Elections 2010 Rakesh Rajani Kuukwaa Uwaziri? Elimu..?

Elections 2010 Rakesh Rajani Kuukwaa Uwaziri? Elimu..?

Lakini inadaiwa kuwa kwa siasa za Kiswahili Swahili kama zetu mawaziri wenyewe ni political balloons tu lakini watendaji wakuu ni makatibu wakuu wa wizara.
 
Utaelewa baada ya baraza la mawaziri kutangazwa. Vinginevyo.

Vipi mzee wetu mpendwa TingaTinga yupo kwenye zile nafasi kumi za upendeleo?

Aliahidi kumrudisha Six madarakani lakini naona hakuwa ameangalia ule upepo wa 70% ulikuwa unavuma kwenda wapi.
 
Huyo jamaa anawatumia baadhi ya wanajamii kumpigia kampeni,basi tugawane mlichohongwa na huyo RR!
 
Mimi sioni matumaini yoyote yatakayo toka ndani ya serikali ya CCM. Tuweni wavumilivu tu mpaka hapo 2015. Watu wote waliowazuri nchi hii hawataweza kuperform ndani ya serikali ya CCM.

Tuweni wakweli tusijidanye kupata chochote katika miaka hii mitano maana ni miaka ya mafisadi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. There is no Positive change in this country which willl come under Fisadi's Governmament. Forget itiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..

Mabadiliko ya kweli ni 2015 kila mtu amejiandaa kisaikolojia hata CCM wanajua hilo hivyo hakuna atakaye zuia.PEOPLE'S POWERRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRRR!
 
ndoto zingine bwana ccm ina wenyewe na rr si miongoni wa wamiliki wake hivyo basi hili kwangu ni ndoto ya mchana na itabaki kuwa hivyo!
 
Hao kina Erasto Mpemba tunao wengi tu ila wanarudishwa nyuma na siasa chafu na uongozi mbovu unaoua mianya ya uvumbuzi - aisee umemcheki yule dogo wa Kenya aliyevumbua taa ya sola kwa ajili ya vijiji vyetu?

Hata siasa bora na uongozi mzuri unavumbuliwa pia. Bila uvumbuzi hakuna maendeleo. Wewe endelea kubisha tu.

Halafu hivi huna mwingine zaidi ya huyo Mpemba?
 
wewe uko nchi gani wewe ndugu yangu....
we toka lini ukaona mtu anaweza kubadili fikira za mwenyekiti wa CCM...
Angalia Kina Magufuli, Mwakyembe, Anna Kilango nae karibia achinjiwe baharini...
Ndani ya CCM hakuna cha maana atakachoweza badilika bora abaki zake na ile Taasisi Mpya..

CCM imeoza na ukiingia lazima unuke huu sio ushabiki ndo kweli yenyewe kama huamini ( karushe Almasi ****** uone kama itarudi ikiwa ina harufu nzuri)
Mwishowe wakiona kawaingilia sana utasikia tunaambiwa katimuliwa uwaziri kwa sababu si Mtanzania... Muulize Jenerali Ulimwengu....

Punguza ushabiki mshkaji. Its not good for your soul. And tone down your cynicism. Its not good for your soul either. Ni ka ushauri tu.
 
Hata siasa bora na uongozi mzuri unavumbuliwa pia. Bila uvumbuzi hakuna maendeleo. Wewe endelea kubisha tu.

Halafu hivi huna mwingine zaidi ya huyo Mpemba?

Mkuu, nadhani hakuna uvumbuzi mpya unaohitajika, vitu vizuri vinafahamika, tatizo ninaloliona CCM wamejengea mfumo wao kwa ''kokoto na simenti kali'' . Uongozi bora hauwezi kuwepo kama hakuna siasa safi, vilevile huwezi kuwa na siasa safi bila ya uongozi bora. Suala la msingi ni kwa namna gani uongozi bora unapatikana. Uongozi bora unawekwa na wananchi. Bahati mbaya kuna uongozi mbaya unaozuia wananchi kuchagua viongozi bora. Ukiendelea kunyumbulisha ni kuwa msingi wa vyote viwili, uongozi bora na siasa safi ni wananchi. Kwa hiyo Watanzania ndiyo wenye nguvu ya kuamua kukataa uongozi mbaya na kuuweka mzuri ambao utachochea kuwepo kwa siasa safi na uongozi bora. Kwa sasa hivi uongozi wa juu uliokuwepo, yaani rais na serikali yake sio wa wananchi, hivyo hauwezi kuweka siasa safi na wala hauwezi kuruhusu uongozi bora kuwepo. Kama JK na CCM wangekuwa wapo kwa ajili ya wananchi wangeshatekeleza mawazo yake. Rajesh Rajani hataweza kufanya lolote, afadhali akatae uteuzi kama atapewa, abaki huko aliko kama taasisi inayotoa mawazo mbadala hadi watanzania tutakapoweza kutumia nguvu tulizonazo kuweka uongozi bora na kuondoa uongozi mbaya.
 
