Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Mashaallah, mwezi wa Qur'an namshukuru Allah kwa kufikisha juzuu nyinginyingi tu katika kuienzi Qur'an tukufu,

Nawausia na nye ndugu zangu tusisahau kuisoma Qur'an walau hata sura moja kwa siku.


Ramadhani Mubarak
 
منهج الأنبياء:

[emoji257]DUA YA QUNUUT[emoji257]

Qunuut kwa maelezo ya Fuqahaa (wanachuoni wa fiqh), ni du'aa inayosomwa katika Swalah katika sehemu maalum wakati mtu anapokuwa amesimama baada ya kurukuu (au kabla kwenye kauli nyingine). Na inatumika katika Swalah ya witr kwenye raka'ah ya mwisho baada ya kurukuu kwa kauli yenye nguvu.

Qunuut ni du'aa itumikayo wakati wa matatizo, majanga na maafa yanapowafika Waislam. Na wakati huo ndipo du'aa hii huombwa na huwa inaombwa katika kila Swalah na si Swalah ya alfajiri tu kamailivyozoeleka na baadhi ya watu kwa kutumia baadhi ya hadiyth ambazo hazijasihi kuhusiana na Qunuut ya kudumu (katika Swalah ya Alfajir). Du'aa hii si fardhi bali ni Mustahab, na Swalah ya mtu ni sahihi kabisa hata kama hajasoma Qunuut, na wala usiposoma Qunuut huhitaji kufanya sijdatus-sahw (sijida za kusahau) kama wanavyodhani wengine. Inapendezwa kufanywa wakati ikifikia dharura kamatulivyotaja juu. Na vilevile wakati mwingine wa kuisoma Qunuut ni wakati wa Swalah ya Witr.

Ni kinyume na Sunnah kuisoma Qunuut kwenye Swalah za asubuhi na kudumu nayo kama inavyofanywa kwani hilo halijathibiti katika hadiyth sahihi kutoka kwa Mtume (Swallah Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma du'aa hiyo wakati Maswahaba zake sabini wajuzi wa Qur-aan walipouliwa kwenye sehemu iitwayo Bi-ir Ma'uunah na Makabila ya Bani Sulaym ya Ri'il, Dhakwaan, Ussayah wakati alipowatuma kwenda kuwafundisha diniyao. Aliisoma du'aa ya Qunuut kwa muda wa mwezi mzima dhidi ya hao Wauaji. (Hadiyth ya Anas iliyopo kwenye Al Bukhaariy na Muslim).

Pia kwenye Hadiyth nyingine iliyopokelewa na Abu Hurayrah, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kuwaombea baadhi ya Maswahaba waliokuwa wamepotea kwa maadui, na aliomba kiasi cha mwezi kisha akaacha, na Abu Hurayrah alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwanini ameacha kuwaombea, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu,''Je,huoni kuwa washarejea?" (Al Bukhaariy na Muslim)

Hivyo, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Qunuut hiyo ambayo inaitwa Qunuut an Nawaazil kwa muda ambao yale aliyokuwa akiyaomba, yamejibiwa ndipo akaacha.

Vilevile imethibiti kuwa alikuwa akiwaombea wale waliokuwa dhaifu, wananyanyaswa na maadui na kuwa chini ya wavamizi kama hali tuliyonayo leo huko Iraq, Afghanistan, Palestina, Chechnya na kwengineko.

Imepokewa pia kuwa Abu Maalik Al-Ash'ariy alisema: "Nilimuuliza baba yangu, 'Ee baba yangu, uliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nyuma ya Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhum ajma'iyn). Je, walikuwa wakisoma Qunuut katika Swalah ya alfajiri?' Akajibu, Ee mwanangu, hili ni jambo jipya lililozushwa,'" (Imesimuliwa na wapokezi wote (watano) isipokuwa Abu Daawuud). Hakika muongozo mzuri na bora ni ule wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Na Qunuut inaposomwa, basi ni vizuri kusoma kwa ile shida inayoombewa kwa wakati huo; kama ni njaa au udhaifu au manyanyaso n.k., iombwe kutokana na masuala hayo, na si kusoma du'aa ile iliyozoeleka kwenye Qunuut 'Allahumma ihdiyna fiyman hadayta, wa'afina fiyman 'afayta...' Du'aa hii inawezwa kusomwa kwenye Qunuut ya witr na si kwenye Qunuut ya Nawaazil.

