Kutokana na kadhia ntayoielezea hapa chini ndio niliyasikia manung'uniko ya wazee, kibaya wazee hawajui kama NHIF ina mkurugenzi mtendaji, wazee wanamjua Mama Samia, lawama zote ni Mama Samia,. Hapa ndio kwa mara ya kwanza nimeone wazee waliokunywa maji ya kijani wakiilaani CCM, na mengine mengi.
Wiki iliyopita nimeshuhudia jambo la ajabu kabisa kutoka NHIF, ukiacha kuhuzunika ila limenitafakarisha sana.
NHIF imeanza utaratibu wa kuhakiki kadi za bima, utaratibu ambao haukuwepo kabla, utaratibu ambao umeanza kiholela bila kuwataarifu wanachama wake, utaratibu wa hovyo kama lilivyo shirika lenyewe ovyo.
Wazee wengi wamekuwa na magonjwa yanayowafanya watumie dawa maisha yao yote, wazee hawa wengi wao hawana nguvu za kwenda kila mwezi kuchukua dawa hospitalini kutokana na magonjwa yao, hivyo inalazimu ndugu wa karibu wachukue jukumu la kwenda kuchukua dawa hospitalini.
Chakushangaza NHIF sasa inakataza hawa wazee kuchukuliwa dawa, wanataka hawa wazee wafike wenyewe kuchukua dawa. Hapa ndipo tatizo lilipo. Muda mrefu tumekuwa tunaomba hawa wazee wapewe dawa za muda mrefu (siku 90 - siku 180), ili achukue dawa mara anapoenda kumuona daktari, ila NHIF hawataki, wanataka toa dawa za siku 30 tu.
Hawa wazee wamechangia huu mfuko maisha yao yote ila leo wanaonekana wasumbufu kwa mfuko waliouchangia maisha yao yote.
Kutokana na kadhia hii ilibidi ndugu wawarudie wazee hao majumbani mwao na kuja nao hospitali, kwa namna wazee hawa walivyochoka, wengine wanakuja kwenye wheel chairs, wengi ni wakushikwa mikono, wapo hata wanaotetemeka tu muda wote, yani hao wote wanafanyiwa makusudi na NHIF.
Kwa hiki kinachofanywa na NHIF tutegemee vifo vingi vya wazee kwa kukosa madawa yanayowafanya waendelee kuwepo duniani hapa.
Ni hayo tu.