Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ile kampeni ya kuua viongozi na makamanda wa makundi pinzani kwa utawala wa Israel bado haijaonekana kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Raisi Ibrahim raisi wa Iran alifariki kwenye ajali ya ndege miezi 2 iliyopita.Katika uhai wake hakuwa na mzaha na utawala wa kiyahudi huko Israel.Yeye ndiye aliyeamrisha jeshi la nchi yake kuipiga Israel baada ya ubalozi wake kushambuliwa huko Israel.
Kifo cha raisi huyo na waziri wake wa mambo ya nje ambao wote walitajwa wenye misimamo mikali ilitarajiwa kupatikana viongozi ambao wangekuwa baridi dhidi ya utawala huo.Wote wawili waliofuatiia siku za mwanzo tu za uongozi wao wameonekana kuwa na misimamo mikali kuliko waliowatangulia.
Kwa upande wa Hamas,kiongozi aliyechaguliwa kushika nafasi ya Ismail Haniya ndiye kabisa ni mtua asiyetamani hata kukenua meno kwa Israel.Yahya Sinwar ni kiongozi wa Hamas ambaye amesota magereza ya Israel kuliko wote waliomtangulia.Na ndiye anayetajwa na Israel kuwa ni maiti anayetembea na bado amepokea kijiti cha uongozi wa Hamas akiwa na hamasa tele.
Mtu anaweza akajiuliza kwa kuwaua viongozi hao jee Israel imejipatia usalama wake au imejiongezea hasira za maadui zake ?