Na endapo utaswali nyuma ya Imaam anayesoma Qunuut katika Swalah ya Alfajiri, basi unatakiwa umfuate na Swalah yako ni sahihi, kwani kumfuata Imam ni wajibu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

"Imaam amechaguliwa ili afuatwe" na akasema: "Msitofautiane na Maimaam wenu",

na pia katika Swahiyh Al-Bukhaariy amesema:

"Wanawaongoza katika Swalah; ikiwa wamepatia, (ujira) ni wenu na wao, na wakikosea, (ujira) ni wenu na (dhambi) ni zao."

Wa Allaahu A'alam

☘[emoji257]☘☘[emoji257]☘[emoji257]☘☘[emoji257]
Nakusoma mkuu
Pia tuletee na maneno yake itakuwa poa zaidi
 
✳✅ Nikweli nabii Suleiman alikuwa na wanawake 1000..❤ 700 wake wa ndoa na 300 masuria. ..wanawake masuria (women slaves ).. ni wanawake wanaopatikana kwa vita vya jihad (holy war vita vitakatifu ).... *( kama nyara.....⏩.tazama quran.sura 70 :30. .women slaves...wanawake hawa masuria hufungi nao ndoa ...wao ni nyara na hamna idadi ya mwisho kuwamiliki na wanasilimu yaani wanakuwa waumini.....wakikataa kusilimu .yaani kuamini wanakuwa watumwa.na itabidi walipe kodi kwa nchi ya kiislam. Au nchi yawaumini . ( taifa lililokombolewa.kwa vita vitakatifu). .... Hata maswahaba walikuwa nao wanawake hawa. .ila maswahaba waliwaaacha huru .... ....mitume na manabii wa m/mwenyezi wanakuwa wana sifa nyingi tofaut na sisi. ..mfano .wanakuwa na nguvu sana.akikushika na mkono wake huwezi kujichomoa. ...wana nguvu za kiume zisizopungua wanauwezo wa kufanya kitendo cha ndoa 24 hrs continously bila kupumzika * non stop ).... Hata kidogo....wakitembea ugenini hawapotei njia. ..✳ wakipigana vita na yoyote hushinda ..mfano nabii daudi kumuua jitu kubwa sana * hefty and a giant goliath * David and goliath.... mitume wanaweza kaa bila kula kwa masiku mengi. .mfano nabii issa mathayo 4 :2 akafunga siku 40 mchana na usiku ..N .B ▶ manabii hawalali usingizi ...wanapumzisha mwili ( repose the body)...hawalali maanake huwa wanaongea na mola usingizin kwa kuoteshwa ..♎ mitume na manabii wanaweza tembea mwendo mrefu bila kuchoka. ....♦sauti yao hufika mbali kuliko yoyote ....wao huona mbali ( keen sight) kuliko yoyote ↘ mioyo yao huwa haina chuki kinyongo. .siwachoyo. .siwabahili. ..hawafanyi uovu au kuasi amri ya Allah. ...✡ hawali mpaka wasikie njaa na wakila☕ hawali wakashiba......hawapigi miayo. ....hawacheki wao hutabasamu tu. .......miili yao hunukia perfume. .♐...mitume na manabii shetani hawezi kuwapoteza wala kuwapandikiza fikra potofu. Tazama mathayo 4 5. .na quran 72 :27 na 28. ......N.B hakuna nabii wala mtume wa m/mungu alieoa mke mmoja ..aliyeoa wake wachache ni nabii Ibrahim alioa 3. .na nabii Ayub 3...na mitume Muhammad s.a.w.alioa wanawake 11. ......haya waigeni manabii oeni mitaala acheni ku-divert.(michepuko).
Daaruul ilmu Naafia...Marangu. kilimanjaro
Ni kweli mkuu
Mitume walikuwa si watu wa kawaida ni mojawapo ya alama kubwa za kuwepo M/Mungu (sw), kutokana na elimu na karama walizokuwa nazo, Inastaajabisha mno!

