Raisi Samia umetufanyia mengi mazuri pia, usisahau hili elimu yetu tutumie kiingereza kuanzia chekechea

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
4,177
Reaction score
4,887
Kwanza nakupa pongezi raisi wangu Kwa kutoyumbishwa na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu Kwa hili nakupingeza sana.

Umetufanyia mambo mengi sana mazuri mpaka Sasa nchi imetulia na uchumi wetu umetulia endelea kupiga kazi mama.

Kuna hili jambo la lugha ya kufundishia elimu yetu ya awali Yani chekechea na msingi ni kilio Cha watanzania wengi maana huwa tunamia sana tunapoona watoto wetu wanafanya vibaya katika elimu ya secondary Kwa sababu ya lugha ya kiingereza.

Umefika wakati Sasa wa kutumia lugha ya kiingereza kuanzia chekechea ukilifanikisha hili mama utakuwa umewapa watanzania kitu Cha thamani sana na watakushukuru sana.

Elimu yetu imekuwa Haina dira Kwa sababu ya kuchanganya lugha mama ebu tuondolee hiki kirusi kinacholitafuna Taifa.

Kuna wananchi wengine kipato chao ni kidogo lakini wanalazimika kuwapeleka watoto wao shule zinazotumia lugha ya kiingereza Ili watoto wao wasifanye vibaya pale watakapofika secondary.

Narudia tena mama tunaomba utuondolee hiki kirusi.
 
Ni either kiwe kiswahili mwanzo mwisho, au kiingereza mwanzo mwisho!

Mambo ya kuanza na kiswahili unamalizia kiingereza ni ujinga.
 
Hakuna mazuri aliyofanya lakini hoja yako naiunga mkono.kiswahili kifutwe ili tutumie lugha ya kiingereza.kiingereza kinafursa nyingi kuliko kiswahili.Mtu anasoma Kwa kiswahili darasa la kwanza hadi la Saba halafu akianza kidato Cha kwanza anakuwa haelewi sababu ya lugha ya kiingeleza kutokuijua.
 
Kwanza nakupa pongezi raisi wangu Kwa kutoyumbishwa na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu Kwa hili nakupingeza sana.

Umetufanyia mambo mengi sana mazuri mpaka Sasa nchi imetulia na uchumi wetu umetulia endelea kupiga kazi mama.

Kuna hili jambo la lugha ya kufundishia elimu yetu ya awali Yani chekechea na msingi ni kilio Cha watanzania wengi maana huwa tunamia sana tunapoona watoto wetu wanafanya vibaya katika elimu ya secondary Kwa sababu ya lugha ya kiingereza.

Umefika wakati Sasa wa kutumia lugha ya kiingereza kuanzia chekechea ukilifanikisha hili mama utakuwa umewapa watanzania kitu Cha thamani sana na watakushukuru sana.

Elimu yetu imekuwa Haina dira Kwa sababu ya kuchanganya lugha mama ebu tuondolee hiki kirusi kinacholitafuna Taifa.

Kuna wananchi wengine kipato chao ni kidogo lakini wanalazimika kuwapeleka watoto wao shule zinazotumia lugha ya kiingereza Ili watoto wao wasifanye vibaya pale watakapofika secondary.

Narudia tena mama tunaomba utuondolee hiki kirusi.

Elimu hii hii na lugha yetu ya kujivunia inatosha, Watoto si wanasoma na kufaulu wakitaka au?
 
Back
Top Bottom