Ramadhan Special Thread

Al-Inshiqaq 84:7-12

فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
Basi yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wa kulia.

فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا
hakika atakuwa na hesabu nyepesi Sana,,,ndugu zangu haya mambo hayaji hivi hivi tu bali hatuna budi kufanya matendo mema ambayo ndio Itakuwa sababu ya kupata neema siku ya kiyama.

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا

Atarudi kwa watu wake kwa furaha,, inamaana atarudi kwa watu wa peponi

وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهْرِۦ
Na yule ambaye atapewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake ,,, huyu atapewa kitabu kwa mkono wa kushoto kwa nyuma ukiwa mkono wape umepinda


فَسَوْفَ يَدْعُوا۟ ثُبُورًا

Atalia kwa kuangamia,,, huyu ni muovu na atapata adhabu



وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا

Na ataingizwa motoni

Ndugu zangu katika imani hizi aya zinazungumzia mtu mwema na muovu,,,hakika mtu mwema atapewa kitabu chake kwa mkono wa kulia na ishara tosha kuwa amefuzu,,, huyu hatahojiwa kwa matendo yake.

Lakini huyu muovu atakayepewa daftar Lake kwa mkono wa kushoto huyu ni ishara mbaya ALLAH ATUEPUSHE TUSIWE MIONGONI MWAO, huyu atapata adhabu na kuingizwa Motoni.

Mtume swalla llahu alayhi wasallam anasema hakika yule atakaye hojiwa na Allah ameangamia,, huyu ataulizwa juu hisabu yake.

Ndugu zangu hakika mwezi wa Ramadhani unaondoka alhamdulillah wengi wetu tumekuwa watu wa ibada na matendo mema basi tuweke adhima ya kuendelea na amali njema ambazo zitatufanya tupewe madaftar yetu kwa mkono wa kulia
 
It is obligatory to have belief in the Messengership of the Prophet (Muhammad ). Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: Allah's Messenger (ﷺ) said: "By Him (Allah) in Whose Hand Muhammad's soul is, there is none from amongst the Jews and Christians (of these present nations) who hears about me and then dies without believing in the Message with which I have been sent (i.e. Islamic Monotheism), but he will be from the dwellers of the (Hell) Fire." [Sahih Muslim, the Book of Faith, Hadith No. 153 (S.S.M. 20)] See also the footnotes of (V.3:85), (V.3:116) and (V.84:22).

Sura 3 Ayah 85 note:

a) It is obligatory to have belief in the Messengership of the Prophet (Muhammad ). Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: Allah's Messenger (ﷺ) said: "By Him (Allah) in Whose Hand Muhammad's soul is, there is none from amongst the Jews and the Christians (of these present nations) who hears about me and then dies without believing in the Message with which I have been sent (i.e. Islamic Monotheism), but he will be from the dwellers of the (Hell) Fire." [Sahih Muslim, the Book of Faith, Vol.1, Hadith No. 240 (153) (S.S.M. 20)]. [See also (V.3:116)]

b) The asking of (angel) Jibrail (Gabriel) from the Prophet (ﷺ) about Belief, Islam, Ihsan (perfection) and the knowledge of the Hour (Doomsday), and their explanation given to him by the Prophet . Then the Prophet (ﷺ) said (to his Companions): "Jibrail (Gabriel) ['alayhis-salam] came to teach you your religion." So the Prophet (ﷺ) regarded all that as a religion. And all that which the Prophet (ﷺ) explained to the delegation of 'Abdul-Qais was a part of Faith. (See Sahih Al-Bukhari, Hadith No. 50 and 87) And the Statement of Allah [Subhanahu wa Ta'ala]: "And whoever seeks a religion other than Islam, it will never be accepted of him." (V.3:85).

Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: One day while the Prophet (ﷺ) was sitting in the company of some people, a man came and asked, "What is Faith?" Allah's Messenger (ﷺ) replied, "Faith is to believe in Allah, His angels, (the) Meeting with Him, His Messengers, and to believe in Resurrection."* Then he further asked, "What is Islam?" Allah's Messenger (ﷺ) replied, "To worship Allah Alone and none else, to perform As-Salat (the prayers), to give the Zakat (obligatory charity) and to observe Saum (fasts) during the month of Ramadan,"** then he further asked, "What is Ihsan (perfection)?" Allah's Messenger (ﷺ) replied, "To worship Allah [Subhanahu wa Ta'ala] as if you see Him, and if you cannot achieve this state of devotion then you must consider that He is looking at you." Then he further asked, "When will the Hour be established?" Allah's Messenger (ﷺ) replied, "The answerer has no better knowledge than the questioner. But I will inform you about its portents:

(1) When a slave (lady) gives birth to her master.