Niliwahi kusoma hadithi, maswahaba waliwahi kumuuilza Mtume (s.a.w) "Hivi ni mtu gani ambae amependelewa zaidi na M/Mungu (s.w) katika hii dunia"
Akawaambia "Mtume,mtoto wa Mtume,mtoto wa Mtume,mtoto wa Rafiki wa M/Mungu"

Mtume(s.a.w) alikuwa anamzungumzia Yusuph (a.s) kwani Baba yake (Yakub a.s) ni Mtume, Babu yake Isihaka (a.s) ni Mtume,Babu mzaa Babu yake (Ibrahim a.s) ni Mtume

Nahis ndiyo maana wale wanawake wa kimisri baada ya kumuona yusuph wakajikuta tu, wanatamka "Hasha Lillah hakika si mtu huyu,huyu ni malaika,tena malaika mtukufu mno"

Kwa hiyo Mtume (s.a.w) alikuwa anamaanisha Mtume Yusuph (a.s) uzuri ni neema ndogo tu aliyopewa, kulinganisha na ile chain ya Mitume iliyopo katika uzao wake, MashaAllah!

Ramadhan Kareem
 
بسم الله الرحمن الرحيم

MADA YAPILI

MAMBO YENYE KUBATILISHA FUNGA

Mambo yenye kubatilisha funga tumeyagawa katika makundi mawili

1. Mambo ambayo Wanazuoni wamewafikiana

2. Mambo ambayo wanazuoni wamekhitilafiana

I. Mambo ambayo wamewafikiana kwamba yanabatilisha funga ni:

1. Kula kwa makusudi

2. Kunywa kwa makusudi

3. Kujitapisha

4. Kujitowa manii

5. Kufanya tendo la unyumba mchana wa Ramadhani

6. Kuingia kitu ndani kupitia tundu zilizo wazi

7. Kupatwa na Hedhi

8. Kupatwa na Nifasi

9. Kupiga sindano ya kuongeza nguvu au ya chakula

II. Mambo ambayo Wanazuoni wamekhitilafiana

1. Dawa ya kutia puani

2. Dawa ya kutia sikioni

3. Dawa ya kutia jichoni

Baadhi ya wanazuoni wameyataja mambo yafuatayo kwamba hayafunguzi

1. Kujipulizia inhela

2. Kuweka kidonge cha presha chini ya ulimi na kutomeza kitu chochote kinapowekwa

3. Kuwekewa gesi ya oksijini

4. Kuonja chakula bila ya kumeza mate

بسم الله الرحمن الرحيم

MADA YAPILI

MAMBO YENYE KUBATILISHA FUNGA

Mambo yenye kubatilisha funga tumeyagawa katika makundi mawili

1. Mambo ambayo Wanazuoni wamewafikiana

2. Mambo ambayo wanazuoni wamekhitilafiana

I. Mambo ambayo wamewafikiana kwamba yanabatilisha funga ni:

1. Kula kwa makusudi

2. Kunywa kwa makusudi

3. Kujitapisha

4. Kujitowa manii

5. Kufanya tendo la unyumba mchana wa Ramadhani

6. Kuingia kitu ndani kupitia tundu zilizo wazi

7. Kupatwa na Hedhi

8. Kupatwa na Nifasi

9. Kupiga sindano ya kuongeza nguvu au ya chakula

II. Mambo ambayo Wanazuoni wamekhitilafiana

1. Dawa ya kutia puani

2. Dawa ya kutia sikioni

3. Dawa ya kutia jichoni

Baadhi ya wanazuoni wameyataja mambo yafuatayo kwamba hayafunguzi

1. Kujipulizia inhela

2. Kuweka kidonge cha presha chini ya ulimi na kutomeza kitu chochote kinapowekwa

3. Kuwekewa gesi ya oksijini

4. Kuonja chakula bila ya kumeza mate
 
بسم الله الرحمن الرحيم

MADA YA TATU

NINI KINAMPASA MWENYE KUFANYA JAMBO LIKABATILISHA FUNGA YAKE

Katika mada ya pili tuligusia baadhi ya mambo ambayo mfungaji akiyafanya funga yake itabatilika. Ni nini itampasikia mtu mwenye kufanya jambo likabatilisha saumu yake?

