Mabadiliko yanayotakiwa katika utawala huu sio ya mtu mmoja mmoja, bali ni kwa mfumo mzima. Kwa kumuweka Rakesh, hapo ni sawa na kumwaga pipa la damu baharini ukitegemea kuona bahari ikibadilika rangi.
Wapo viongozi wa mfano wake, lakini wanaonekana kinyume mara tu wanapofanya kazi katika misingi ya uadilifu, hata kama ni wewe MMM, bado ukiingia huko amini utaVAA kama wao (simaanishi nguo mioyo na fikra)
So nivyema wakamspear Rakesh wa watu, kwa utawala ujao.
Maana kwa heshima aliyo nayo katika jamii, ni ndani ya miaka 2 tu, tutamjadili hapa kivingine.
CCM ni mtambo wa kubadilisha, muangalie mzee Pinda alipiga kelele kuhusu mashangigi , suti (eti tuvae vitenge , je unamuona akivaa tena vitenge vya mwatex?NIDA?KTM? waapiii), keshabadilika mzee wa watu, ndo alikuwa mbele kabisa katika suala la uchakachuzi sumbawanga mjini SIO PINDA YULEEE!! CCM hiyo MMM.
Maoni yangu atakuwa kama wao we need overhaul ya system yoote sio kwa Maghembe tu, ni kuwanzia Mzee Mwenyewe mpaka afsa mtendaji wa kata unayokaa.