jr boy. ndio, zama hizi na zile ni tofauti kidunia ama kidini hali ni ile ile, na Allah hakuwa ni mwenye kusahau kuwa kuna zama zitakuja kuwa hivi zilivyo, lakin alimtuma mtume atufundishe dini hii ambayo ni yenye kuenea mazingira yote na itafanyiwa kaz mpaka kitakapokaribia kiyama. Na kama tutazisingizia zama! Basi ni bora kutoa hizo carpet mpya ambazo ndio kisingizio cha wengi kuliko kukanusha au kupinga sunna za mtume, kwasababu sunna ni zenye kupendeza zaidi mbele ya Allah na kwetu pia kuliko hayo mabusati. Au kuna anayeweza kusema kuwa Allah alisahau au hakujua kuwa zitakuja zama kama hizi?! Bila ya shaka hakuna ambae anayeweza kusema hivyo. Na ametakasika Allah kutokana na yale wanayomsemea kutakasika kuliko mbali. Amesema Allah "pindi zitakapotamka ndimi zenu na itakaposema midomo yenu yale ambayo hamna elimu nayo na mnadhania ni jambo jepesi hali ya kuwa mbele ya Allah ni jambo kubwa" surat Nuur. Jambo ambalo hujui basi fanya research ya kina wala usitoke mbele kupinga ikawa ni sababu ya kuangamia..