Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

[emoji257][emoji257]MTU KAMUINGILIA MKEWE MCHANA WA RAMADHANI KWA SABABU YA UJINGA WAKE


❪[emoji411]❫ السُّــــ☟ـــؤَال : ﺭﺟﻞ ﺟﺎﻣﻊ ﺯﻭﺟﺘﻪ ﻓﻲ ﻧﻬﺎﺭ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻭﻫﻮ ﺻﺎﺋﻢ ﺟﺎﻫﻼ ﺑﺎﻟﺤﻜﻢ ﻭﺑﺎﻟﻜﻔﺎﺭﺓ، ﻭﺑﻌﺪ ﺫﻟﻚ ﺗﺒﻴﻦ ﻟﻪ اﻷﻣﺮ، ﻓﻤﺎﺫا ﻳﺠﺐ ﻋﻠﻴﻪ؟


[emoji404]Swali: mtu kamuingilia mkewe mchana wa ramadhani haliyakuwa kafunga haliyakuwa hajui hukmu yake na kafara yake, na baada ya kumuingilia likambanikia hukmu yake, nini kinampasa juu yake?


❪[emoji411]❫ الجَـــ☟ـــوَاب :ﻣﻦ ﺟﺎﻣﻊ ﺯﻭﺟﺘﻪ ﻓﻲ ﻧﻬﺎﺭ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﻭﺟﺒﺖ ﻋﻠﻴﻪ اﻟﻜﻔﺎﺭﺓ، ﻭﻫﻲ:


[emoji736]Jawabu: mwenye kufanya tendo la ndoa na mkewe mchana wa ramadhani ni wajibu juu yake kafara, nayo hiyo kafara:


ﻋﺘﻖ ﺭﻗﺒﺔ ﻣﺆﻣﻨﺔ، ﻓﺈﻥ ﻟﻢ ﻳﺠﺪ ﻓﻴﺼﻮﻡ ﺷﻬﺮﻳﻦ ﻣﺘﺘﺎﺑﻌﻴﻦ، ﻓﺈﻥ ﻟﻢ ﻳﺴﺘﻄﻊ ﻓﻴﻄﻌﻢ ﺳﺘﻴﻦ ﻣﺴﻜﻴﻨﺎ ﻣﻊ اﻟﺘﻮﺑﺔ ﻭﻗﻀﺎء ﺫﻟﻚ اﻟﻴﻮﻡ،


Kumwacha mtumwa muumini huru, akiwa hakumpata basi atafunga miezi miwili mfululizo, na akiwa hakuweza basi atawapa maskini sitini chakula pamoja na kuomba toba kwa Allah pamoja na kuilipa siku hiyo


ﻭﻻ ﻳﻌﺪ ﺟﻬﻠﻪ ﺑﺘﺤﺮﻳﻤﻪ ﻭﻭﺟﻮﺏ اﻟﻜﻔﺎﺭﺓ ﻣﺴﻘﻄﺎ ﻟﻠﻜﻔﺎﺭﺓ ﻋﻨﻪ، ﻭﻫﻮ ﻳﻌﻴﺶ ﻓﻲ ﻫﺬﻩ اﻟﺒﻼﺩ ﻭﻳﺠﺐ ﻋﻠﻰ ﺯﻭﺟﺘﻪ ﻣﺜﻞ ﻣﺎ ﻭﺟﺐ ﻋﻠﻴﻪ.


Na wala hazingatiwi kuwa ni mjinga kwa uharamu wake na uwajibu wa kafara, ikawa sababu ya kudondoka kafara kwake, nae anaishi katika miji hii na wajibu kwa mkewe yale yaliyo kuwa wajibu kwake."


Fatwa ya lajnah ya kudumu


❪[emoji432]❫ المصْــــدَرُ: ❪فَتــَاوى اللجنَةِ الدَّائمَة, اﻟﺴﺆاﻝ اﻷﻭﻝ ﻣﻦ اﻟﻔﺘﻮﻯ ﺭﻗﻢ (17086❫


══════ ❁✿❁ ══════

[emoji429] [emoji3578] Abou hudaa Al-jaziiriyyi حفظــــــــــه اللــــــــــه تعالــــــــــى ورعــــــــــاه[emoji433]

[emoji257]Mafunzo sahihi ya ndoa[emoji257]




VUNA THAWABU KWA KUSAMBAZA KWA WENGINE[emoji108]

[emoji441]Kua muadilifu us'badili chochote[emoji95]

[emoji257]Mafunzo sahihi ya ndoa[emoji257]
 
1680228085002.png
 
[emoji3521] RAMADHWAAN NI MWEZI WA DU'AA.
ALLAAH (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ANATAJA KUHUSU KUOMBA DU AA BAADA YA KUTUFARIDHISHA SWAWM: [emoji3521]

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

186. Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah:186][emoji432]

Zinaendelea Aayah za kuhusu Swawm baada yake.