Mtu atakapofanya jambo katika mambo yenye kubatilisha saumu pasina kukusidia kama vile kulala akatokwa na manii, au atakayefanya jambo kwa kusahau kama amefunga akala au akanywa, au kazidiwa na matapishi akatapika, funga yake mtu huyo haitobatilika bali ataendelea na funga yake kwa ushahidi wa maneno ya Mtume Muhammad SAWW.

1. Mwenye kula au kunywa hali ya kuwa amesahau kama amefunga na atimize funga yake, kwani huyo amelishwa na amenyweshwa na Allah.

2. Mwenye kuzidiwa na matapishi hana kulipa na mwenye kujitapisha itamlazimikia kulipa.



Ama mwenye kufanya jambo kwa kudhania na ikamdhihirikia kinyume chake huyo funga yake itabatilia. Mfano mwenye kula daku akidhani kwamba bado alfajiri haijaingia ikamdhihirikia kwamba alfajiri imeshaingia, huyu funga yake haitosihi na itamlazimikia ajizuwie kutwa nzima na siku hiyo aje kuilipa. Kama yule aliyedhani kwamba jua lishazama akafutari ikamdhihirikia kwamba jua kumbe bado halijazama atajizuwia na kula na funga yake ya siku hiyo itabatilika na itamlazimu kuja kuilipa siku hiyo.

Ama atakayezimia baada ya kutia nia na hakuja juu mpaka baada ya magharibi funga yake ya siku hiyo haitosihi na itamlazimikia kuja kuilipa, ama akija juu kabla ya kuzama jua funga yake haitobatilika.

Ama atakayepatwa na hedhi au nifasi katika sehemu ya mchana funga yake itabatilika hata kama itakuwa bado dakika 5 kuzama jua, na siku hiyo atakuja kuilipa.

Ama atakayeamka na janaba na hakuwahi kuliondosha mpaka ikaingia alfajiri hali ya kuwa amelala na nia, funga yake itakuwa sahihi kwa ushahidi wa kitendo cha Mtume SAWW imepokewa kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume wamesema ya kwamba “Mtume SAWW alikuwa akiamka asubuhi hali ya kuwa na janaba alilolipata kwa kukutana na ahli yake na sio kwa kuota huku akiwa na funga.

Ama atakayekutana na mkewe katika mchana wa Ramadhani pasina kuwa na ruhusa ya kisheria funga zao zitabatilika na itawalazimu kuja kuilipa funga ya siku hiyo na Mume itamuwajibikia kutoa kafara nzito ambayo ni:

1. Kuwacha huru Mtumwa au

2. Kufunga miezi miwili mfululizo au

3. Kulisha masikini sitini

Ama mwenye kufanya jambo la kubatilisha funga kwa makusudi pasina rukhsa ya kisheria huyu atakuwa amechuma dhambi kubwa mno na amefanya kosa kubwa sana kwa kuidharau nguzo katika nguzo za Uislamu, na itamuwajibikia:

1. Kutubu toba ya kweli

2. Kuilipa funga hiyo

3. Kutoa kafara kama ikiwa zimepita Ramadhani ya kibaba kimoja kwa kila siku na kwa idadi ya Ramadhani zilizopita bila ya kulipa.

4. Na baadhi ya Wanazuoni wamesema atatoa na kafara kubwa pia.

TANBIHI

Ikiwa mtu alifungua pasina sababu ujanani kwake funga hiyo bado ipo katika dhima yake na ni wajibu kuilipa na kutowa kafara.

Na mwenye kuilipa funga aliyoiharibu pasina ruhusa ya kisheria dhima itamuondoka lakini kisheria bado atakuwa hakuipa funga hiyo au hizo haki yake. Mtume SAWW amesema “Mwenye kufungua siku moja tu katika Ramadhani pasina rukhsa ya kisheria hatoweza kuilipa hata kama atafunga mwaka.
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 4 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*BAADA YA KUFAHAMAU NINI IMANI NA WAPI MAHALA PAKE, LEO KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU TUFAHAMU PIA NINI TAQWA NA WAPI MAHALA PAKE.*

*♡ فما هي التقوى؟*
*TAQWA NI NINI?*

*♡ "التقوى: هي الخوف من الجليل، والعمل بالتنزيل، والرضا بالقليل، والاستعداد ليوم الرحيل"*

