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Source: thestar.co.ke
 
Inatuhusu nini? Kwanini unashobokea nchi ya watu? Umewahi kuona wakenya wakiandika jambo lolote nzuri kuhusu Tanzania zaidi ya ubaya?

Ndiyo ile unakuta dereva ameweka bendera ya Kenya kwenye kioo cha gari yake au unakuta kijana amevaa bangili bendera ya Kenya!

Umewahi kuona bendera yetu kwao? Jifunzeni ubinafsi acheni ulimbukeni ukizingatia wanawadharau
 
Haya mwenzetu tuambie umejuaje kama huyo si Mkenya aliyeleta taarifa? Na kwanza taarifa ipo jukwaa la Kenya. Nani anashoboka na mwenzake sasa?
 
Inatuhusu nini? Kwanini unashobokea nchi ya watu? Umewahi kuona wakenya wakiandika jambo lolote nzuri kuhusu Tanzania zaidi ya ubaya?

Ndiyo ile unakuta dereva ameweka bendera ya Kenya kwenye kioo cha gari yake au unakuta kijana amevaa bangili bendera ya Kenya!

Umewahi kuona bendera yetu kwao? Jifunzeni ubinafsi acheni ulimbukeni ukizingatia wanawadharau
Acha makasiriko mkuu we unajua jukwaa hili n kwa ajil ya WATANZANIA tu
 
Back
Top Bottom