Uchaguzi 2020 Rajab Abdul "Harmonize" kugombea ubunge Tandahimba

Uchaguzi 2020 Rajab Abdul "Harmonize" kugombea ubunge Tandahimba

Ila watu tumekuwa tunabaguana na kudharauliana kielimu na tunaona ni kitu cha kawaida kabisa,hasa darasa la saba na form 4 wanaongoza kwa kudharauliwa na kuonekana hawana mchango wowote ule.

Hii sio sawa hasa ukizingatia wengine walishindwa kuendelea na masomo kwa changamoto mbalimbali ila wewe unakuja na kumfanya aonekane hana msaada wowote ni mtu duni kisa kaishia la 7.
 
Ukirejea hotuba ya mheshimiwa rais mikoa ya kusini alikaririwa katika hotuba yake akitamani msanii wa muziki wa bongo fleva Harmoniza awe mbunge.
Ikiwa ni hivi leo muda mfupi uliopita bunge limevunjwa na hiyo kutoa fursa kwa uchaguzi mkuu kuanza.

Hapa niseme tu ni mashaka na ile kauli ni kma mheshimiwa rais alikuwa anamtania Harmonize , lakini nae amejikoki anaingia kwenye mchakato kulitaka Jimbo la Tatahimba amabalo hapo mwanzo lilikuwa mikononi mwa mbunge Katani Ahmed Katani wa cuf ambae baadae alirejea ccm.

Sasa hapa swali hivi ni kweli bwana harmonize atapenya hata katika mchujo wa kura za maoni? Huku ikizingatiwa mbunge Katani amejiunga CCM ili agombee kupitia huko pia Kuna makada wengine wamekipigania chama muda mrefu Sana.

Siasa sio mchezo unaoweza kucheza peke yako unahitaji Sana support kubwa Sana ya mifumo ya kichama kuanzia juu mpaka kwenya mashina. Je bwa huyu amejiandaa vya kutosha ?

Siasa sio music ajipange vya kutosha kijana, vinginevyo mie namtakia Kila la kheri!
 
Mzee wa Uno akanipangie mimi kodi niliyeteswa na National Income,

Maisha safari haki ya Mungu
 
Hao ndio tunawahitaji tuwajaze bungeni na wakina Musukuma, Kibajaji etc

Hao tukipeleka muswada bungeni wanagonga meza tu kuunga mkono hoja maana hata kilichoandikwa ndani hawakielewi.

Bunge la kisayansi 2020-2025 linawezekana, tuwaunge mkono wagombea wa dizaini hii kwa wingi.
Acheni ubaguzi, kwani hao maprofesa wamefanya nini
 
Back
Top Bottom