*TAQWA NI - KUMUKHOFU ALLAH, NAKUTENDA KWA MUJIBU WA QUR'ANI, NAKURIDHIA KIDOGO CHA HALALI, PIA KUJIANDAA NA SAFARI (MAUTI)*

*HII NDIO MAANA YA TAQWA KWA UFUPI SANA.*

*♡ محل التقوى- القلب.*
*MAHALA PA TAQWA NI MOYONI.*

*♡ الإيمان تصديق بالقلب، والتقوى محلُّها القلب.*
*■ KUMBUKA: IMANI NI KUSADIKI KWA MOYO (MAHALA PAKE NI MOYONI) TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI.*

*♡ أشار النبي - صلَّى الله عليه وسلَّم - إلى صدره وقال: ((التقوى هاهنها))*

*ALIASHIRIA MTUME (ﷺ) KIFUANI NA AKASEMA: TAQWA IPO HAPA (NDANI YA KIFUA YANI MOYONI)*

*SASA TAZAMA HAPA.*

*♡ الإيمان محلُّه القلب، والتقوى محلها القلب والإيمان في القلب، وكذلك الصيام سر بينك وبين ربِّك لا يعلمه إلاَّ هو.*
*■ IMANI MAHALA PAKE NI MOYONI, TAQWA PIA MAHALA PAKE NI MOYONI, KADHALIKA FUNGA NI SIRI BAINA YAKO NA MOLA WAKO MLEZI, HAKUNA ANAE IJUA FUNGA YAKO ILA ALLAH PEKEE.*

*♡ إذا تستطيع أن تأكل وتشرب بعيد عن عيون الناس وتدعى أنك صائم.*
*HIVO BASI, WAWEZA KULA NA UKANYWA MBALI NA MACHO YA WATU, KISHA UKADAI UMEFUNGA.*

*● LAKINI KWA SABABU FUNGA NI IBADA YA SIRI, BILA SHAKA SIRI HIYO AIJUA ALLAH MTUKUFU NA YEYE KWAKE HAKIFICHIKI KITU.*

*♡ فإذا كان الإيمان أمرًا سريًّا، وكانت التقوى أمرًا سريًّا، وكان الصيام أمرًا سريًّا.*
*SASA BASI, IKIWA IMANI NI JAMBO LA SIRI. NA PIA TAQWA IKAWA NI JAMBO LA SIRI. NA HATA FUNGA NAYO IKAWA NI JAMBO LA SIRI.*

*♡ فناسب ذلك أن يأتي الصيام بين الإيمان والتقوى.*
*NDIO IKAWA SABABU YA MNASABA KWA HILO KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA.*

*♡ لأنَّ الثلاثة أمورٌ سرّيَّة لا يطَّلع عليها إلا علام الغيوب.*
*KWA SABABU HAYA MAMBO MATATU NI MAMBO YASIRI AMBAYO HAKUNA WA KUYAONA ILA MJUZI WA YALIYO JIFICHA (ALLAH MTUKUFU)*


*♡ ولذلك اسمع إلى قول مولانا في الحديث القدسي يؤكد سرّيَّة الصيام، فيقول:*
*KWA AJILI HIYO, SIKILIZA KAULI YA ALLAH MTUKUFU KATIKA HADITHIL QUDSIY ATILIA NGUVU SIRI YA IBADA YA FUNGA KWA KUSEMA*

*"ﻛُﻞُّ ﻋَﻤَﻞِ ﺍﺑْﻦِ ﺁﺩَﻡَ ﻳُﻀَﺎﻋَﻒُ ﺍﻟْﺤَﺴَﻨَﺔُ ﻋَﺸْﺮُ ﺃَﻣْﺜَﺎﻟِﻬَﺎ ﺇِﻟَﻰ ﺳَﺒْﻌﻤِﺎﺋَﺔ ﺿِﻌْﻒٍ ﻗَﺎﻝَ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﺰَّ ﻭَﺟَﻞَّ ﺇِﻟَّﺎ ﺍﻟﺼَّﻮْﻡَ ﻓَﺈِﻧَّﻪُ ﻟِﻲ ﻭَﺃَﻧَﺎ ﺃَﺟْﺰِﻱ ﺑِﻪِ ﻳَﺪَﻉُ ﺷَﻬْﻮَﺗَﻪُ ﻭَﻃَﻌَﺎﻣَﻪُ ﻣِﻦْ ﺃَﺟْﻠِﻲ ﻟِﻠﺼَّﺎﺋِﻢِ ﻓَﺮْﺣَﺘَﺎﻥِ ﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻓِﻄْﺮِﻩِ ﻭَﻓَﺮْﺣَﺔٌ ﻋِﻨْﺪَ ﻟِﻘَﺎﺀِ ﺭَﺑِّﻪِ ﻭَﻟَﺨُﻠُﻮﻑُ ﻓِﻴﻪِ ﺃَﻃْﻴَﺐُ ﻋِﻨْﺪَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻣِﻦْ ﺭِﻳﺢِ ﺍﻟْﻤِﺴْﻚِ"* متفق عليه.
*MAANA YAKE:*

