Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Michuano ya soka iliyochukuliwa kama burudani kwa wale waliofunga Ramadhan, huku wakisubiri daku.
Sasa ni Rasmi imegeuka na kuwa mipango ya kampeni ya CCM, bado hatujajua kama jambo hili ni Bahati mbaya au ni kitu kilichopangwa na waandaaji, na bado hatujajua kama timu zote zinazoshiriki zimekubali kutumiwa na CCM badala ya dini ya kiislam inayohusika na mwezi wa Ramadhan au la.
Bali itakuwa aibu na laana kubwa mbele ya Allah kwa michuano hii kutumiwa na CCM, chama ambacho kwa karibu miaka 70 kimeshindwa kukomboa wananchi kwenye lindi la umasikini.
Akizungumza baada ya kupewa nafasi wakati wa pambano kati ya K4S na Instanbul, Bwana Ally Bananga amemshukuru Rais kwa kukuza michezo hadi kufikia mechi za Ramadhan Cup.
Huku akisema CCM haikubaki nyuma kwenye michezo na ndio maana inamiliki timu kwenye ligi kuu , ambayo ni KMC ya Kinondoni, kiukweli sikuwahi kudhani timu ile ni mali ya CCM.
Bali nimesikitishwa sana na Waandaaji wa Ramadhan Cup kuikabidhi michuano hiyo kwa CCM, haya ni sawa na matusi ya nguoni kwa Wapenda soka na hata Waislam waliofunga Ramadhan, yaani viongozi wa ccm ndio mara zote wanakuwa Wageni Rasmi wa mechi hizo.
Mambo yakiendelea hivi nitajitoa rasmi kutazama michuano hii .