Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #21
Mwalimu alisema ili nchi iendelee inahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Naona tumejikita katika kutafuta watu tunaoona kuwa ni bora - Rakesh Rajani, Anna Tibaijuka n.k. Ila hata uwe na watu makini na waliobebea kiasi gani kama huna siasa safi na uongozi bora huwezi kufika popote. Sana sana utaishia kuwatibua tu watu hao wenye uwezo. Historia yetu haidanganyi - rejea yaliyomkuta John Magufuli!
Lakini yawezekana kuwa na siasa safi na uongozi bora bila ya watu wenye siasa safi na wenye kuleta uongozi bora?