Kwanza inafaa ikuingie kwamba nchi zetu hizi hazikua na watu tangia mwanzo, mababu zetu walihamia tu, labda huwa hampewi hiyo elimu shuleni, ni kwamba hayo makabila ya Tanzania yalihamia kutoka kwa mataifa mengine, Wanyamwezi waliingia Tanzania kwenye karne ya 17, huo ni mfano mmoja tu na kila kabila lina historia yake.
Hivyo sisi tulichokifanya kwa Wamakonde na hawa Wahindi ni kuidhinisha uwepo wa jamii zao na kuzitambua kikatiba kama jamii za Kenya. Wao walikuja tu kama jinsi jamii zingine zilivyokuja. Kwa mfano jamii yangu ya Wakikuyu walitokea kule Kongo, wakapitia hapo Tanzania na kuishi Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka 1,000 ndio hatimaye wakahamia huku Kenya. Hivyo itakua unafiki kutotambua jamii zingine ambazo zilihamia huku kihivyo kabla Kenya haijawa taifa huru.
Nyie hapo mnajiita Watanzania leo, lakini hiyo ni baada ya mzungu kuja na kuchora chora mipaka baina ya Waafrika na kuanzia hapo akawaambia mjiite Watanzania au mwanzo Watanganyika, na sisi akatuambia tujiite Wakenya. Huko kwenu kuna jamii zaidi ya 120 zinazotambuliwa na katiba yenu, hivyo wacha kubwatuka maana hamna utofauti wowote na Waafrika wengine.
Tatizo ni kwamba nyie mumetelekeza tamaduni na asili zenu kiasi cha kuwa kama watumwa wasiojua historia au asili yao. Utakuata asilimia kubwa ya Watanzania hawajui hata kuamkuana kilugha, utumwa kabisa huo.