(2) When the shepherds of black camels start boasting and competing with others in the construction of higher buildings. And the Hour is one of the five things which nobody knows except Allah."

The Prophet (ﷺ) then recited: "Verily, the knowledge of the Hour is with Allah (Alone)." (31:34). Then that man left and the Prophet (ﷺ) asked his Companions to call him back, but they could not see him. Then the Prophet (ﷺ) said, "That was (angel) Jibrail (Gabriel) ['alayhis-salam] who came to teach the people their religion."

Abu 'Abdullah [radhi-yAllahu 'anhu] said: He (the Prophet (ﷺ) ) considered all that as a part of Faith. [Sahih Al-Bukhari, 1/50 (O.P.47)].

* In this Hadith, only 4 articles are mentioned, while in another Hadith, 6 articles are mentioned: (i) Allah, (ii) His Angels, (iii) His Books (the Torah, the Gospel, the Qur'an and all the other Holy Books revealed by Allah), (iv) His Messengers, (v) Day of Resurrection and (vi) Al-Qadar (Divine Preordainments), i.e. whatever Allah has ordained, must come to pass.

** Again the principles of Islam mentioned here are 4, but in other narrations, they are 5 -- 5th is the pilgrimage (Hajj) to Makkah for the one who can afford it once in a lifetime.

Sura 3 Ayah 116 note:

See the footnote of (V.3:85) and also see (V.4:47) and its footnote.

Sura 84 Ayah 22 note:

It is obligatory to have belief in the Messengership of the Prophet (Muhammad ). Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: Allah's Messenger (ﷺ) said: "By Him (Allah) in Whose Hand Muhammad's soul is, there is none from amongst the Jews and Christians (of these present nations) who hears about me and then dies without believing in the Message with which I have been sent (i.e. Islamic Monotheism), but he will be from the dwellers of the (Hell) Fire." [Sahih Muslim, the Book of Faith, Hadith No. 153 (S.S.M. 20)] See also the footnotes of (V.3:85), (V.3:116) and (V.84:22).
 
Je huwa mara nyingi unajikuta mzito wa kufanya mambo mema?

Basi tambua ndugu yangu katika imani hakika moyo wako umepata kutu ndio maana inakuwa vigumu kwako kufanya matendo mema

Anasema Allah juu ya wale wanao kadhibisha malipo au wanaopinga au hawaamini siku ya malipo ni wale watenda dhambi na wanao ruka mipaka ya Allah,, na kwa matendo yao hayo basi hakika nyoyo zao zinakuwa na kutu na hivyo hawamwamini Allah.

Katika suratil mutafifini Allah anasema

:14 - Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma

Kwahiyo yanayotia kutu katika nyoyo zetu ni madhambi yetu na si kingine,kadri jinsi unavyozidi kufanya dhambi basi moyo wako unazidi kufunikwa na doa jeusi na hivyo hutosikia la mwadhini wala mnadi swala kwa kiswahili kilichozoeleka.

Wewe hutakuwa karibu na mambo ya kheri hata kidogo bali utapenda zaidi mambo ya Shari,,, tuangalie hadith ifuatayo ktk lugha ya kiingereza lkn nitaifasir.


Narrated Abu Hurairah [radhi-yAllahu 'anhu]: Allah's Messenger (ﷺ) said, "When a slave (a person) commits a sin (an evil deed) a black dot is dotted on his heart. Then if that person gives up that evil deed (sin), begs Allah to forgive him, and repents, then his heart is cleared (from that heart covering dot); but if he repeats the evil deed (sin), then that covering is increased till his heart is completely covered with it. And that is Ar-Ran which Allah mentioned (in the Qur'an): "Nay! But on their hearts is the Ran (covering of sins and evil deeds) which they used to earn."

Mtume swalla llahu alayhi wassalam Amesema hakika mja akifanya dhambi basi moyo wake unaweka au kupata doa jeusi, ila kama mtu huyo akiacha dhambi, na kumuomba Allah msamaha basi doa hilo huondoka, na kama akirudia dhambi hiyo tena kwa maana mara nyingi zaidi basi hilo doa hukua mpaka kufunika moyo wake wote,,,, na hiyo Ayah ndio hiyo nilioandika pale juu.

