Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakusoma mkuuمنهج الأنبياء:
[emoji257]DUA YA QUNUUT[emoji257]
Qunuut kwa maelezo ya Fuqahaa (wanachuoni wa fiqh), ni du'aa inayosomwa katika Swalah katika sehemu maalum wakati mtu anapokuwa amesimama baada ya kurukuu (au kabla kwenye kauli nyingine). Na inatumika katika Swalah ya witr kwenye raka'ah ya mwisho baada ya kurukuu kwa kauli yenye nguvu.
Qunuut ni du'aa itumikayo wakati wa matatizo, majanga na maafa yanapowafika Waislam. Na wakati huo ndipo du'aa hii huombwa na huwa inaombwa katika kila Swalah na si Swalah ya alfajiri tu kamailivyozoeleka na baadhi ya watu kwa kutumia baadhi ya hadiyth ambazo hazijasihi kuhusiana na Qunuut ya kudumu (katika Swalah ya Alfajir). Du'aa hii si fardhi bali ni Mustahab, na Swalah ya mtu ni sahihi kabisa hata kama hajasoma Qunuut, na wala usiposoma Qunuut huhitaji kufanya sijdatus-sahw (sijida za kusahau) kama wanavyodhani wengine. Inapendezwa kufanywa wakati ikifikia dharura kamatulivyotaja juu. Na vilevile wakati mwingine wa kuisoma Qunuut ni wakati wa Swalah ya Witr.
Ni kinyume na Sunnah kuisoma Qunuut kwenye Swalah za asubuhi na kudumu nayo kama inavyofanywa kwani hilo halijathibiti katika hadiyth sahihi kutoka kwa Mtume (Swallah Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam).
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma du'aa hiyo wakati Maswahaba zake sabini wajuzi wa Qur-aan walipouliwa kwenye sehemu iitwayo Bi-ir Ma'uunah na Makabila ya Bani Sulaym ya Ri'il, Dhakwaan, Ussayah wakati alipowatuma kwenda kuwafundisha diniyao. Aliisoma du'aa ya Qunuut kwa muda wa mwezi mzima dhidi ya hao Wauaji. (Hadiyth ya Anas iliyopo kwenye Al Bukhaariy na Muslim).
Pia kwenye Hadiyth nyingine iliyopokelewa na Abu Hurayrah, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kuwaombea baadhi ya Maswahaba waliokuwa wamepotea kwa maadui, na aliomba kiasi cha mwezi kisha akaacha, na Abu Hurayrah alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwanini ameacha kuwaombea, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu,''Je,huoni kuwa washarejea?" (Al Bukhaariy na Muslim)
Hivyo, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Qunuut hiyo ambayo inaitwa Qunuut an Nawaazil kwa muda ambao yale aliyokuwa akiyaomba, yamejibiwa ndipo akaacha.
Vilevile imethibiti kuwa alikuwa akiwaombea wale waliokuwa dhaifu, wananyanyaswa na maadui na kuwa chini ya wavamizi kama hali tuliyonayo leo huko Iraq, Afghanistan, Palestina, Chechnya na kwengineko.
Imepokewa pia kuwa Abu Maalik Al-Ash'ariy alisema: "Nilimuuliza baba yangu, 'Ee baba yangu, uliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nyuma ya Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhum ajma'iyn). Je, walikuwa wakisoma Qunuut katika Swalah ya alfajiri?' Akajibu, Ee mwanangu, hili ni jambo jipya lililozushwa,'" (Imesimuliwa na wapokezi wote (watano) isipokuwa Abu Daawuud). Hakika muongozo mzuri na bora ni ule wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Na Qunuut inaposomwa, basi ni vizuri kusoma kwa ile shida inayoombewa kwa wakati huo; kama ni njaa au udhaifu au manyanyaso n.k., iombwe kutokana na masuala hayo, na si kusoma du'aa ile iliyozoeleka kwenye Qunuut 'Allahumma ihdiyna fiyman hadayta, wa'afina fiyman 'afayta...' Du'aa hii inawezwa kusomwa kwenye Qunuut ya witr na si kwenye Qunuut ya Nawaazil.
