Ramadhan Special Thread

1. Kula daku na kuchelewesha kula daku hadi karibu sana na kuadhiniwa alfajiri

Kwa kauli ya Mtume (saw): (Kuleni daku, hakika katika kula daku kuna Baraka) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na inahesabika kula daku kwa kupatikana chakula kingi au kidogo, hata kama ni tama la maji kwa kauli ya Mtume (saw): “Daku uchache wake ni baraka, basi msiache kula daku, hata kama atakunywa mmoja wenu tama la maji, kwani Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanawaswalia wenye kula daku” [Imepokewa na Ahmad.]

Na inapendekezwa kuchelewesha kula daku, kutoka kwa Zaid ibn Thaabit t Anasema: (Tulikula daku pamoja na Mtume ﷺ, kisha tukasimama kuswali (yaani swala ya alfajiri), anasema Anas ibn Malik: nikasema: ilikuwa ni kipindi cha mda gani kati ya kula kwenu hiyo daku na kuswali? Akasema: kiwango cha (kusoma) Aya hamsini) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

- Kunywa wakati adhana inapo adhiniwa

Mtu anaposikia adhana na kinywaji chake kipo mkononi mwake basi anaruhusiwa kunywa hadi amalize; kutoka kwa Abu Hureirah anasema: Amesema (saw): “Atakaposikia mmoja wenu adhana na hali ya kuwa chombo cha kunywea maji kipo mkononi mwake basi asikiweke kando mpaka amalize haja yake ya kutumia hicho chombo” [Imepokewa na Abuu Daud.]

Na wanazuoni wamesema kuhusu hadithi hii ni kwa Yule ambae ana shaka kutokeza kwa alfajiri, ama akihakikisha kuwa alfajiri imetokeza kwa huyu hafai kuendelea kula wala kunywa, na akiendelea kufanya hivyo Saumu yake imebatilika na itamlazimu Ailipe

2. Kufanya haraka katika kufungua saumu

Yapendekezwa kwa aliyefunga kufanya haraka kufungua saumu yake pindi tu anapohakikisha kwamba jua limezama na kuingia jioni.; kwa kauli ya Mtume (saw): (Watu wangali katika kheri pindi wanapoharakisha kufungua saumu zao) [Imepokewa na Abuu Daud.].

Na inapendekezwa mtu kufungua saumu kwa rutab (tende tosa), asipopata rutab basi afungue kwa tende, na hizo tende ziwe ni hesabu isiyogawanyika kwa mbili (kama vile tende moja, tatu, tano na mfano huu), asipopata tende basi na anywe matama ya maji; kulingana na hadithi ya Anas ibn Malik, anasema: “Alikuwa Mtume (saw) anafungua saumu kwa Rutab (Tende Tosa) kabla hajaswali, na ikiwa hakuna Rutab basi alikuwa akifungua kwa tende kidogo hivi, na ikiwa hakuna tende alikuwa akinywa [ Hasaa: alikunywa.] matama ya maji” [Imepokewa na Tirmidhi.].

Na akiwa hakupata kitu chochote cha kufungulia saumu basi atanuia kufungua saumu kwa moyo wake, na hili litamtosheleza kwamba amefungua.

Atakae Funguwa kwa bahati mbaya

Atakapo kula mtu aliyefunga hali ya kudhania kwamba jua limezama na kuingia jioni, au kwa kutoelewa kutokeza kwa alfajiri, kisha ije kum’bainikia kinyume na alivyodhania, basi haimlazimu kwake kuilipa saumu hiyo; kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu U: { Wala si lawama juu yenu mkikosa, lakini (kuna lawama) katika yale ziliyoyafanya nyoyo zenu kwa kusudi } ( Al-Ahzab- Aya 5).