*"Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba. Na Allah ﷻ Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk"*

*■ HII NDIO HEKIMA YA KUJA IBADA YA FUNGA BAINA YA IMANI NA TAQWA, KWA SABABU HIVYO VITU VITATU VYOOTE NI VITU VYA SIRI NA NDIO MAANA VIMEAMBATANA.*
*♢♢ والله أعلم*
☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*

*Mrisho Maulid Othman*
_*[emoji336]+255655559911*_

*Ukumbi Wa Faidika Na Mawaidha.*

*الدعوة اﻹسلامية*
 
Asalam alaykm warhamatullah wabarakat.
IMG-20170531-WA0003.jpg
IMG-20170530-WA0017.jpg
 
Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote nawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.
Jazakah allah Kheyr
 
jamani mi mwislm swafi lakini siezi funga Ramadan watu wanizungukao wajua nafunga mana huko nje naonekana mumini mzuri ila ndo siezi funga.ibada zote nafanya nala daku nala iftar ila kufunga siezi nimejaribu mara kibao nimeshindwa. nikifunga nakosa nguvu nakua sioni hata kazi hazifanyiki nakua nalala mda wote. jaman nifanye nini nifunge kama wengine au nile nini usiku ili mchana niwe wakawaida?
Kwanza pandisha imani yako, jitahd kufanya dhikr, kusoma Qur'an na fikiria ile cku utakaporudi kwa Mola wako.
Chelewa kula Daku at least uwe unakula saa 04:30a.m pia jitahd kunywa maji mengi ucku.
 
[emoji253]DAARUL MUSTAFA[emoji253]
[emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267][emoji267]
TAFADHALI SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA KWAKO

*IBADA MUHIMU ZA KUZIDISHA KTK MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN*

*BISMILLAHI RAHMAN RAHYM*

A.ALYKUM.
ALHAMDULILLAAH
WA S.A.W.

Ndg zng tumshukuru Sana ALLAH S.W. kwa kutufikisha salama ktk Ramadhan.

Hakika ktk mafundisho ya Uislaam tumesisitizwa sana kuzidisha ibada MBALIMBALI ili kupata rehma na barka zilizopo ktk RAMADHAN.

miongoni mwa ibada hizo ni kufanya sana DHIKRI na kuomba dua kwa wingi.

Hakika MWEZI MTUKUFU wa RAMADHAN umegawanyika ktk makumi matatu..

Kumi la kwanza ni kumi la *REHMA*

KUMI LA pili ni kumi la *MSAMAHA*

kumi la tatu ni kumi la kuokolewa ktk moto wa *JAHANNAM*

*NYIRADI ZA KUZIDISHA KTK KUMI LA KWANZA*

Kwa kua kumi la mwanzo ni kumi la*REHEMA* basi Imependekezwa sana ktk kumi hilo kujitahidi sana kusoma uradi
*(YAA ARHAMAR RAHIMINA)*

*IDADI YA URADI*
Idadi ya uradi huo ni Mara 1000 kila siku.

*NIYA YA URADI*
Utatia Niya ya uradi huo kabla ya kuanza kufanya uradi huo... utasema hv BISMILLAHI RAHMANI RAHIM . ALLAHUMMA SWALLI WA SALLIM WA BAARIK ALAA SAYYIDNAA MUHAMMAD WA ALAA AALIHI WA SALLIM.

*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNIJAZE REHEMA ZILIOZOPO KTK KUMI HILI LA MWANZO KTK RAMADHAN. NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

Baada ya hapo utaanza kusoma uradi mpaka utakapo maliza idadi kamili..