Kwahiyo ndugu katika imani hakika tukijiachia na kufanya madhambi basi ujue itafika kipindi wewe unakuwa huna hofu ya Allah hata kidogo kwasababu tayar moyo wako unakuwa umeharibika na huingizi kitu chochote tena, unakuwa kama makafiri tu ambao wao hawataki kumwamini Allah wala Mtume Muhammad na ujumbe aliokuja nao kwani nyoyo zao zimekufa kabisa.

Kuna hadith moja Rasul wa Allah anasema hakika katika mwili wa mwanadamu kuna pande la nyama,na likitengenea au kuwa safi pande hilo basi mambo yote ya mja yatakuwa mazuri na likiharibika pande hilo basi mambo yote huharibika,kisha akasema pande hilo ni moyo.

Ndugu zangu moyo ndio ogani ya utambuzi wa kumjua Allah, na ndio maana kuna ayah Allah anasema juu ya watu wasio amini Ayah zake kwamba "macho wanayo na hawaoni kwayo, masikio wanayo na hawasikii kwayo na nyoyo wanazo na hawatambui kwazo "

Bimaana tuna macho lakini tunashindwa kuona jinsi uumbaji wa Allah ulivyofanyika na kutafakari juu ya uweza wake, mathalani angalia uumbaji wa mbingu saba bila nguzo, angali sayar yetu na viumbe viliomo hakika mwenye akili yatosha kujua hakika kuna Allah muumba wa vyote.

Tuna masikio tunasikia ayah za Allah na mawaidha lkn hatuzingatii kuwa hakika kuna Allah na tutakuja kuhesabiwa

Nyoyo tunazo lkn tunashindwa kutambua uwepo wa Allah subhanaahu wa taala.

Naihusia nafsi yangu na yako tumche Allah subhanaahu wa taala siku zote.
 
Mtume swalla llahu alayhi wa sallam alisema Umma wangu wote utaingia peponi isipokuwa wale wasio taka wenyewe


Ndugu zangu katika imani hakika inashangaza sana kwa waumini kuingia motoni kutokana na hesabu za matendo mema na maovu na malipo yake.

Jema moja mtu hulipwa mara kumi na huenda mpaka mia saba kutokana ikhlas au utakaso wa Nia yake na Ovu moja hulipwa mara moja tu. Sasa utashangaa siku ya kiama maovu yanakuwa mengi katika mizani kuliko mambo mema hakika huu ni msiba.

Yaan dhambi moja moja zinakuwa nyingi mpaka zinapita mambo mema kweli hii inaingia akilini? Tunafeli wapi waumini?

Katika hadith iliyopokelewa na Abu hurairah (r. a) amesema Mtume swalla llahu alayhi wasallam hakika Allah ameweka Malaika juu yenu ambao wanaandika matendo yenu na amewaelekeza namna ya kuandika, mja akidhamiria kufanya jema moja na asilifanye atalipwa jema moja kamili, ana akidhamiria kulifanya na akafanya jema hilo basi hulipwa mara kumi mfano wake na mpaka mara mia saba na zaidi.
Akidhamiria kufanya ovu moja na asilifanye basi hulipwa jema moja kamili na akidhamiria kufanya ovu na akalifanya basi huandikiwa ovu moja kamili.

Ebu angalia huruma ya Allah subhanaahu wa wataala juu ya viumbe wake

Na ndio maana tunaambiwa ukifanya ovu moja basi haraka sana fuatishia na jambo jema kwasababu jema hufuta ovu, mfano umetukana umeandikiwa ovu moja na ukatoa sadaka ukaandikiwa kumi ina maana kumi mema toa ovu moja unabakiwa na mema tisa,ebu ona jinsi Allah alivyo mkarimu ndugu zangu lkn bado cha kusikitisha bado kuna watu wataingia motoni.

