Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Hivi ndivyo binadamu tunatakiwa kua,kukumbushana mambo ya kheri,unaweza kufanya jambo dogo tu kama la mleta uzi Kumbe kwa MOLA ni jambo kubwa,tumuombe ALLAH atujaalie tuwe ni wenye kukumbushana mara kwa mara mpaka mauti zitapotufika.
Ndugu umefunga?
 
NASIHA ZA RAMADHAN.
1-Anza kwa kuzingatia mwezi huu mtukufu uwe wa kujihesabu, kutenda amali nyingi na kujirekebisha hali yako na uhusiano wako na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) uwe bora zaidi:

2- Kumbuka kwamba huu mwezi ni mgeni ambaye amekutembelea kisha ataondoka, hivyo mpokee mgeni wako na mkirimu kwa mazuri yote anayostahiki.

3-Tahadhari na kutokufunga bila ya sababu au udhuru wowote, kwani kufanya hivyo, Swawm yako haitolipika hata ukifunga mwaka mzima.
 
Assalam alleykum warhmatulah wabaraqatuh

Ndugu zangu mimi jumatatu nilipata ajali, alhamdulilah kiafya niko poa, ila upande wa uchumi siko poa ukizingatia bajaj yangu ndio ilikuwa kila kitu

Sasa kuna rafiki yangu, kwao mashallah amesema niwe naenda kufuturu kwao!

Kusema kweli nafeel shame hii imekaaje mana kwao ni extended family naombeni ushauri.
 
Waalaykum ssalaam warahmatullahi wabarakatuh

Ndugu niliona ile post ya Ajali ila uyo Rafiki ako kma kakualika mwenyewe haina shida we nenda huenda kashaongea na familia yake uyo

Mtoaji rizki ni Allah huu ni mwezi wa kutoa sadaqa sanaa kwaio rafiki ako anataka kupata thawabu kupitia wewe nenda mkuu wala usione haya
 
Back
Top Bottom