Ukimaliza uradi utanyanyua mikono yako kisha utaomba duaa ya shida zako mbalimbali
Usiwache kumsalia mtume S.a.w. kila baada ya maombi yako ni muhimu sana.

Ukimaliza kumi la mwanzo utakua umefanya uradi huo mara 10,000.

*MUDA WA KUSOMA URADI HUO*
Inaruhusiwa kusoma uradi ktk muda wowote utakaopanga mwenyewe lkn muda utakaochagua utautumia muda huo huo mpaka masiku 10 yaishe..

Lkn muda mzuri wa kuvuta uradi huo ni lisaa limoja kabla ya kutoka adhana ya maghribi.. Kwani muda huo ni muda mzuri unaokubaliwa duaa nyingi ktk RAMADHAN.

UKIJITAHIDI kufata utaratibu huu mpaka ukamaliza kumi LA mwanzo basi Insha ALLAH UTAPATA REHEMA Zilizomo ktk kumi hilo la mwanzo..

*NYIRADI YA KUSOMA KTK KUMI LA PILI KTK RAMADHAN*

kumi la pili ni kumi la KUSAMEHEWA MADHAMBI YOTE YALIOPITA.

Ktk kumi la pili utasoma *ASTAGHFIRULLAAH LA'ADHIM WA ATUUBU ILAIHI* mara 1000 kila siku.

Utatumia Utaratibu kama ulivotumia utaratibu wa mwanzo isipokua ktk NIYA.

*NIYA YAKE NI KAMA IFATAVYO*......
*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNISAMEHE MADHAMBI YANGU YOTE NILIOFANYA KWA MAKUSUDI AU KWA BAHATI MBAYA NAOMBA UNIPE RADHI ZAKO NA MSAMAHA WAKO ULIOPO KTK KUMI HILI LA PILI KTK RAMADHAN. NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

kisha utavuta uradi huo na utamalizia kwa kuomba duaa zako MBALIMBALI.

Ukimaliza uradi huo ktk kumi la pili utakua umeomba msamaha kwa ALLAH mara elfu kumi.

Inshaa Allah ALLAH atatukubalia TOBA ZETU kwa baraka za kumi la pili KTK RAMADHAN.

*URADI KTK KUMI LA TATU*

Kumi la tatu ni kumi la Kuepushwa na moto wa JAHANNAM.

utafata taratibu zilzotangulia kisha utatia niya hii.[emoji116]

*EWE ALLAH ULIE TUKUKA HAKIKA NIMETIA NIA YA KUSOMA URADI HUU ILI NIPATE RADHI ZAKO NA UNIUPUSHE NA ADHABU ZA DUNIANI NA ADHABU ZA JAHANNAMU NAKUOMBA UNIKUBALIE IBADA YANGU HII KWAKO.*

Kisha utasoma URADI HUU[emoji116]
*ALLAHUMMA AJIRNAA MINA NNAARI SAALIMINA* mara 1000 kila siku.
Kisha utaomba duaa zako za matatizo MBALIMBALI.

Ukimaliza uradi huo ktk kumi la mwisho utakua umeomba uepushiwe shida za duniani na adhabu za AKHERA mara elfu kumi.

Jumla ya uradi zote utakua umesoma uradi mara elfu THAELATHINI ktk RAMADHAN yote.

*MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KTK NYIRADI HIZO NI*[emoji116]

1. Hakikisha unao UDHUU KTK URADI.

2.HAKIKISHA unaelekea KIBLA ktk uradi.

3.usikatishe uradi kwa ajili ya mazungumzo isipokua kwa dharura.

4.chagua sehemu moja maalum ya kufanya nyiradi zako zote mpaka RAMADHAN itakapoisha. Labda itokee dharura kama KAZI,SAFARI,N.K.