Kuna hadithi nyingine Mtume rehma na amani ziwe juu yake anasema kila baada ya swala za faradhi tuseme subhanallah mara kumi, alhamdulillah mara kumi na allahu akbar mara kumi ina maana jumla ni mara thalathini ukizisha mara tano kwa idadi ya Swala tano jumla unapata mia hamsini, sasa chukua mia hamsini mara thawabu kumi jumla unapata thawabu 1.500

Halafu usiku kabla ya kulala sema subhanallah mara 33 kisha alhamdulillah mara 33 kisha allahu akbar Mara 34 ina maana jumla 100 haya mara thawabu kumi kwa kila jema inamaana unapata jumla 1000,,,haya chukua 1.500 ya awali jumlisha 1000 jumla unapata thawabu 2.500,,kisha Mtume akauliza je kuna mtu ambaye anaweza kufanya maovu 2.500 kwa Siku?

Swahaba akamuuliza Mtume je inakuwaje watu wanaghafirika kufanya hivyo? Mtume akasema akiingia katika swala mmoja anazongwa na shetwani ndani ya swala mpaka akimaliza anasahu kusoma nyiradi hizo na wakati wa kulala anazongwa mpaka usingizi unampitia.

Ndugu zangu ebu angalia ni kiasi gani tutaenda kuadhibiwa kwa kukosa kufanya mambo mepesi kama haya.

Je unaswali? Swala ndio nguzo ya dini na ndio ya kwanza kuhesabiwa siku ya kiama, sasa unaiacha vipi ibada hii kwa mfano.

Allah atuongoze inshallah
 
Skip to main content



Search form​




Ukurasa Wa Kwanza /Zakaatul-Fitwr: Hikmah Na Hukmu Zake

Zakaatul-Fitwr: Hikmah Na Hukmu Zake​

Zakaah-Swadaqah

Zakaatul-Fitwr : Hikma Na Hukmu Zake

www.alhidaaya.com



Nini Makusudio Ya Zakaatul-Fitwr Na Nini Hikmah Yake?

1. Muislamu anayetoka kufunga Mwezi mtukufu wa Ramadhwaan anatakiwa amalizie funga yake kwa kutoa Zakatul-Fitwr kama shukurani kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Kumuwezesha kutekeleza Swawm.

2. Juu ya hivyo, Zakatul-Fitwr itamsafisha mwenye kufunga kutokana na maovu ya ulimi aliyotamka kama maneno machafu na ya upuuzi.

3. Kumuepusha Muislamu na ubakhili.

4. Zakaatul-Fitwr pia itawaepusha masikini na wanaohitaji kutokana na kuomba siku ya 'Iyd.

Hayo ni kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنْ اللَّغْوِ وَالرَّفَثِ وَطُعْمَةً لِلْمَسَاكِينِ مَنْ أَدَّاهَا قَبْل َالصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ الصَّدَقَاتِ". رواه أبو داود قال النووي : رَوَاهُ أَبُو دَاوُد مِنْ رِوَايَةِ ابْنِ عَبَّاسٍ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ

Kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Zakaatul-Fitwr iwe ni fardhi kwa ajili ya kumsafisha aliye funga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu, na kwa ajili ya kuwalisha masikini. Atakayeitoa kabla Swalah basi ni Zakaah iliyokubaliwa, na atakayeitoa baada ya Swalah itakuwa ni sadaka" [Abuu Daawuwd, na kasema An-Nawawy amesimulia Abuu Daawuwd katika riwaaya ya Ibn 'Abbaas kwa isnaad nzuri]


Hukmu Zake:

Zakaatul-Fitwr Ni Fardhi Kwa Kila Muislamu


Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa kila Muislamu, mkubwa na mdogo, mwanaume na mwanamke, aliye huru na mtumwa. Hii ni kutokana na usimulizi Swahiyh ufuatao:

عَن ْابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: " فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ صَاعًا مِنْتَمْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ عَلَى الْعَبْدِ وَالْحُرِّ وَالذَّكَرِ وَالأنْثَى وَالصَّغِيرِ وَالْكَبِيرِ مِنْ الْمُسْلِمِينَ". البخاري

Kutoka kwa bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma): "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa mtumwa na aliye huru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa miongoni mwa Waislamu kwa kutoa swaa' moja ya tende kavu au swaa’ moja ya shayiri." [Al-Bukhaariy]

* swaa’ moja = kilo mbili na nusu (mteko) viganja viwili vya mkono vya mtu wa wastani vilivyojaa mara nne.

Hivyo ni wajibu wa kila Muislamu atoe Zakaatul-Fitwr kwa ajili yake na kwa ajili ya familia yake na wote waliomo katika jukumu lake.



