IJUE SWAUM YAKO 3⃣6⃣
📚 سؤال وجواب في أحكام الصيام.
📜HAWAJAWAHI KULIPA NA AMESAHAU SIKU ALIZOACHA KUFUNGA KUTOKANA NA MZUNGUKO WAKE WA HEDHI, JE AFANYE NINI.?
Swali:
Tangu nimewajibika kufunga Ramadhani ninafunga, lakini sijawahi kulipa masiku ambayo nimeacha kufunga kwa sababu ya mzunguko wangu wa mwezi (hedhi), na wala sijui (mpaka sasa) idadi ya siku ambazo nilifungua, tafadhali nielekeze nifanye nini hivi sasa?
Jawabu:
Kwanza ni wajibu kwa mwanamke huyu atubu kwa Allaah na aombe msamaha kwa yale aliyoyafanya, na afuatilie siku ambazo ameacha kufunga kadri awezavyo kisha azilipe, na kufanya hivi itakuwa jukumu lake limeondoka, na tunatumai kwamba Allaah atakubali toba yake (atamsamehe)
✍️ فضيلة الشيخ محمد العثيمين رحمه الله
Tarjama; Ustadh Abu Halima Arafat حفظه الله تعالى ورعاه
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
🌱 جزى الله خيرًا من قرأها وعمل بها وساعدنا على نشرها..
فَالدَّالُّ عَلَى الْخَيْرِ كَفَاعِلِه