Na kauli yake Mtume (saw): “Hakika ya Mwenyezi Mungu amewaondoshea umma wangu (hawaandikiwi madhambi) kwa jambo watakalolikosea bila ya kukusudia na kwa watakayofanya kwa kusahau, na kwa watakayolazimishwa kufanya (hali ya kuwa wao wenyewe wanayachukia)” [ Imepokewa na Ibnu Maajah.]

3. kuomba Dua wakati wakufungua swaumu

Kwa ilivyo Thubutu kutoka kwa Mtume (saw) Alipokuwa akifunguwa Saumu Akisema: “Kiu imeondoka, na jasho limekuwa majimaji (limeanza kutokeza), na yamepatikana malipo (ya thawabu) apendapo Mwenyezi Mungu” [Imepokewa na Abuu Daud.].

Na amesema Mtume (saw): “Hakika kwa aliyefunga saumu wakati anapofungua kuna dua isiyorudi) [ Imepokewa na Ibnu Maajah.] yaani dua inayokubalika moja kwa moja mbele ya Mwenyezi Mungu U.

4. Kuacha mambo ya upuzi na mambo machafu

Kwa kauli ya Mtume (saw): “Ikiwa ni siku ambayo mmoja wenu amefunga, basi asifanye mambo machafu, [ Yarfuth Kufanya mambo machafu: yatokamana na neno uchafu, nako ni kutamka matamshi mabaya, na vile vile hutumika neno hili kumaanisha tendo la ndoa na vitangulizi vya tendo hili.] wala asikemee wenziwe[ Yaskhab: Yuwakemea: yatokamana na neno kemea, nako ni kubishana na kupiga ukulele.], anapotukanwa na mtu, au anapopigwa vita basi na aseme: Mimi ni mtu niliyefunga” [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

(Yaani ajitahidi kujiepusha kupigana na kutukanana na watu).

Na kwa neno lake Mtume (saw) (Asie acha maneno machafu na kuyatumia basi Mwenyezi Mungu hana haja kwa mtu huyo kuacha chakula chake na kinywaji chake) [Imepokewa na Abuu Daud.]

5. Kuzidisha kwa wingi kufanya Ibada

Kama kusoma Qur’an, na kufanya adhkari kumtaja Mwenyezi Mungu, na kuswali swala ya Tarawehe, na visimamo vya usiku (swala za usiku wakati watu wamelala), na kufanya visimamo vya usiku wa Lailatul Qadri, na kuswali swala za sunnah, na kutoa sadaka, na kuwa mkarimu na kujitahidi katika kufanya mambo ya kheri, na kuwalisha waliofunga wakati wa kufungua saumu zao, na kwenda U’mrah, kwasababu matendo mema siku ya Ramadhani malipo yake yanaongezeka mara nyingi sana, kutoka kwa Ibn Abbas anasema: “Alikuwa Mtume (saw) ni mkarimu kushinda watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibril, na alikuwa Jibril akikutana na Mtume kila usiku wa mwezi wa Ramadhani, ikawa anamfundisha Qur’an (yaani Jibril anamfundisha Mtume Qur’an), basi Mtume (saw) pindi anapokutana na Jibril alikuwa mkarimu katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa” [Imwpokewa na Bukhari.].

6. Kujitahidi kwa Ibada hasa kumi lamwisho katika Mwezi wa Ramadhani

Imepokewa na bibi A’isha t Amesema: (Alikuwa Mtume (saw) likingia kumi la mwisho akijifunga kibobwe [(Shadda mi’zarah) Nikinaya cha mtu kujitihidi katika ibada zaidi kuliko ilivo zowewa. Na kumesemwa ni kinaya cha mtu kujiepusha na mkewe, Almi’zar: ni kikoi nacho nikile kinchovaliwa sehemu chini ya muili.] na akiuhuisha usiku na akiwamsha wakezake[(Ayqadha Ahlahu) akiwatanabahisha kwa ajili ya ibaada na akiwahimiza juu yake.]) [Imwpokewa na Bukhari.]
Imeandaliwa na Kimodomsafi


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…