Nani Apasaye kutoa:

Yeyote mwenye uwezo na hata mwenye kumiliki chakula cha siku moja ajitolee mwenyewe pamoja na watu wake wote ambao wako chini ya jukumu lakekama mke, watoto, wazazi ambao hawana kipato.

Ikiwa mtoto amezaliwa baada ya kuzama jua usiku wa kwanza wa 'Iyd (siku ya mwisho ya Ramadhwaan) naye inapendekezeka kumlipia kwa sababu 'Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) alifanya hivyo ingawa sio fardhi.


Nani Apokee

Ingawa ‘Ulamaa wengine wameona kuwa ni sawa na watu wanopasa kupokea Zakaah ya mali lakini rai iliyo sahihi kabisa na inayokubalika zaidi ni kwamba itolewe kwa maskini na wenye kuhitaji pekee.


Wakati gani wa kuitoa

Wakati unaopendekezeka zaidi ni kuanzia Magharibi ya siku ya mwisho ya Ramadhwaan hadi asubuhi kabla ya Swalah ya 'Iyd.

Pia inaweza kutolewa siku moja au mbili kabla ya 'Iyd kama ilivyokuja dalili katika Swahiyh Al-Bukhaariy kwamba, "Walikuwa (yaani Maswahaba) wakitoa (wakiwapa masikini) kabla ya Fitwr kwa siku moja au siku mbili."

Haipasi kutoa baada ya Swalah kwani huwa si Zakaah tena bali huwa ni sadaka kama alivyosimulia Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma)

"...مَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ الصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ الصَّدَقَاتِ". رواه أبو داود
"Atakayetoa kabla ya Swalah itakuwa ni Zakaah iliyokubaliwa na atakayetoa baada ya Swalah itakuwa ni miongoni mwa sadaka" [Abuu Daawuwd]


Kitu gani kutoa?

Ni chakula kinachotumiwa na watu zaidi katika mji kama ni shayiri, au tende kavu, au mchele n.k. hii ni kutokana na dalili ifautayo:

قال أبوسعيد الخدري رضي الله عنه: "كنا نخرج يوم الفطر في عهد رسول صلى الله عليه وسلم صاعاً من طعام ، وكان طعامنا الشعير والزبيب و الأقط والتمر" أخرجه البخاري

Kutoka kwa Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allahu 'anhu): "Tulikuwa tukitoa siku ya Fitwr zama za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) swaa' ya chakula na kilikuwa chakula chetu ni shayiri, zabibu, jibini na tende" [Al-Bukhaariy]


Kiwango cha kutoa:

Ni swaa' moja ya chakula ambayo ni sawa na kilo mbili na nusu, au miteko ya mikono miwili ya mtu wa wastani mara nne. Hii ni kutokana na kauli ya:
Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa' moja ya chakula, au swaa' ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa' ya tende au swaa' ya aqit (mtindi mkavu) au swaa' ya zabibu." [Al-Bukhaariy]


Kutoa Pesa Inaruhusuiwa?

Haipendekezwi kutoa ila tu ikiwa hawapatikani masikini wa kupewa chakula katika mji. Ikiwa hivyo, basi kukusanywa pesa na watu wenye kuaminika na kutumwa katika nchi ambazo zina masikini zaidi na huku wawanunulie chakula kinachopaswa kugaiwa. Kwa hali hiyo imeruhusiwa.










 
Tukiwa tunakaribia mwishoni kabisa mwa mwezi wa Ramadhani ebu tukumbushane mambo machache

Ramadhani huwa inaingia na watu wake na kutoka na watu wake,,, kwa maana wale wanaomjua Allah tu kupitia mwezi huu humwabudu Allah na kisha mwezi ukiisha nao hao wanaondoka na mwezi wao inna lilah waina ilaih rajiuun.

Ni katika mwezi kama huu nilikata shauri huko miaka ya nyuma kuwa sasa naendeleza kumwabudu Allah baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha na alhamdulillah namshukuru Allah kwa taufiki yake nadumu na ibada mpaka leo,,, na wewe ndugu yangu katika imani unaweza kabisa kikubwa ni kukata shauri tu.

Allah anasema Habadilishi hali za watu mpaka wao wabadilishe hali zao Je anakusudia nini hapa?

Anakusudia kwamba ikiwa wewe utaamua kufuata njia ilinyooka basi atakufanyia wepesi kuiendea njia hiyo, utajikuta ibada kwako inakuwa nyepesi unajikuta unapenda mambo ya kheri.