[emoji3487]. -KUOMBA MAGHFIRAH NA TAWBAH:

Omba maghfira na tawbah kabla ya alfajiri. Kufanya hivi utakuwa miongoni mwa waja wema Anaowasifu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَبِالأَ سْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ

Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah [Adh-Dhaariyaat: 18][emoji432]

Vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Huteremka nyakati hizo kuweko katika mbingu ya kwanza:

[emoji1607] عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy Na Muslim][emoji431]

[emoji3487]. -KUUNGA UNDUGU NA JAMAA:

Jambo muhimu kulitekeleza siku zote. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametahadharisha kwa anayekata mawasiliano na ndugu au jamaa:

((الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ تَقُولُ: مَنْ وَصَلَنِي وَصَلَهُ اللَّهُ، وَمَنْ قَطَعَنِي قَطَعَهُ اللَّهُ)) رواه البخاري ومسلم

((Fuko la uzazi linaning'inia katika 'Arshi linasema: “Atakayeniunga, Allaah Atamuunga, na atakayenitenga Naye Allaah Atamtenga [Atamkatia]”)) [Al-Bukhaariy na Muslim] [emoji431]
 
[emoji3487] SWALAAH YA TAHAJJUD [emoji3488]

Swalaah ya Tahajjud ni Swalaah inayoswaliwa usiku ambayo pia kwa jina lengine ni Qiyaamul-Layl (kusimama kuswali usiku). Nayo huswaliwa wakati wowote baada ya Swalah ya 'Ishaa mpaka karibu na Alfajiri.

Ama ikiwa mtu anataka kupata fadhila zilizotajwa kuswali katika thuluthi ya usiku kama ilivyo katika Hadiythi ifuatayo:[emoji3593]

[emoji1607] عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim][emoji426]

basi wakati huu wa Thuluthi ya mwisho ni kugawa sehemu tatu kuanzia Swalaah ya Magharibi mpaka Swalaah ya Alfajiri. Sehemu ya tatu ndio Thuluthiy-Llayl (thuluthi ya usiku) ya mwisho

Na huswaliwa ifuatavyo: [emoji3593]

[emoji3490]-Idadi ya Swalaah za Sunnah za usiku:

Jumla ya Swalaah za usiku za Sunnah ni Raka'ah kumi na moja kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba: “Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali usiku Raka'ah kumi na akitoa salaam baada ya kila Raka'ah mbili kisha akiswali Witr Raka'ah moja.” [Muslim][emoji426]

Na akasema vile vile: ”Hajapata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuzidisha katika Ramadhwaan wala miezi mingine zaidi ya Raka'ah kumi na moja, akiswali nne, wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali nne wala usiulize uzuri wake na urefu wake, kisha akiswali tatu.” [Al-Bukhaariy na Muslim][emoji426]

[emoji3490]-Namna zinavyoswaliwa Swalaah za usiku:

Unatoa salaam kila baada ya Raka'ah mbili kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:

((Swalaah ya usiku ni (raka’ah) mbili mbili na ukiogopa kukukuta asubuhi basi Swali Witr [Raka'ah] moja)) [Al-Bukhaariy][emoji426]
 
[emoji3598] CHA KWANZA KINACHOHESABIWA KATIKA A‘AMALI ZA MJA NI SWALAAH [emoji3598]

[emoji1607] عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ، فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ ، وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ، فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ : انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ- فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود والنسائي وابن ماجه وأحمد

Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja Siku ya Qiyaamah ni Swalaah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalaah zake za fardhi Atasema Rabb (Mola) ‘Azza wa Jalla: “Angalia ikiwa mja Wangu ana Swalaah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua?”. Hapo tena amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo))

[At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad][emoji426]
 
[emoji382][emoji382]NASAHA KWA WAFUNGAJI


قَـالَ الشيخ صالح الفوزان حفظه الله :


[emoji404]Amesema Al-allaamah imam swaaleh Al-fawzan (Allah amhifadhi)


فقد يصومُ الصائمُ ويشتدُّ جوعُهُ وعطشُهُ ويشتدُّ تعبُهُ وليس له أجرٌ عند الله -عز وجل بسبب أنه :


Hwenda akafunga mwenye kufunga na ikawa kali njaa yake na kiu yake na ikawa kali tabu yake na hana ujira wewote mbele ya Allah kwa sabau hakika yake:


سلط لسانهُ في الكلام الحرام


Ameutumia ulimi wake katika kuongea mambo ya haramu


وسلط نظره على النظر الحرام


Na akayatumia macho yake katika kuangalia mambo ya haramu


وسلط أذنيه على استماع المحرم


Na akayatumia masikio yake katika kuskiliza mambo ya haramu


فهذا في الحقيقة لم يَصُمْ وإنما ترك الطعام والشراب فقط فهو يتعب بلا فائدة


Basi huyu kwa uhakika hajafunga kwani hakika yake amekiacha chakula na na kichwaji tu nae anapata tabu bila ya faida yeyote


فالصيام يشمل جميع هذه الأشياء :صيام البطن عن الأكل والشرب وسائر المفطرات


Funga inafungamana na mambo yote: kufunga tumbo kutokana na kula na kunywa na vitu vingine vyenye kufunguza


وصيام السمع عن كل كلامٍ محرم


Na kufunga kwa kuskia ni kujizuia na maneno yote ya haramu


وصيام النظر عن كل ما حرم الله النظر إليه


Na kufunga kwa kuangalia ni kujizuia kuangalia kila alicho kuharamisha Allah


وصيام اللسان عن النطق بالفحش والآثام


Na kufunga kwa ulimi ni kujizuia juu ya kutamka meneno machafu na madhambi


فتصوم جميع جوارحه


Basi utafunga mwili wote."