RR hakika as an individual may be very difficult 4 him 2 change or deliver simply because the main problem in our country is the system itself. The bad input because of the bad system bring bad results. That.s is our main problem.
 
Lakini kama si RR ni nani ambaye tayari yuko CCM ambaye tunaweza kusema akipewa Wizara ya Elimu miaka mitano ijayo hakuna mtoto atakayekuwa anasoma akiwa amekalia tofali au mchanga?
 
Kwa muundo na utendaji kazi wa serikali ata-end up kwenye frustrations. Ni bora abaki HAKIELIMU kuipa changamoto serikali kuliko kwenda kumnyamazisha
 
Lakini kama si RR ni nani ambaye tayari yuko CCM ambaye tunaweza kusema akipewa Wizara ya Elimu miaka mitano ijayo hakuna mtoto atakayekuwa anasoma akiwa amekalia tofali au mchanga?

Pamoja na kuwa thredi yako inahusu elimu, naangalia katika mapana yake, yaani sekta zote. Ninachokiona hakuna haja ya kufikiria nani awepo wapi katika mfuno huu wa CCM (angalia posti #72). Vita inatakiwa ipiganwe bungeni, na huku nje ya bunge wananchi tuendelee kudai stahili yetu. Ndiyo maana ukimya wa Slaa ambaye yupo nje ya CCM ni pigo kwa shinikizo la wananchi kwa serikali ambalo lilikuwa limeshika kasi, kuwalazimisha watawala kuelewa kuwa madaraka ya kuongoza nchi yapo kwa wananchi, siyo watawala. Kumbuka nguvu ya umma iivyofanya kazi wakati Zitto alipofukuzwa bungeni, Slaa alipotaja mafisadi na wananchi walivyolinda kura.
 
Mabadiliko yanayotakiwa katika utawala huu sio ya mtu mmoja mmoja, bali ni kwa mfumo mzima. Kwa kumuweka Rakesh, hapo ni sawa na kumwaga pipa la damu baharini ukitegemea kuona bahari ikibadilika rangi.

Wapo viongozi wa mfano wake, lakini wanaonekana kinyume mara tu wanapofanya kazi katika misingi ya uadilifu, hata kama ni wewe MMM, bado ukiingia huko amini utaVAA kama wao (simaanishi nguo mioyo na fikra)

So nivyema wakamspear Rakesh wa watu, kwa utawala ujao.

Maana kwa heshima aliyo nayo katika jamii, ni ndani ya miaka 2 tu, tutamjadili hapa kivingine.

CCM ni mtambo wa kubadilisha, muangalie mzee Pinda alipiga kelele kuhusu mashangigi , suti (eti tuvae vitenge , je unamuona akivaa tena vitenge vya mwatex?NIDA?KTM? waapiii), keshabadilika mzee wa watu, ndo alikuwa mbele kabisa katika suala la uchakachuzi sumbawanga mjini SIO PINDA YULEEE!! CCM hiyo MMM.

Maoni yangu atakuwa kama wao we need overhaul ya system yoote sio kwa Maghembe tu, ni kuwanzia Mzee Mwenyewe mpaka afsa mtendaji wa kata unayokaa.
 
Mkuu, nadhani hakuna uvumbuzi mpya unaohitajika

Mtazamo wako si wa kimaendeleo kabisa!! Utasemaje unadhani hakuna uvumbuzi mpya unaohitajika? Mitazamo kama hii ndiyo iliyotufanya tudumae kimaendeleo
 
Back
Top Bottom