Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Raisi Paul Kagame leo mchana ameridhia kupandishwa vyeo vya ngazi ya brigedia jenerali na cheo cha kanali kwa maofisa kadhaa wa jeshi la Rwanda.
Hatua hii yafuatia hatua ya raisi Kagame kumteua waziri mpya wa ulinzi Juvenal Marizamunda, mkuu mpya wa jeshi la Rwanda Meja Jenerali Mubarak Muganga na mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Vincent Nyakarundi mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa za kijeshi ambazo vyombo vya mbalimbali vya habari vya Rwanda vimezipata ukiwemo mtandao wa X mabadiliko hayo ni katika hatua ya kubadilisha wanajeshi ambapo wengi ni waso na vyeo au wenye vyeo vidogo kupanda ngazi.
Makanali wawili Justus Majyambere na Louis Kanobayire wamepandishwa ngazi na kuwa cheo cha Brigedia Jenerali huku maluteni kanali Francis Nyagatare, Bi Jessica Mukamurenzi na Mulinzi Mucyo wakipandishwa kuwa makanali kamili.
Brigedia Jenerali Majyambere alikuwa kamanda wa kusimamia jeshi la SADC huko Gabo Delgado.
Kitu ambacho chachochea udadisi ni uteuzi wa meja jenerali Nyakarundi kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi la Rwanda.. Kwa miaka mitano ilopita Meja jenerali Nyakarundi alikuwa mkuu wa idara ya ujasusi na kabla ya hapo pia amekuwa mwambata katika ubalozi wa Rwanda nchini Marekani kwa miaka 10. Huyu ni mbobezi katika masuala yote ya diplomasia, stratejia na uongozi katika jeshi. Nyakarundi aongea Kiswahili, Kifaransa, kinyarwanda na kiingereza ambazo ni baadhi ya sifa bora kabisa katika medani za kijeshi na ujasusi.
Jenerali Muganga twaweza sema ni "righthand man" au mtu wa uzio wa ndani wa raisi Kagame (Inner Circle) ambae amekaa jeshi kwa miaka 30 na kuwa na uzoefu wote ujulikanao. Mengine yatakuwa ni kuongezea au kuweka theluji nyeupe katika keki.
Wanajeshi wengine walopandishwa vyeo ni 30 kutoka ngazi ya Meja kwenda ngazi ya Luteni Kanali, 280 kutoka ngazi ya ukapteni kwenda ngazi ya meja, 40 kutoka uluteni kwenda Ukapteni na 270 kutoka ngazi ya Luteni Usu(Second Leutenant) kwenda cheo cha Luteni.
Halikadhalika wanajeshi wengine wamepandishwa ngazi kama Warrant Officer II kwenda Warrant Officer I, Sajenti Meja II kwenda Warrant Officer II, Staff Sergent kwenda Sergent Major, na Sergent kwenda Staff sergent. Wanajeshi 119 wamepandishwa ngazi kutoka ukoplo kwenda Sergent.
Wanajeshi 4059 wao wamepandishwa ngazi kutoka Private kwenda Ukoplo.
Siku ya Ijumaa wanajeshi wa ngazi za juu wakiwemo Jenerali Jean Kazura na mnadhimu mkuu wa jeshi na mabrigedia jenerali wanne walistaafishwa jeshi na wengine kumaliza mikataba yao wakiwa ni sehemu ya wanajeshi 1167 waliokumbwa na fagio la kuondolewa jeshini.
Maofisa waandamizi wapatao 170 na wanajeshi 992 wote walisitishwa ajira zao kwa ama kustaafu au kumaliza mikataba yao.
Meja Jenerali Nzaramba ambae ni miongoni mwa maofisa wa jeshi walostaafishwa rasmi au kusitishwa kwa mikataba yao, yeye alistaafu rasmi mwaka jana lakini akawa na mkataba maalum akifundisha katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Nasho na kile cha Gabiro kilichoko katika wilaya ya Gatsibo.
Sababu halisi ya kufukuzwa kazi kwa Nzaramba zilotolewa ni upigaji , matumizi mabaya ya fedha za wanajeshi na vitendo vya ufisadi. Sambamba na hatua hiyo ni kufukuzwa kazi kwa kanali Etienne ambae alikuwa ni daktari wa jeshi lakini mwenye kukiuka kwa kiasi kikubwa maadili na miiko ya kazi.
Dr Etienne alikuwa mkuu wa idara ya upigaji picha za Miali ya moto au X-rays katika hospitali ya kijeshi ya Rwanda.