Na endapo utaswali nyuma ya Imaam anayesoma Qunuut katika Swalah ya Alfajiri, basi unatakiwa umfuate na Swalah yako ni sahihi, kwani kumfuata Imam ni wajibu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:
"Imaam amechaguliwa ili afuatwe" na akasema: "Msitofautiane na Maimaam wenu",
na pia katika Swahiyh Al-Bukhaariy amesema:
"Wanawaongoza katika Swalah; ikiwa wamepatia, (ujira) ni wenu na wao, na wakikosea, (ujira) ni wenu na (dhambi) ni zao."
Wa Allaahu A'alam
☘[emoji257]☘☘[emoji257]☘[emoji257]☘☘[emoji257]
Ni kweli mkuu✳✅ Nikweli nabii Suleiman alikuwa na wanawake 1000..❤ 700 wake wa ndoa na 300 masuria. ..wanawake masuria (women slaves ).. ni wanawake wanaopatikana kwa vita vya jihad (holy war vita vitakatifu ).... *( kama nyara.....⏩.tazama quran.sura 70 :30. .women slaves...wanawake hawa masuria hufungi nao ndoa ...wao ni nyara na hamna idadi ya mwisho kuwamiliki na wanasilimu yaani wanakuwa waumini.....wakikataa kusilimu .yaani kuamini wanakuwa watumwa.na itabidi walipe kodi kwa nchi ya kiislam. Au nchi yawaumini . ( taifa lililokombolewa.kwa vita vitakatifu). .... Hata maswahaba walikuwa nao wanawake hawa. .ila maswahaba waliwaaacha huru .... ....mitume na manabii wa m/mwenyezi wanakuwa wana sifa nyingi tofaut na sisi. ..mfano .wanakuwa na nguvu sana.akikushika na mkono wake huwezi kujichomoa. ...wana nguvu za kiume zisizopungua wanauwezo wa kufanya kitendo cha ndoa 24 hrs continously bila kupumzika * non stop ).... Hata kidogo....wakitembea ugenini hawapotei njia. ..✳ wakipigana vita na yoyote hushinda ..mfano nabii daudi kumuua jitu kubwa sana * hefty and a giant goliath * David and goliath.... mitume wanaweza kaa bila kula kwa masiku mengi. .mfano nabii issa mathayo 4 :2 akafunga siku 40 mchana na usiku ..N .B ▶ manabii hawalali usingizi ...wanapumzisha mwili ( repose the body)...hawalali maanake huwa wanaongea na mola usingizin kwa kuoteshwa ..♎ mitume na manabii wanaweza tembea mwendo mrefu bila kuchoka. ....♦sauti yao hufika mbali kuliko yoyote ....wao huona mbali ( keen sight) kuliko yoyote ↘ mioyo yao huwa haina chuki kinyongo. .siwachoyo. .siwabahili. ..hawafanyi uovu au kuasi amri ya Allah. ...✡ hawali mpaka wasikie njaa na wakila☕ hawali wakashiba......hawapigi miayo. ....hawacheki wao hutabasamu tu. .......miili yao hunukia perfume. .♐...mitume na manabii shetani hawezi kuwapoteza wala kuwapandikiza fikra potofu. Tazama mathayo 4 5. .na quran 72 :27 na 28. ......N.B hakuna nabii wala mtume wa m/mungu alieoa mke mmoja ..aliyeoa wake wachache ni nabii Ibrahim alioa 3. .na nabii Ayub 3...na mitume Muhammad s.a.w.alioa wanawake 11. ......haya waigeni manabii oeni mitaala acheni ku-divert.(michepuko).
Daaruul ilmu Naafia...Marangu. kilimanjaro
Waalekum salaam, kaifa haleshAsalam Alykum warahma tullah wabarakatuh
Jazakah allah KheyrAsalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,
Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote nawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.
Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.
Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu
Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.
Kwa haya machache napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.
Karibuni.
Kwanza pandisha imani yako, jitahd kufanya dhikr, kusoma Qur'an na fikiria ile cku utakaporudi kwa Mola wako.jamani mi mwislm swafi lakini siezi funga Ramadan watu wanizungukao wajua nafunga mana huko nje naonekana mumini mzuri ila ndo siezi funga.ibada zote nafanya nala daku nala iftar ila kufunga siezi nimejaribu mara kibao nimeshindwa. nikifunga nakosa nguvu nakua sioni hata kazi hazifanyiki nakua nalala mda wote. jaman nifanye nini nifunge kama wengine au nile nini usiku ili mchana niwe wakawaida?
Salaam naomba kujua muda wa mwisho kula daku.
Inna Lilah Wa Inna Ilayhi raji'un