❪[emoji432]❫ المصْــــدَرُ: ❪مجالس شهر رمضان المبارك ص(١٥❫.


••┈•✿•┈•••••°••○••°••••┈•✿•┈••

[emoji3578] Abou huda'a Al-jaziiriyyi حفظه الله



FAWA'AID SHEKH FAUZAN
 
[emoji617]HUKMU YA MTU ANAE SWALI LAKINI HAFUNGI RAMADHANI


❪[emoji411]❫ السُّــــ☟ـــؤَال : ﻫﻞ ﻳﻜﻔﺮ ﺗﺎﺭﻙ اﻟﺼﻮﻡ ﻣﺎ ﺩاﻡ ﻳﺼﻠﻲ ﻭﻻ ﻳﺼﻮﻡ ﺑﺪﻭﻥ ﻣﺮﺽ ﻭﺑﺪﻭﻥ ﺃﻱ ﺷﻲء؟


[emoji404]Swali: je atasamehewa mwenye kuacha funga mda ambao kwamba anaswali na wala hafungi bila ya maradhi na bila ya kitu chochote?


❪[emoji411]❫ الجَـــ☟ـــوَاب : ﻣﻦ ﺗﺮﻙ اﻟﺼﻮﻡ ﺟﺤﺪا ﻟﻮﺟﻮﺑﻪ ﻓﻬﻮ ﻛﺎﻓﺮ ﺇﺟﻤﺎﻋﺎ


[emoji3514]Jawabu: mwenye kuacha funga kwa kupinga uwajibu wake basi yeye ni kafiri kwa makubaliano ya wanawachuoni


ﻭﻣﻦ ﺗﺮﻛﻪ ﻛﺴﻼ ﻭﺗﻬﺎﻭﻧﺎ ﻓﻼ ﻳﻜﻔﺮ ﻟﻜﻨﻪ ﻋﻠﻰ ﺧﻄﺮ ﻛﺒﻴﺮ ﺑﺘﺮﻛﻪ ﺭﻛﻦ ﻣﻦ ﺃﺭﻛﺎﻥ اﻹﺳﻼﻡ ﻣﺠﻤﻌﺎ ﻋﻠﻰ ﻭﺟﻮﺑﻪ


Na mwenye kuacha funga kwa uvivu na kuzembea basi hawi kafiri mtu huyo lakini hakika yake yupo katika hatari kubwa kwa kuiacha nguzo katika nguzo za uislam ambayo anaikili juu ya uwajibu wake


ﻭﻳﺴﺘﺤﻖ اﻟﻌﻘﻮﺑﺔ ﻭاﻟﺘﺄﺩﻳﺐ ﻣﻦ ﻭﻟﻲ اﻷﻣﺮ ﺑﻤﺎ ﻳﺮﺩﻋﻪ ﻭﺃﻣﺜﺎﻟﻪ ﺑﻞ ﺫﻫﺐ ﺑﻌﺾ ﺃﻫﻞ اﻟﻌﻠﻢ ﺇﻟﻰ ﺗﻜﻔﻴﺮﻩ ﻭﻋﻠﻴﻪ ﻗﻀﺎء ﻣﺎ ﺗﺮﻛﻪ ﻣﻊ اﻟﺘﻮﺑﺔ ﺇﻟﻰ اﻟﻠﻪ ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ.


Na anastahiki kupewa adhabu na kutiwa adabu na kiongozi kwa yale anayo yaacha mtu huyo na mfano wake, bali wameenda baadhi katika ulamaa katika kutoa fatwa juu ya kumkufurisha mtu huyo na lazima juu yake alipe kile alicho kiacha katika funga pamoja na kuomba toba kwa Allah (Subhaana wataala)."


Fatwa ya lajnah ya kudumu


❪[emoji432]❫ المصْــــدَرُ: ❪فَتــَاوى اللجنَةِ الدَّائمَة,اﻟﺴﺆاﻝ اﻷﻭﻝ ﻣﻦ اﻟﻔﺘﻮﻯ ﺭﻗﻢ 6060❫.


══════ ❁✿❁ ══════

[emoji429] [emoji3578] Abou hudaa Al-jaziiriyyi حفظــــــــــه اللــــــــــه تعالــــــــــى ورعــــــــــاه[emoji433]

[emoji432]═══ AL-HUDAA DURUUSU ONLINE ═══[emoji432]




VUNA THAWABU KWA KUSAMBAZA KWA WENGINE[emoji108]

[emoji441]Kua muadilifu us'badili chochote[emoji95]

[emoji432]═══ AL-HUDAA DURUUSU ONLINE ═══[emoji432]
 
Back
Top Bottom