Na ama utajitenga na njia yake iliyonyooka basi utapotea na atakuacha upotee,, tunaambiwa Lahaula wala quata ila bilah kwa maana hapana nguvu wala uwezo wa kufanya mema na kuacha mabaya isipokuwa kwa kuwezeshwa na Allah subhaanahu wa taala.

Ndugu zangu mwanadamu hana uwezo wa kuacha madhambi au mabaya isipokuwa kwa msaada wa Allah na vile vile hana uwezo wa kufanya mema isipokuwa kwa msaada wa Allah.

Kwahiyo tunamhitaji sana Allah ili tupate mwisho mwema, maisha ni mafupi mno kaburi linatungoja mda wowote ule.

Katika suratul takathur Allah anasema Hakika mwanadamu ameshughulishwa na wingi wa kutafuta mali mpaka analetwa kaburini hajafanya jambo lolote la kheri. Ndugu zangu uislamu haujakataza mtu kutafuta dunia yake akaishi maisha mazuri lakini hii isije ikamfanya akamsahau Mola wake kwa kufanya mambo yatakayo kuja kumfaa mara baada ya kufa kwake,,, kwani hakika akisahau hilo basi Allah anasema hakika atakuja kuuona moto kwa jicho la yakini kwa maana kwa upeo ulio wazi kabisa, na hapo mwanadamu atakuwa ashaangamia kwani hatakuwa na la kufanya kwasababu kama umri wa kuishi duniani alipewa lakini hakuufanyia yenye kumfaa huko akhera.

Kisha Allah anasema katika sura hiyo hiyo kisha tutawauliza juu ya neema tuliyowapa,,Hakika tumepewa neema ya uhai je tumeutumiaje uhai wetu? Tumepewa neema ya umri ni vipi tumeutumia umri wetu? Neema ya akili ni vipi tumetumia neema hiii ?
Neema ya mali ni vipi tumetumia neema hii? Na listi inaendelea......

Ndugu zangu ipo siku moja tutaitwa marehemu fulani bin fulani je tumetanguliza amali gani za kheri ili tutaporejea kwa Allah tuwe na cha kujiokoa na adhabu zake?

Tuamche Allah ukweli wa kumcha.
 
Je kwanini siku ya kiama makafiri watatamani wageuke kuwa mchanga

Tuiangalia hii aya katika suratul AN NABA

78:40 - Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!

siku ya kiama tutaonyeshwa yale matendo yetu tuliyo yatanguliza na yale tuliyo yaacha baada ya kufa kwetu, na mara baada ya kuonyeshwa hapo mwanadamu atajua hakika yeye yupo upande gani, ima wa kheri au wa shari.

Sasa Allah anasema Hakika hatujapuuzia chochote katika kitabu, kinyama chochote hai katika ardhi au ndege warukao kwa mbawa mbiwi hao ni umma kama nyinyi nao watakusanywa siku ya kiama

Kwahiyo hao viombe nao Allah atapitisha hukumu yake katika namna ambayo hatadhulumiwa hata mmoja, hata kondoo asiye na pembe atapewa nafasi ya kupata haki yake kwa kondoo mwenye pembe,,,kwa maana kuna wanyama wenye pembe huwaonea wasio na pembe basi siku hiyo haki itapatikana.

Baada ya Allah kupitisha hukumu yake na kila kiumbe kupata haki yake hapo Allan atasema kwa wale viumbe Kuweni mchanga na watakuwa mchanga

Sasa makafiri watashuhudia tukio hilo,, kwakuwa wanajua walimpinga Allah hapa duniani pamoja na mafundisho aliyokuja nayo Mtume Muhammad swalla llahu alayhi wasallam hakika watajua kuangamia kwao kumefika basi hapo watatamani wangekuwa mchanga kama wanyama wale na kufutikia mbali kabisa,,,, lakini hizo ni ndoto za alinacha hakika Moto ndio yatakuwa makazi yao

Ila muislamu asijione yeye yupo salama, huwezi ukawa mtenda dhambi mpaka kifo kinakufikia ukajiona utakuwa salama laa!

Tumche Allah azza wa jalla
 
Oya nyie magaidi, Ramadhani ni lini mana kuna demu wa kigaidi nataka kumla so ameniambia mpaka Ramadan ipite.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…