5.HAKIKISHA UNAMSALIA MTUME S.A.W KILA UNAPOMALIZA NYIRADI NA DUAA ZAKO

*MWISHO*

Musinisahau kuniombea msamaha ktk duaa zenu.
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 5 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}*
*Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.* (2:183)
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*■ LEO TENA KATIKA DARSA YETU SEHEMU YA TANO, IN SHA ALLAH TUTAANGALIA AU KUITAFUTA HEKMA YA KUJA AYA YA DUAA BAADA YA AYA ZA FUNGA.*

*♡ لماذا وضع الله آية الدعاء بين آيات الصيام؟*
*KWA NINI ALLAH MTUKUFU AMEWEKA AYA YA DUAA BAINA YA AYA ZA FUNGA?*

*♡ لم وضعت الآية: ﴿ وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴾*
*KWA NINI IMEWEKWA AYA HII?*
```Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.``` [البقرة: 186]، الآية

*♡ والتي قبلها: ﴿ شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ ﴾ الآية.*
*NA AMBAYO IPO KABLA YAKE:*
```Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.```

*♡ والآية التي بعدها: ﴿ أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَى نِسَائِكُمْ ﴾*
*NA AMBAYO IPO BAADA YAKE:*
```Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu.```

*♡ فلماذا جاءت بين الآيتين آية الدعاء؟*
*BASI KWANINI NA IPI HEKMA YA KUJA BAINA YA AYA MBILI IKAJA AYA YA DUAA?*

*IN SHA ALLAH TUTAENDELEA NAYO KATIKA DARSA YA SITA.*
☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*


*الدعوة اﻹسلامية*
 
Aliulizwa mmoja wa watu wema kwanini unakwenda msikitini kabla ya adhana? akasema: Adhana ni kwa ajili ya walioghafilika, na naomba nisiwe mmoja wao!!
(Tunamuomba Mola salama)
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Nilimuuliza kwa nini unapenda daima kunywa maji msikitini, hali unayo nyumbani kwako?
Akasema: ili alipwe yule aliyeyaweka msikitini
"nafsi za daraja ya juu"
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Ukiambiwa aibu ya mtu ifanye isimame kwako; ikisimama kwako utapata thawabu za kusitiri, na anayemsitiri Muislamu husitiriwa na Mwenyezi Mungu
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Dua tatu musizisahau katika sijida zenu:
-Ewe Mola hakika mimi nakuomba unipe mwisho mwema
-Ewe Mola niruzuku toba ya kweli(nasuha) kabla ya mauti
-Ewe Mola ewe unaepindua nyoyo uthibitishe moyo wangu kwenye dini yako
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Nuia kusambaza maneno haya na tia nia ya kheri ili Mwenyezi Mungu akuondolee matatizo ya dunia
Kumbuka: fanya kheri hata kama ni ndogo

[emoji840]TUAMRISHANE[emoji840]
[emoji840]MEMA[emoji840]
 
SWALI:



Assalam alaykum warahmatullah wabarakatu



Huku ninakoishi kuna baridi sana, sasa majumbani kwetu kuna viatu ambavyo hutumika kutembelea ndani ya nyumba tu kwa sababu ya baridi, yaani ni twahara sasa ninaweza kuvitumia kuswalia.







JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuswali na viatu vinavyovaliwa ndani ya nyumba.





Hakika ni kuwa hata kama viatu hivyo vingekuwa vinavaliwa nje ya nyumba unafaa kuswalia maadamu ni twahara, havina najisi. Utwahara wa viatu ni kuwa vikavu.



Tufahamu kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa wanaswali na viatu ambavyo walikuwa wanatembelea navyo ndani ya Msikiti. Na kwa ajili hiyo Mughiyrah bin Shu‘bah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha na kupangusa juu ya champali na viatu vyake” (Ahmad na at-Tirmidhiy).

Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyopokewa na Abu Salamah Sa‘iyd bin Yaziyd aliyesema: “Nilimuuliza Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu): Je, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali na viatu vyake”. Akasema: “Ndio” (al-Bukhaariy na Muslim).



Kwa hiyo, waweza kuvaa hivyo viatu hata ikiwa hakuna baridi. Na hata ikiwa umetokwa na wudhuu baada ya kuwa umevivaa ukiwa nao, huna haja ya kuvivua bali waweza kupangusa juu yake wakati wa wudhuu kisha ukaswali navyo maadamu kabla ya kuvivaa ulikuwa ushatia nia ya kupangusa juu ya viatu endapo wudhuu utaondoka na kabla ya kuvivaa uwe umetia wudhuu kwa kuosha miguu kabla ya kuvaa viatu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom